Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Kuna kitu nmeona kinajadiliwa hapa kuhusu ground beam, wengi wanasema eneo lenye kichanga halihtji ground beam, lakini kama ukifanya soil investigation kawaida ya hali ya udongo huwa inabdlika kulingana na mda.. Pia udongo huwa ina tabia ya kujongea. Eneo unalojenga wewe inawezekana kukwa na mchanga lakini mita 10 toka ulipo kukwa na udongo wa aina nyingine.

Nini umuhimu wa ground beam. Kazi kubwa ya ground beam n kuzuia un equally settlements (kutitia kwa nyumba kusikokua sawa) unapoeka mkanda au ground beam unafanya nyumba yako ititie kwa pamoja hvo kuzuia nyufa zisitokee kwenye nyumba..


Ushauri wangu ni muhimu kueka ground beam regardless ya aina udongo sababu tabia ya udongo huwa haitabadiliki...
 
Hapa ndiyo tutaelewa concept ya Jenga Uza. Ni nyumba za kiwango duni sana. Mjenzi amatumia minimum amount ili aje apate faida kubwa akiuza. Likipita tetemeko dogo tu,nyumba yote inageuka kifusi.
 
Nami pia nimo katika tasnia hii ya ujenzi, mtoa maada kaeleza vizuri ingawa vipo ambavyo kateleza kidgo lakini kwa vile anasema yeye ni fundi basi anahitaji pongezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni kosa la Architecture na Mara nyingi hua inatokea kwa mtu ambaye anajenga vitu vikubwa lakini anataka mafundi wa bei rahisi.

Mfano katika majengo kama hayo lazima uweke duct za kufanya yote hayo...
Ushawahi kujiuliza kwann maghorofa mengi ya uswahilini yanaonyesha bomba za maji kwa nje, bomba hazipaswi kuonekana kwa nje ya jengo iwe ni storm water, grey water n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kwamba muongo, jengo ili likamilike inabidi watu wote washirikishwe
Architecture
Engineer
Electrical
Plumber
M.E.P n.k
Wengi wanajenga lakini hawashirikishi hao watu, hii naongelea majengo ya ghorofa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam,
Kwenye mchango 75mm ni nyingi mno, Sifa moja ya Mchanga hua ukifanya settlement basi hua mara moja tuu,
Tofauti na clay soil
Ndo maana treatment za kujenga sehemu yenye clay soil ni tofauti na sehemu yenye sand

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nylon ni kwaajili ya kuzuia unyevunyevu.

Kujenga sehemu yenye mfinyanzi yahitaji umakini sana. Ogopa sana ule Udongo unaopasuka ukiwa mkavu, ndiyo chanzo cha nyufa.

Kichanga ni udongo ambao hauna madhara na unaweza hata usiweke beam
Hapa niko tofauti na wew me nimesurvey maeneo mengi ya pwani kuanzia Kibaha kuja hadi Dar ambako kuna udongo wa kichanga, nyumba nyingi zikijengwa huwa naona zina ufa inaweza isiwe kubwa sana ila lazima unakuta kuna viufa kwenye msingi lakin maeneo ya Kaskazin kama K'njaro na arusha sijawahi kuoa hivyo viufa kama nakosea nirekebishwe
 
nondo ndogo za kufunga nondo kubwa au bangili hizo ndo zina kazi ya kuzuia cracking kitaalam
Nimekusoma mkuu. Naomba unishauri au maoni ktk hili;
Kuna nyumba ndogo yenye chumba na sebule na choo/bafu. Urefu m8 na upana m5, msingi wake umewekewa nondo 2 (zimelazwa)pamoja na hizo stirrups. Udongo wa eneo ni aina ya kichanga.
 
Nimekusoma mkuu. Naomba unishauri au maoni ktk hili;
Kuna nyumba ndogo yenye chumba na sebule na choo/bafu. Urefu m8 na upana m5, msingi wake umewekewa nondo 2 (zimelazwa)pamoja na hizo stirrups. Udongo wa eneo ni aina ya kichanga.
Nondo mbili?? Nondo mbili wamezifungaje hao mafundi..
Kitaalamu ground beam au beam yoyote inahtaji angalau nondo 4 za kuanzia mm 12,kwenda mbele.. Kwa nn ziwe nondo 4..
Beam nyingi znazosukwa huwa ni mstatili au mraba.. Na mara nyingi hayo maumbo huwa yana pembe 4,kitaalamu kwenye pembe ya beam ndo eneo ambalo linakua zaidi lipo hatarini kwenye kupatwa na nyufa. Hvo wataalam wanshauri angalau kwenye kila pembe ya Beam ipate nondo moja. Hvo ukiwa na beam ya mstatili, au Mraba lazma uwe na nondo 4 znazocover eneo lote la beam..

Sababu ya pili ni kuwa ili uwezd kumaintain shape ya beam yako, pamoja na cover (uwazi unaoachwa kati ya outer surface ya beam na nondo) unatakiwa uekwe nondo 4 ili kila pande iwe na cover.. Sasa unapoeka nondo mbili inakua vigumu kuipata shape ya pembe 4 ya beam yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani mkuu kwa maelezo yako. Si unajua wa mafundi mtaani mambo yao.
Kama hutojali unaweza weka picha za hizo beam mkuu?
 
Naomba kujua:-

1. mfuko mmoja cement ya kawaida unawezajengea tofali ngapi kupandisha boma kwa kutumia tofali za block za nchi 5?

2.Naomba pia kujua mfuko mmoja cement ya kawaida unawezajengea tofali ngapi za msingi za block za nchi 6?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu beam yenye nondo 3 mtaalam?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…