Fahamu utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua

Fahamu utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Licha ya kuwa na wafuasi chungu nzima kutoka mataifa tofauti duniani, pia alikuwa na wakosoaji wengi vilevile kutokana na mafunzo ya kanisa lake.

Hii leo tunakuangazia kuhusu utabiri aliotoa na utata uliomzunguka.

Maji ya Upako
Mwaka 2013 hamu ya maji ya upako {Maji matakatifu} ya TB Joshua yalizua mkanyagano uliosababisha vifo vya watu wanne katika kanisa moja lililopo katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Maelfu ya watu waliokimbilia maji hayo 'matakatifu waliamini kwamba yana uwezo wa kutibu.

Chombo cha habari cha AFP kiliripoti kwamba mkanyagano huo ulitokea wakati waumini walipoanza kusukumana kwenda kupata maji hayo mbele ya kanisa hilo.

Wengi walimkosoa TB Joshua baada ya tukio hilo lakini maafisa wa polisi nchini Ghana wanasema ni vigumu kutupia mtu lawama.

Msemaji wa polisi Freeman Tetteh wakati huo alisema kwamba watachunguza kubaini ni nani wa kulaumiwa.

Mwaka 2014, paa la nyumba moja ya wageni iliopo ndani ya kanisa la SCOAN la muhubiri huyo katika eneo la Ikotun -Egbe mjini Lagos lilianguka .

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuanguka kwa jumba hilo ilifikia 115, ikiwemo raia 84 wa Afrika Kusini kulingana na waziri mmoja wa taifa hilo, Jeff Radebe.

TB Joshua alilaumiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa jumba hilo.

Alidai kwamba baadhi ya watu walitaka kumuua kupitia tukio hilo.

Wakati huo, rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitembelea kanisa hilo na kuamua kuanzisha uchunguzi kuhusu kile kilichotokea.

'Miujiza yenye utata'
Lakini mzozo uliokuwa ukimzunguka muhubiri huyo haukuishia hapo, kwasababu wengi pia walimkosoa kuhusu miujiza yake mingi katika mikutano yake.

Mwaka 2017, Chris Okotie, muhubiri Maarufu nchini Nigeria , alimshutumu Joshua kwa kufanya 'uganga'.

Lakini waziri wa zamani wa usafiri wa ndege, Femi Fan Kayode ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa TB Joshua alimtaka Okotie kuacha kumshambulia Joshua na badala yake kuitisha umoja katika kanisa hilo.

Wakosoaji wake wa Kikristo wamekuwa wakisema kwamba mbinu anazotumia TB Joshua haziendani na zile zilizopo katika bíblia.

Baraza la Kanisa la Pentecostal nchini Nigeria halikukubali kanisa la Joshua kuwa chini yake.

YouTube yampiga marufuku TB Joshua
Mwaka 2021, mtandao wa Youtube uliondoa runinga yake ya Emmanuel TV katika mtandao huo kutokana na matamshi ya chuki baada ya kanda moja ya vídeo ya muhubiri huyo akijaribu kutoa mapepo katika miili ya wapenzi wa jinsia moja kuzua hisia kali.

Baadaye mtandao wa Facebook uliondoa kanda zote za vídeo za ibada hiyo.

Ebola Afrika Magharibi
Wakati mlipuko wa Ebola ulipozuka Afrika ya magharibi, serikali ya jimbo la Lagos iligundua jinsi idadi ya watu ilivyoongezeka katika kanisa la TB Joshua, ikalazimika kuwaomba raia kutowapeleka wagonjwa wa maradhi hayo katika kanisa hilo ili kuzuia usambazaji wa ugonjwa huo.

TB Joshua alikubali kusimamisha baadhi ya mipango ya kutibu ya kanisa hilo lakini akatuma chupa 4,000 za maji ya upako nchini Sierra ili kutibu ugonjwa huo.

Utabiri wa TB Joshua

Muhubiri TB Joshua kama alivyo maarufu kwa utabiri anadaiwa kubashiri kifo cha Michael Jackson, Kupotea kwa ndege ya Malaysia MH370 na nyenginezo.

1. Michael Jackson
Kuhusu kifo cha Michael Jackson, Aliwaambia waumini wake kwamba ''umaarufu wangu ni mkubwa kwasababu watu wanajua niko kila mahali''.

''Naona kutatokea kitu kikubwa kwa nyota huyo ambaye ataondoka na kwenda mahali ambapo hatorudi tena na najua siku atakayokwenda''

Na baada ya kifo cha Michael Jackson , TB Joshua alisema kwamba huo ulikuwa utabiri alioutoa miezi sita iliopita.

Lakini watu wamekuwa wakikosoa mafunzo yake ya utabiri na kudai kwamba amekuwa akitumia fursa za matukio kujipigia debe.

2. Virusi vya Corona
Mwaka uliopita , wakati mlipuko wa corona ulipoanza , TB Joshua alisema kwamba virusi vya ugonjwa huo vitaisha mwezi Machi wakati wa ibada moja lakini baada ya virusi hivyo kuendelea kuuwa watu, alienda mlimani kufanya maombi ili virusi hivyo viondoke.

Lakini licha ya utata unaomzunguka , waumini wamekuwa wakijaa katika kanisa lake ili kuomba mwongozo.
 
Ngoja nifanye kwanza kazi kidogo huu uzi ntaurudia. Kuna clip inasambaa anasema Angeles wamemnyakua kama roketi akawa anaiangalia dunia kwa chini (means hakufa)

NB: Nachoamini mimi ni kuwa witch doctors wameibukia kwenye upastor so ni mwendo wa kupiga hela. Devil come n collect your people[emoji134]
 
Kwanini uuze karama uliyopewa bure na Mungu, hayo maji ilibidi ayatoe bure kama roho mtakatifu amemuongoza atumie maji katika maombezi basi ayaombee bure na awape watu bure, hiyo ya kuuza maji na mafuta haipo sehemu yoyote kwenye biblia, akaeleze vizuri alupewa maagizo na nani.
 
Kwanini uuze karama uliyopewa bure na Mungu......hayo maji ilibidi ayatoe bure kama roho mtakatifu amemuongoza atumie maji katika maombezi basi ayaombee bure na awape watu bure.......hiyo ya kuuza maji na mafuta haipo sehemu yoyote kwenye biblia, akaeleze vizuri alupewa maagizo na nani
Huyu mzee hauzi maji ndugu.tatizo hamfatilii wala hamumjuia Bali mnafatilia wapigaji
Huyu mzee anampa mtu bure halafu mtu anayageuza faida anaenda kuuza
Kosa la nani hapo?
Ifike mda mkae kimya kujiepusha na hatia za ulimi.mmemtukana sana huyu mzee na wala hamumjui Bali mnafuata maneno ya vichochoroni na blog uchwara na wapinga kristo.usiokote maneno ya watu na kuyaendeleza
 
Kuna sauti niliisikia ya balozi wetu nchini Nigeria mzee Ben Bana anasema, lazima wampeleke kwenye sehemu aliyozaliwa ili mkuu wa Kimila wa Igbo ndio athibitishe kifo chake autangazie umma.


Sasa nikajiuliza, huyu mtu wa kiroho na mambo ya kimila wapi na wapiii!!!!!?
 
Pamoja na maelezo ya mafundisho na miujiza yoooooooooote tunayoyasoma na kuambiwa kuhusiana na Yesu lakini bado walimkamsta wakampa mateso kisha wakamuua, ije kuwa huyo TB Joshua!!!!!?

Wapo baadhi ya watu wasio amini uwepo wa Mungu na wanajipambanua wazi wazi hadharani. Imani ni baina ya nafsi ya "mtu", i.e mmoja mmoja na huyo anayemuamini kwa maana ya aidha Mungu au vinginevyo.

MUHIMU; Maneno yangu siyo sheria
 
Pamoja na yote hayo tb joshua ndie mtumishi aliekua anasaidia zaidi watu,he had a lot of humanitarian activities nchi nyingi zaidi ndani ya afrika na huko ulaya
At last ungemuappreciate kwa hilo manake hao unaoamini ndio wa Mungu kweli mbona hatuoni charity work zao?hujui amri kuu aliyoiagiza Mungu ni upendo?na upendo si maneno bali matendo,kama tb joshua alionyesha upendo kwa matendo kama ipasavyo bible nadhani he is the best among hao ambao ni wa Mungu kweli na wala hawaonyeshi upendo bali wanajilimbikizia mali wenyewe!
Biblia inasema zaburi ya 82,ninyi ni miungu bali mtakufa kama wanadamu na ndo hiko kimetokea kwake,kama alikua wa shetani au wa Mungu andiko limetimia amekufa kama mwanadamu
Let him go,his legacy will forever live to those he touched!
Kama kuna cha kuchukua kikubwa kwa tb joshua ni kupenda watu,kuwahurumia na kuwa non judgemental!
Let love lead my brother✌❤
 
TB Joshua alipata umaarufu pengine ni kweli alikuwa anatumia NGUVU ZA MUNGU au nguvu za giza, sijui.

Watu walipona, viwete walitembea na wengi wenye shida walifunguliwa, kwa vile hakuna aliyekiri kuponywa naye tuyaache hivyo hivyo, labda atokee wa kutoa ushughuda.

Mbinu zake alizotumia sijui kama zipo kwenye Biblia, labda from those pages removed from the Bible. Upo wakati alikuja bongo peku, just imagine

Na iwapo alitumia nguvu za giza huwa zina malipo pia, waulize waliotupa punje kule tunduma au wale wa wahunzi huru, lazima ulipia mwisho wanataka kutoka kwako sadaka yenye uchungu na ukishindwa ipo adhabu pia muulize Mshana Jr kilichomfanya auze kilinge.

So this man of god alijua yake na yakamkuta hivyo.

Nilikuwa mfuatiliaji wa mafundisho yake sometimes nikaja kuachana nayo pia.

All in all let TB JOSHUA be where our God will like him to be.
 
Kitu nimejifunza mpaka sasa ni kukaa mbali kabisa na waumini wa hawa "mitume". Ni watu hatari kwa afya yako kiujumla.
 
Back
Top Bottom