Fahamu tabia za watu kulingana na magari wanayomiliki

Fahamu tabia za watu kulingana na magari wanayomiliki

halafu wanapenda ugomvi kuliko kula...nadhani ufupi wao unachangia

Sent using Jamii Forums mobile app
We hujakutanna na sisi wenye Landrover 109 AKA Mando!! Pembeni ya engine unaweka vidumu vyako viwili vya petrol na siti ya pembeni naweka gobole langu!! Sipakii abiria kabisa nyuma naweka Jiko langu dogo la gas vichane kadhaa vya ndizi! Hapo safari ni Mwanza to moshi non stop! Disemba ndiyo mwezi wake!!
 
We hujakutanna na sisi wenye Landrover 109 AKA Mando!! Pembeni ya engine unaweka vidumu vyako viwili vya petrol na siti ya pembeni naweka gobole langu!! Sipakii abiria kabisa nyuma naweka Jiko langu dogo la gas vichane kadhaa vya ndizi! Hapo safari ni Mwanza to moshi non stop! Disemba ndiyo mwezi wake!!
[emoji1787][emoji1787]hizi nimepanda sana nikiwa naenda shule utotoni.... in fact ni gari roho ya paka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kuwa serious kidogo unachanganya unachanganya Mercedes benz na Toyota crown au Mark X sehemu moja..Benz umeichukulia poa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Zinaangukia kundi moja...kwa sababu ukifuatilia Mark x,Athlete crown, Nissan fuga au Skyline haya n magari ya kijapan ambayo yana hadhi inayokaribia Mercedes-Benz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apo kwenye PRADO,HARRIER NA V8 umesahau sifa moja hawa wamiliki huwa ukiwatizama kwa njee wakiwa wanaendesha utaona simu iko sikioni sasa nashindwa kuelewa huwa wanaongea na simu mda wote au ndio mapozi ya kuendesha gari..siwaelewagi au wanakua wameshikilia tama kwa kutumia Simu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apo kwenye PRADO,HARRIER NA V8 umesahau sifa moja hawa wamiliki huwa ukiwatizama kwa njee wakiwa wanaendesha utaona simu iko sikioni sasa nashindwa kuelewa huwa wanaongea na simu mda wote au ndio mapozi ya kuendesha gari..siwaelewagi au wanakua wameshikilia tama kwa kutumia Simu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa wanapretend kuwa wao ni wazee wa madili makubwa makubwa kuliko hata MO[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi Wa landrover TDI tunakuaga kipande ya wapi hapo?

"ishi ulaumiwe, kufa usifiwe"
 
Sisi Wa landrover TDI tunakuaga kipande ya wapi hapo?

"ishi ulaumiwe, kufa usifiwe"
Nyie wa TDI rejea wamiliki wa VX na Nissan Patrol...
Lakini zaidi Wamiliki wengi wa TDI ni wakazi wa manyara, huko landanai kubeba wamasai kupeleka mnadani [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amini usiamini, aina ya gari unalomiliki linaweza kuelezea tabia yako kwa kiasi kikubwa..Soma hapa

1. IST, Raumu,Ractis,Nissan Tiida,Note, Mazda Demio,Honda fit,v itz new model.
Wamiliki ya magari haya huwa waangalifku kwa kiasi kikubwa kwani wengi wao huwa ni waajiriwa wapya wapya makazini na mishahara ya kwanza kwanza ndiyo imetumika kujipatia usafiri huu. Watu hawa huforcus zaidi katika mipango yao ya baadae na hawana papara ila kama ni dada anamiliki gari hizi basi jua kahongwa na mume wa mtu. Watu wa kundi hili pia wana mademu zaidi ya mmoja.

2.Passo, Vitz old model, Starle, March,Swift
Mara nyingi wamiliki wa gari hizi huwa ni wapiga dili tu kitaani...Kuoga kwao huwa ni swala la nadra sana.Muda mwingi wanakuwa wakipiga misele ya hapa na pale kujipatia chochote kitu.K undi hili lina bahati ya kumiliki mademu wazuri kinoma.

3.Carina,corolla....Wamiliki wa magari haya huwa ni bahili sana...kuzimikiwa na gari porini kisa mafuta kwao ni suala la kawaida sana na unakuta wana hela mfukoni..vile vile wamiliki wa gari hizi wana mambo ya kizamani au kizee zee.U siombe kusafiri na hawa watu...njiani hawanywi hata maji na mara nyingi wanafahamu sana siri nyingi za wake za watu kwa kuwa mara kwa mara wanatumiwa kama txi

4.Rav 4,Suzuki Vitara na Escudo.....wamiliki wengi wa hizi brands ni wachaga...December kukuta modwl hizi zimeongozana kulekea Moshi ni suala la kawaida sana.

5.Noah, Voxy,Nissan Serena....Wamiliki wa gari hizi hawaishi maisha ya uhalisia wao..Wanajiadai wamenunua family vehicle kumbe wanapiga nazo safari za kukodishwa kisirisiri.

