Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Ndio Maana huwa tunamchukua Fundi mchundo unampeleka site Na powder anachora kulingana na maelekezo yako. Ili kuepuka hizi gharama zenu.


Mfano, Mimi ninawakubali Sana Themibuider kwa Ramani nzuri na muonekano WA kuvutia WA Jengo, Ila bei yao Sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna ramani ya fundi ambae hajui darasa inaweza kua proper na Haina vigezo vya kupitishwa na watu wa mipango miji unless unajenga kwenye squatters
Na lazima itakua mbaya au photo copy ya raman za zamani
 
Ahsante kwa mawazo
Hakuna ramani ya fundi ambae hajui darasa inaweza kua proper na Haina vigezo vya kupitishwa na watu wa mipango miji unless unajenga kwenye squatters
Na lazima itakua mbaya au photo copy ya raman za zamani
Ahsante Sana mtalamu, tunajenga kulingana na uwezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :

1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, Hakina utaenjoy service yangu.
0655173113


UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI.

Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP.

sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.
Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk Eneo LA slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.
Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0655173113
Safi unatufungua wengi. Nimependa ufasaha katika uandishi wake, kichwa chako kimetulia. Mungu akijaalia nitakutafuta hivi karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru nimekukuta online mtoa mada.
Natarajia kuanza ujenzi lakini nilitaka msingi wa jamvi, msingi ni wa nawe na fundi kaniambia zinahitajika trip 10 za mawe kwa ajili ya msingi huo.

Naomba msaada wa kujua je huu mzingi wa jamvi ya mawe, kokoto, molarm, mchanga na cement hautasababisha kupata mpasuko??

Udongo wa eneo ni mfinyanzi na ni eneo lililokuwa likitumiwa kwa kilimo cha mpunga.

Kiwanja hicho kiko Musoma na ukubwa wake ni sqm 1023.

Naomba ushauri wako mkuu. Nifanyeje au nijengeje msingi ambao hautasababisha nyumba kupata mipasuko??

Ahsante sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Building materials used pia huleta tofauti.
YUpo ambae atatumia bati la mchina au nondo za kichina
Yupo ambae atatumia vigae mwengine bati hawa ni tofauti.
YUpo ambae atatumia tiles from spain while mwengine zile za chalinze pale hawa hawatafanana.
Ni hayo tuu kwa kuongezea
 
Nashukuru nimekukuta online mtoa mada.
Natarajia kuanza ujenzi lakini nilitaka msingi wa jamvi, msingi ni wa nawe na fundi kaniambia zinahitajika trip 10 za mawe kwa ajili ya msingi huo.

Naomba msaada wa kujua je huu mzingi wa jamvi ya mawe, kokoto, molarm, mchanga na cement hautasababisha kupata mpasuko??

Udongo wa eneo ni mfinyanzi na ni eneo lililokuwa likitumiwa kwa kilimo cha mpunga.

Kiwanja hicho kiko Musoma na ukubwa wake ni sqm 1023.

Naomba ushauri wako mkuu. Nifanyeje au nijengeje msingi ambao hautasababisha nyumba kupata mipasuko??

Ahsante sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya kuchimba msingi amwage mchanga nchi saba . Then suka chuma ( U bar) kisha mwaga zege .baada ya hapo anza kujenga msingi wako.

Udongo utakaotokana na kuchimba msingi usiutumie kama kifusi, tafuta kifusi kingine jaza then compact ...panga mawe...then mwaga jamvi....
 
Baada ya kuchimba msingi amwage mchanga nchi saba . Then suka chuma ( U bar) kisha mwaga zege .baada ya hapo anza kujenga msingi wako.

Udongo utakaotokana na kuchimba msingi usiutumie kama kifusi, tafuta kifusi kingine jaza then compact ...panga mawe...then mwaga jamvi....
Ahsante sana mkuu kwa msaada wako mzuri.

Be blessed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kutofautiana na wewe kidogo ktk suala la kusema kwamba mafundi wote ni wazembe kwa upande wa kuset vyoo&wiring,mimi fundi wangu alimwaga zege vyooni na bafuni ila akabakiza nafasi za kuweka vyoo na kitolea maji machafu bafuni alipokuja mtaalam wa choo baada ya kuviweka akamalizia yeye kuziba pengo la zege lililobaki.

Wiring na mfumo wa maji machafu ya jikoni hakuna namna utafanya ili usitindue kuta shida itakuja pale unapookota mafundi uchwara mtaani wanakuja wanatindua kuta wanalaza mabomba na wire kisha wasizizibe na mchanga ili kumrahisishia fundi plaster kufanya kazi yake kwa ufanisi hapa lazima utaona wote wanafanana akili ila siyo hivyo.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Ila nadhani tunahitaji vifaa rahisishi vya kutindua sio hivi ambavyo tumevizoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm msingi umetumia kozi10hadi naufunga ml11kupandisha tofali juu,hadi kufunga lenta7.8
IMG_20190202_164725.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom