Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali (Treasury Bills & Bonds)

Nenda kwa stokebrokers siyo benki. Hapo utapata usaidizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa mkuu na unachokiongea ndio nimekumbana nacho , nilimuuliza swali kwa uwezo wangu kifedha kama nikinunua bonds kwa shilingi Milioni 1 nitanufaikaje kwa option ya siku 30,90 au mwaka mzima ( Hawakuweza hata kunijibu kwa sababu hata interest hawazijui )...


Hivyo basi naomba unisaidie mchanganuo kwa kuegemea hicho kiasi nilicho suggest

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Mkuu kuna post nieleza tofauti ya bills na bond kwa time frame pamoja na interest!..jaribu kucheki post za nyuma.
Kufaidika itategemea ulikuwa successful kwa bid price ipi baada ya kushiriki kwenye mnada.
Mfano; kama umefanikiwa kupata discount ya Tsh 100 ya serikali kwa 70.0000 ina maana kama face value yako ni 1m hapo utatoa 700000/= ina maana tayari una faida ya 300000/= amabayo italipwa on maturity date! hapo ni kwa bills ila kwa bond mbali na hio faida kuna interest pia inategemea umewekeza kwa miaka mingapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkuu hiyo Faida ya 300,000 ni kwa kipindi cha muda gani???


Naomba unichambulie kwa kipindi cha Siku 30 ...


Samahani kwa kukuuliza sana

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Asante sana mkuu hiyo Faida ya 300,000 ni kwa kipindi cha muda gani???


Naomba unichambulie kwa kipindi cha Siku 30 ...


Samahani kwa kukuuliza sana

Sent From My Nokia Ya Tochi
Boss huo ni mfano tu,,nimesema faida itategemea kama umewekeza either kwenye bills or bond pamoja na discount uliyopata baada ya kushiriki kwenye auction na kushinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Leo nimeshinda nauchimbua his u Uzi samahani naomba unieleweshe hiyo tbills minimum ya 500000 kwa mafungu ya 10000 ,Sijaelewa vizuri

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Mkuu nimeingia kwenye website ya BOT na kukuta hii action Bill ya Mwezi March mwaka huu ila sijaelewa kutafsiri hilo jedwali

Sent From My Nokia Ya Tochi
 

Attachments

  • 1503510359238.png
    24.5 KB · Views: 152
Haki ya mungu Nikielekezwa hizo documents mbili nilizopost na kuzielewa wallah najiona sehemu baada ya Miaka kadhaa nitakuja humu na ushuhuda ....


Tangu Jana hiyo website ya BOT nadhani Mimi itakuwa nimekuwa kiumbe kilichoitembelea zaidi ..

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Mkuu nimeingia kwenye website ya BOT na kukuta hii action Bill ya Mwezi March mwaka huu ila sijaelewa kutafsiri hilo jedwali

Sent From My Nokia Ya Tochi
Hizi ni result za bills ya hio date iliyotajwa ukiangalia hapo kwenye number of bids(yaani idadi ya walioshiriki kwenye auction) then kuna successful bids (hawa walioshinda) then kuna highest na lowest bid price( hizi ndo range ya discount walizoomba washiriki) then kuna minimum successful price( hapa ni baada ya bank kuangalia ni price gani itawafaa kulingana na discount za wawekezaji walizoomba ili wasipate hasara) then kuna hio weighed average price(WAP) hii ndo niliyosema post zilizopita kama ulifanya kwa non-competitive bidding hio price iliyooneshwa ndo discount/bid price yako.

Sasa ukiangalia vizuri watu wengi hawawekezi kwenye siku 35 and 91
Ila kuanzia 182 and 364 ndo angalau watu wanawekeza kwa sababu price inakuwa chini kidogo na wanatengeneza faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…