Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu;
Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea salama na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Kwanza kabisa nianza kwa kuanza kuwapongeza wote ambao mnapambania Biasha zenu.Mungu awasimamie na kuwapa Ushindi.
Leo naleta mjadala unahusu eneo nyeti sana katika biashara.Eneo hili linahusu Masoko na Mauzo.Nitajenga Msingi wa mjadala kwanza kwa kueleza tofauti na uhusiano uliopo katika Masoko na Mauzo.Kwa lugha nyepesi Masoko yanahusika na Soko lote kwa nyakati zote.Kwa maana ya kwamba kitengo cha Masoko kinahusika na Soko lilivyo sasa hivi na lilivyokuwa jana na litakavyokuwa kipindi kijacho.Kwa upande wa Mauzo inahusika zaidi na Soko kwa wakti uliopo na hasa kwa mteja/wateja waliopo ambao wapo tayari kufanya manunuzi.Hivyo basi mtu wa masoko humtegemea mtu wa mauzo awabadili wateja wawe wanunuzi na wanunuzi wawe wateja.Mtu wa mauzo naye humtegemea mtu wa masoko amletee wateja wawe wanunuzi na wanunuzi wawe wateja.
Katika kampuni au biashara mpya kazi za Masoko na Mauzo zinapaswa kufanywa kwa pamoja.Hii inafanya kuwa na ulazima wa mtu wa masoko kuwa na ujuzi wa mauzo na pia mtu wa mauzo kuwa na ujuzi wa masoko.
Sasa nirudi katika Hoja ya msingi ambayo inajadili mbinu za Kupenya katika SOKO.
Kupenya katika soko ni mchakato unaohusisha kuingiza bidhaa au huduma mpya katika soko.Ni mchakato wa kisayansi ambao unahitaji utaalamu na uzoefu ili uweze kufanikiwa.Mchakato huu hufanyika na kila biashara iwe kubwa au ndogo.Kwamafno mtu anayetaka kufungua duka la aina yoyte huwa naweza kuanza kwa kuangalia wengine wanaofanya biashara hiyo wanafanyaje(Hii kitaalamu inaitwa Competitor analysis) Pia anaweza kuanza kwa kuangalia iwapo eneo analotaka kuweka hiyo biashara kama kuna uhitaji na hiyo huwa inaitwa(Market analysis)
Kwa kutegemea ukubwa na malengo yako ya kibaishara mchakato wako unaweza kuhusisha tu eneo dogo kama sehemu ya mtaa wako au mtaa mzima au kata nzima aua tarafa nzima au hata wilaya na mkoa mzima.Wakati mwingine unaweza kufanya mchakato wako kwa kutazama soko la Taifa zima.
Jambo lingine ambalo ni lzima ulifanye unapotaka kupenya katika soko ni kuielezea bidhaa yako na aina ya changamoto ambazo unalenga kuzitatu.Ni lazima bidhaa au huduma yako iwe ina lengo fulani ambalo watu wako tayari kulipia ili kupata huduma husika au bidhaa husika.Ili kuelezea hili lazima ufahamu vizuri mahitaji ya wateja wako na uonishe na suluhisho lako.
Jambo lingine ambalo lazima ulizangatie unapotaka kupenya katika soko ni kuamua mkakati wa namna ya kufanya masoko na namna ya kufanya mauzo.Kwa mfano moja ya mikakati yetu kama "Masoko" ni kutumia JF kama mojawapo ya majukwaa ya kufikia wateja wetu.Kwa utafiti wetu tumeona tu kwamba uandishi wa makala hizi fupi pamoja na mijadala tunayoshirikiana na wadau humu inatuwezesha kujenga uthabiti katika utoaji wa huduma na kuwafikia wateja wetu.
Unapoandaa Mkakati wa Mauzo na Masoko lazima uuwekee Vipimo vya Mafanikio na uwe tayari kurekebisha Mkakati wako kwakuzingatia mrejesho wa sokoni na wateja.Ni lazima uchagua mbinu za matangazo aina ya matangazo sehemu ambayo utatangaza biashara yako na aina ya wateja ambao unalenga kuwafikia.Jambo la Muhimula kuzingatia unapotaka kupenya katika Soko ni kufahamu kwamba Bidhaa au huduma yako sio kwa ajili ya kila mtu.Biashara yako/huduma yako ina aina maalum na ya kipekee ya wateja ambao ndio unapaswa kuwatafuta na kuwafikia ili waweze kununua bidhaa yako.
Wateja hawa ni lazima wawe na sifa zifuatazo:Kwanza wawe na uhitaji wa huduma au bidhaa yako,Pili wawe na uwezo wa kuinunua bidhaa yako kwa gharama halisi,Na Mwisho waweze kuifurahi bidhaa na huduma yako na kuwa mabalozi wazuri.Huyu Ndio Mteja wa ndoto yako na ndio aina ya mteja ambaye unapaswakulenga kumpata.
Karibu tujadili zaidi namna bora za kuweza kupenya katika soko na kutengeneza faida katika biashara.Tuwasiliane kwa Emai:masokotz@yahoo.com