6. X trail, Dualis, Vanguard,Cluger,BMW X3..Wamiliki wa haya magari wanaumri mdogo, wa kati na umri mkubwa na wapo smart sana katika kufanya mambo yao...Wawapo kazini,nyumbani au barabarani umakini kwao ni kipaumbele.Ni wasafi na hawana hela za mawazo.Wakiongea wanakuwa na uwezo mkubwa sana wa ushawishi. Dada kama unatafuta mchumba kundi hili linafaa zaidi

7.Nissan Elgrand, Toyota Alphard
Wamiliki wa magari haya huwa na ustaarabu wa namna fulani...wengi pochi yao huwa nene na wanachepuka sana ila wanachepuka kwa akili. Watu hawa pia hupenda starwhe kama gari zao zilivyo.

8.Mark X,Brevis, Crown,Nissan Fuga,Nissan Skyline,Bmw series,Mercedes Benz...Hapa wamiliki huwa ni vijana machachari wanaopenda vitu vizuri lakini mara nyingi hawafikirii maisha ya baadae.Wachache wao sana hujiwekeza kwa ajili ya maisha ya baadae..watu wa kundi hili hutumia muda mwingi barabarani kufanya ligi ambazo mwisho wa siku hakuna anayewapa tuzo.

9.Prado....Maranyingi hapa utakutana na wazee ambao ni wastaarabu machoni ila moyoni mwao bado wana uchu sana na mabinti hasa wale wa kidato cha tano na sita. Na kama akiwa mmiliki ni mwanamke basi mara nyingi huwa na kaserengeti boy ka kula nako raha.

10.Nissan Navara, VW Amarock.....wamiliki wa haya magari usijenge nao urafiki...hawakawii kukudhalilisha mbele za watu.Ni watu wa kupenda kujiinua kila wapitapo na magari yao.Kwa ujumla hawana ustaarabu wanatawaliwa na masifa.

11.Landceuiser II, Hard top....wamiliki wa haya magari hawana tofauti sana na hapo juu namba 10.Isipokuwa hawa huwa na sifa zaidi na mkibishana kitu kidogo yeye kuchomoa bastola ni swala la kawaida sana.Mara nyingi wanaume wenye magari haya husalitiwa sana na wapenzi wao.

12.Subaru especially Forester.....wamiliki wa magari haya wengi wapo Arusha..wengi wao ni walevi wa miraa,Konyagi,K Vant bila kusahau bangi ya kisimiri japo si kwa wote.Wengi wa wamiliki wa magari haya ni malaya sana na hawawaza maisha yao ya kesho.Wao hujiona ndiyo wajanja wa mji kumbe hamna kitu. Kama wewe ni binti jiadhari sana kupata mume kutoka kwwnye kundi hili.

13.Land cruiser VX, Nissan Ptrol au Safari.....wamiliki wa magari haya wengi wao ni wastaafu wa taasisi fulani fulani zinazolipa vizuri. Huwa wana hekima na busara nyingi ukikaa nao hakika utapata chochote kitu cha kujifunza kuhusu maisha.Ni wakorofi kiasi endapo watakasirishwa.

14.Mazda except demio....wamailiki wa mazda huwa ni wwbishi na hawashauriki...wakishanunua mazda zao zikawatesa spea ndiyo hujuta na kukumbuka ushauri wa awali.

15.Harrier.....wanaume wengi wanaomiliki magari haya hawana furaha.Wanajua wazi kuwa gari wanazoendesha ni gari pendwa za kina mama ila hawana namna wanaendesha tu kwa sababu wameshinikizwa na wake zao kununua aina hii ya gari.Pia wamiliki wa gari hizi hawana sauti kwa wake zao

16.Nissan Murano. Wamiliki wa magari haya wengi huwa na furaha sana wanajiamini kwa kilw jambo wanalolifanya ijapokuwa baadhi yao wanamiliki gari hii kutokana na shikizo la wenzi wao.

17.Altezza....rejea namba 8 na 12

Hizo ni baadhi tu ya tabia zinazoendana na aina ya gari mtu anayomiliki.



Sent using Jamii Forums mobile app

Yallaah! Maskin gari yangu ndio inasifa hizo?
Samahan mdau naomba kujua Source ya Taarifa yako umeitoa wapi?
Ni timu ipi ya wataalam ilifanya utafit ikaprovide those RESULTS.
Failure to do that.
NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK............
 
Yallaah! Maskin gari yangu ndio inasifa hizo?
Samahan mdau naomba kujua Source ya Taarifa yako umeitoa wapi?
Ni timu ipi ya wataalam ilifanya utafit ikaprovide those RESULTS.
Failure to do that.
NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK............
Kwanza ningependa kujua gari yako inaangukia kwenye kundi namba ngapi.

Pili hii ni research halali niliyoifanya mimi
Methodology iliyotumika ilikuwa observation...

Nimefanya uchunguzi kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kukaa karibu na watu wenye magari tofauti tofauti...nilipojaribu kuoanisha tabia za watu kadhaa wanomiliki aina fulani ya gari, nilibaini wanafanana.
So research hii kwa hapa Tz haijafanywa na mtu mwingine ila mimi tu Boeing 747.
Mtu mwingine akija na utafiti kama huu atanitumia mimi kama Reference.

Boeing 747, (2019). Fahamu Tabia za Watu Kulingana na Aina ya Gari Analomiliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom