Haya masuala ni ya kiimani zaidi, ni vizuri kumuacha kila mtu akaamini kile anachotaka,kuna watu ninawafahamu wamelala hospitali miaka na miaka kwa stroke lakini walipona with a single touch from TB Joshua na mpaka sasa wanaendelea na maisha vizuri, kuna mwingine nilisoma nae alipata kichaa ghafla tulipokua chuo mwaka wa pili, na amepelekwa kwa wataalamu wa afya ya akili mpaka nje ya nchi hakupona, familia ilirudi nyuma wakaamua kuwa wanamfungia ndani tu for more than 4years, baadae watu wakawashauri wamuhangaikie kiroho, walipita makanisa mengi hapa TZ hakupona, mama yake akatuomba tumsaidie kufanya fund raising aende kwa TB Joshua, tulichangishana kila kona wakaenda, with a single touch the lady is doing great na anafanya kazi UN kwa sasa wala huwezi jua kama aliwahi kuwa kichaa
Mfano wa mwisho ni dada mmoja jirani na ninapoishi alijifungua mtoto mwenye matatizo ya akili, wanaita mtindio wa ubongo, huyu dada amehangaika na mtoto mpaka India, mwisho wa siku alikata tamaa, last year mtoto wake alitimiza umri wa miaka saba, akaaamua kumpeleka kwa TB Joshua,hivi tunavyoongea yule mtoto anasoma shule moja na wanangu tena huwezi jua kama alizaliwa na matatizo, very intelligent boy
Mimi niseme tu swala la imani huwa sizungumzi kwa sababu kila mtu huwa anaguswa kwa namna yake, na pengine huwezi kuamini mpaka upitie situation fulani itakayokufanya uamini
Sio wajinga, kuna watu wanapitia mapito mengi sana na wamehangaika kila kona ila wamepata msaada kwa huyu mtumishi. Mshukuru Mungu hujawahi kupitia mapito au mahangaiko ya namna hiyo na muombe Mungu pia akuepushie