Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

kwa hii govt inayolia kila siku haina hela, hatutazinguana mbeleni? mf pension funds, kandarasi, wazabuni, local bank nk
hamna mkuu zoezi Zima linasimamiwa ki uadilifu sana banki kuu. Hivo ni ngumu serikali Ita default katika kulipa.

Endapo uchumi ukilega lega kama yaliyowakuta ugiriki ndo serikali inaweza kushindwa kulipa. Ila so far kwa Tanzania tupo safe.

Lakini ulichosema ni sahihi kabisa kwamba endapo nchi ikifilisika basi inaweza kushindwa kulipa. Hiyo ni kweli na ndicho kinachotokea ugiriki sasahiv. Lakini kwa Tanzania hilo sio rahisi sana maana hata banki kuu nadhani wapo makini sana kwenye Hili.
 
Mkuu Davion Delmonte Jr. samahani kama nitakua narudia kuuliza kile ulichoelezea ningependa kujua kwa ufasaha zaidi ni namna gani au utaratibu ukoje ile uweze kununu hizo bonds (yaani kama kuna kujisajili kwanza mambo yakoje).
swali la pili ni je mfumo huu ni tofaut na ule wa UTT na mifuko yao au ni sawa??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Davion Delmonte Jr. samahani kama nitakua narudia kuuliza kile ulichoelezea ningependa kujua kwa ufasaha zaidi ni namna gani au utaratibu ukoje ile uweze kununu hizo bonds (yaani kama kuna kujisajili kwanza mambo yakoje).
swali la pili ni je mfumo huu ni tofaut na ule wa UTT na mifuko yao au ni sawa??
kama unataka kununua bonds pindi BOT wanavo announce kuna form zinaitwa BOT-FORM GBI ambazo utadownload kwenye website yao. Maelezo yote yapo pale namna ya kuijaza. Kama unaona inachanganya kidogo unaweza ukapitia kwa ma broker japo yaweza kuwa na charges lakini kama ukiamua mwenyewe inawezekana pia.

suala lingine ni kwamba UTT na bonds ni vitu tofauti kabisa ntalielezea hilo kwa mapana kwani kunachapisho la uelewa juu ya UTT.
 
UTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI

Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.

i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)

Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na banki kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.

Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.

Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji;
i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.

ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.

iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.

iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)

Soko la treasury bills
Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;

a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.

b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.

Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).

Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks

Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.

Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)

Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.

Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.

Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.

Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo;
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N

F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365

Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%

Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.

Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.

Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.
Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.

Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu..

Your calculation looks good and attractive on paper, but I'm afraid in real world kweli unaweza kununua treasury bills ya miez mitatu ya face value of 100 million, ukanunua kwa 75million..... Actually sijawahi kununua dhamana za serikali mimi ni graduate wa finance ndo nimemaliza mwaka huu but niko very interested kwenye financial securities nitakapokuwa vizuri nitahusika sana DSE, nimefurahi sana kuona huu uzi wako... Yan umeundikika kimadesamadesa hadi raha... Ila tu nimeshangaa kuona mfano wako wa treasury bill ambayo ni risk free and short-term hlf inatoa return kubwa... Wengi watavutika ila in real word inaweza isiwe profitable sana kama mfano wako maana from wat I know watu huwa wanainvest kwenye bonds(defensive securities) ili kupunguza risk iliyoko kwenye stocks(aggressive securities), hivyo sikutarajia sana kuona return kubwa kiasi hicho inatoka kwenye treasury bills... Ila inawezekana ikawa sahihi maana mimi ni mgeni sana kwenye soko la dse
 
Sema vile watu hawajui.. Lakini faida za kuwa na hizi financial assets ni kubwa mno. Kuliko unavoweza kufikiri

Mkuu nimezoea kuona nmb...crdb...swala...kenya airway wakiuza hisa...je hizi hisa sijui unaziita bond za serikali zinatofautiana vipi na hizi za nmb...crdb and the alike???
Je nikitaka nunu hisa za serikal ntazipata wapi??? Wapi wanatangaza...ntajua vipi kwamba mda flani wanauza???
 
ulichosema ni sahihi kwamba inflation na kupanda kwa dola kunaweza kushusha thamani ya uwekezaji wako. Lakini ukiangalia kwa upande mngine hiyo milioni 10 kama ungeiacha bank ungeumia zaidi kwa sababu hiyo faida ya 3 milioni siyo haba.

Japo nipo nje ya mada....kwa ujuzi wako kwa nn hisa za NMB zinaporomoka kwa kasi??? Tokea 4000 mpaka 2700 !!! Nini sababu??? Na kipind hiki ni kipindi rafiki kwa ununuzi wa hisa??
 
Back
Top Bottom