Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Mleta mada nakupongeza kwa kuipenda kazi yako. Ila nakuomba pia uwe unatumia ushauri wa wataalamu wa ujenzi. Namaanisha uchote maarifa kwa Architects, Engineer na Quantity Surveyor. Mie nimesoma ujenzi na nimepitia maelezo yako naona kama hayajajitosheleza pengine ni kutokana na ufahamu wa kitaalamu. Kwa mfano, nyumba sio lazima iwe na ground beam, kuna sababu hupelekea iwepo au isiwepo.kwa hiyo wakati mwingine mnaongezea gharama za ujenzi zisizokuwa za lazima kwa kigezo/kauli mbiu ya nyumba imara

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaah n kwel kabisa, hapo kwenye kumwaga zege chini wakat wa kuanza msingi huwa mafund wengi wamekariri tu ila ukwel ni,kuwa kutanguliza mchanga angalau inch 3 hv ni bora zaid kulko hyo zege.

Mafundi wanaongezaga garama tu il wanufaike, ila profeessionally hamna mantik yoyote
 
Yaah n kwel kabisa, hapo kwenye kumwaga zege chini wakat wa kuanza msingi huwa mafund wengi wamekariri tu ila ukwel ni,kuwa kutanguliza mchanga angalau inch 3 hv ni bora zaid kulko hyo zege..
Mafund wanaongezaga garama tu il wanufaike, ila profeessionally hamna mantik yoyote
Kuongezea nyama hapo( kwa idhini ya mleta mada) hiyo issue huja kutokana na type ya udongo wa eneo husika. Bila shaka akifika kwenye kipengele hicho ataelezea kwa undani, naamin huwezi mwaga mchanga 75mm sehem yenye mchanga ili uanze ujenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaah n kwel kabisa, hapo kwenye kumwaga zege chini wakat wa kuanza msingi huwa mafund wengi wamekariri tu ila ukwel ni,kuwa kutanguliza mchanga angalau inch 3 hv ni bora zaid kulko hyo zege..
Mafund wanaongezaga garama tu il wanufaike, ila profeessionally hamna mantik yoyote
Inategemeana na tabia ya Udongo husika. Si hivyo tu kuna Sehemu tunalazimika kusuka nondo
 
Kuongezea nyama hapo( kwa idhini ya mleta mada) hiyo issue huja kutokana na type ya udongo wa eneo husika. Bila shaka akifika kwenye kipengele hicho ataelezea kwa undani, naamin huwezi mwaga mchanga 75mm sehem yenye mchanga ili uanze ujenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaa ni sawa, huwez mwaga mchanga sehem yenye mchanga na ndomana nimeeleza kuwa cha kutangulia chini kabla ya kuanza kujenga tofal ni mchanga na sio zege..

ufund wa kuanza na zege chini hauna mantik katka uimara ws nyumba regardless type of soil
 
Unaelewa nini juu ya "U bar" ?
 
Inategemeana na tabia ya Udongo husika. Si hivyo tu kuna Sehemu tunalazimika kusuka nondo
Sawa, ila naomba Nieleweke kuwa ninachokikataa ni Zege la chin kabda ya kuanza kujenga tofali/mawe ya msingi na SIO Beam ya zege inayofungwa na nondo ambayo inamalizia level ya msingi
 
Kwanini nyumba zetu huwa zina majiko ndani lakini hazina sehemu za kutolea moshi nje?! Tangu kwa archtecture mpaka kwa civil engineer.
Kwanini mjenzi haachi maeneo ya kuweka vyoo, anamwaga zege kisha anakuja kutindua zege, wakati alifahamu tangu mwanzo kutawekwa mfumo wa maji machafu, na hata maji masafi, kwanin yasiwekwe wakati wa ujenzi wanasubiri jadi nyumba inaisha wanaanza gharama za kutindua zege na ukuta?!
Mnaposoma huwa hamfundishwi au ni ujinga wa wataalam wetu?!
Hilo la matoleo ya vitu vya maji machafu, ni kweli wamekalili, wanasubiri zege limwagwe ndio waanze kubomoa.
 
Mkuu inasemekana msingi unaojengwa kipindi cha mvua huwa imara sana, kuna ukweli ktk hilo?
 
Hilo la matoleo ya vitu vya maji machafu, ni kweli wamekalili, wanasubiri zege limwagwe ndio waanze kubomoa.
Ili kuepuka hili unaweza kubadili fundi unaemtumia. Atakuwa hajitambui
IMG_20190115_215813_280.jpg
 
Sawa, ila naomba Nieleweke kuwa ninachokikataa ni Zege la chin kabda ya kuanza kujenga tofali/mawe ya msingi na SIO Beam ya zege inayofungwa na nondo ambayo inamalizia level ya msingi
Mkuu naomba ujibu swali langu nililokuuliza hapo juu
 
Mkuu Pmoses95
ebu naomba tips ya kujenga msingi kwenye ardhi yenye udongo wa mfinyanzi na kichanga, vile vile naomba unieleweshe umuhimu wa kuweka nylon? kwenye msingi wa nyumba, wengine tupo kijijini na tuna tamani kujenga imara
 
Nylon ni kwaajili ya kuzuia unyevunyevu.

Kujenga sehemu yenye mfinyanzi yahitaji umakini sana. Ogopa sana ule Udongo unaopasuka ukiwa mkavu, ndiyo chanzo cha nyufa.

Kichanga ni udongo ambao hauna madhara na unaweza hata usiweke beam
 
Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :

1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, Hakina utaenjoy service yangu.
0655173113

UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI.

Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP.

sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.
Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk Eneo LA slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.
Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0655173113
Asante. Nimejifunza mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom