Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

Hapo mimetoa mfano, lakini kama ukifuatilia kwenye zabuni za BOT ni kwamba faida itatategemea ile discount ya kununua treasury bills.

Ikiwa unapata discount kubwa basi ujue faida unayopata nayo itakuwa kubwa. Nakushauri u visit website ya BOT Kuna matokeo ya treasury bills auction zilizofanyika
 
Hisa na dhamana za serikali ni vitu viwili tofauti. Kwa Tanzania makampuni ndiyo yanatoa hisa na serikali inatoa bonds na treasury bills kupitia BOT.
 
Very good and educative post ....
Nina rafiki yangu anayeishi US ..., yeye aliwekeza haraka sana ktk uuzaji hisa wakati ule TBL , Twiga Cement , Kenya Airways na makampuni mengine yalipoji register na DSE ...

Kwa kipindi cha miezi 6 tuu tangu awekeze, alipata faida ya Tzs 30 mil alipoziuza hisa zake alizowekeza ktk solo la hisa .. Huyu mtu alinihamasisha sana kuwekeza DSE tangu wakati huo .., ilikuwa miaka ya 2005 kama sikosei ...

So Davion, keep teaching us broo about huu ubepari per see ...
 
Wakubwa kwenye kilinge VP unaweza kunielewa kuhusu hisa ikoje na mini NASA kwenye Chanel ya biashara thanks then
 
chapisho lijalo ntazungumzia hisa na ntafanya kama ulivyosema kufanya comparison ya hisa na bond.
Mwanangu inabidi utueleweshe inamaana katika iyo face value inakuwa constantly au ni makubaliano kulingana ukuuaji wa uchumi wa nchi au? Maana inawezekana ukapata pungufu ya 33.33%
Labda ungetuelewesha kwamba inawezekana ikawa pungufu ya iyo amount au ungetuelewesha kwamba kulingana na kiwango kikubwa cha mtaji ulio nao ndio unapata iyo 33.33%. Maana usije ukakurupuka na iyo million 10 unaenda kuweka mwisho wa siku unakuja kupata 10% ambayo ni karibu na fixed a/c
Kingine kodi ya serikali wanakata asilimia ngapi? Kama ni 18% au pungufu yake
 
Mkuu kama kuna Thread inayozungumzia Shares, Bonds na Treasury Bills
Ungetuelewesha apo, maana vinatuchanganya sana
 
Tatizo bongo bhaaana uhaminifu ni mdogo saaana afu hakuna utaratibu wowote wa kurejesha hizi pesa for the case of any janga....

Naona deci... sijui nin watu wanalia tu na hata kifuta jasho hakuna... ingawaje ilikua inajulikana na serikal... si use... huu.

Baba nyie anzeni mi mpaka nipate pesa ya kuchezea.. nitatoa sadaka

Sent from "La -Vista"
 
Nimejaribu kufatilia katika website ya BOT. Lakini naona kwenye minada ya BOT kalibia ile asilimia inaanzia 9 kushuka chini. Naomba ufafanuzi apo kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…