Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Mwaka 2012 nilibahatika kuhudhuria mafunzo fulani kuhusu biashara na uwekezaji.Mafunzo haya yalifanywa na wataalam ambao walikuwa wanalenga kuhamasisha uwekezaji ili kukuza biashara ndogo na za kati.Lilikuwa somo zuri sana.Katika moja ya mijadala tulizungumzia kuhusu vikoba na kwa hakika mtaalamu yule alisema VICOBA katika namna zake zote ikiwamo VIBATI na SACCOS ni aina mojawapo ya UWEKEZAJI katika mfumo wa BUSINESS angels ambao unawezesha biashara ndogo na za kati.Hata hivyo alisisitiza kwamba kuna tatizo katika uwazi,usimamizi na ufuatiliaji hali ambayo inapelekea Hivi vikoa visiweze kukua na kuwa Mifuko ya uwekezaji.
Business Angel ni nani?
Business ni angel ni mtu.Sio malaika ni mtu binafsi ambaye ana kipato cha ziada anayejitolea kuwekeza katika kampuni ndogo inayoanza.Kwa kawaida mtu huyu huwekeza fedha zake au kwa kushirikiana na wengine kwa lengo la kusaidia hizi biashara kifedha.Lakini Muwekezaji huyu pia huwezi kuchukua hatua na kuwekeza muda,utaalamu na uzoefu wake katika biashara hii mpya.
Biashara nyingi ndogo na mpya huwa na changamoto nyingi ikiwamo kukosa fedha,kukosa utaalam,kukosa connection n.k.Kampuni hizi au biashara hizi wakati mwingine huwa na wazo au huduma au bidhaa nzuri na yenye tija na faida kubwa lakini kutokana na kukosa ama fedha au utaalamu hushindwa kupiga hatua na kwenda mbele.Business angels huwekeza katika biashara hizi ili kuwasaidia wainuke lakini wakati mwingine huwekeza ili kupata faida na wakati mwingine huwekeza ili kujiweka bize na kutenda tenda jema.
Sheria inasemaje kuhusu Business Angels:
Business Angels ni wawekezaji sheria zinazowaongoza ni sheria kama sheria nyingine za biashara na mikataba.Kwa mfano kama Business angel atapewa gawio basi gawio litatozwa kodi.Kama Business angel atakuwa na mkataba maalum basi mkataba huwa utazingatiwa.Tofauti ya business angel na muwekezaji mwingine ni kwamba Business Angel anakuwa FREE kuwekeza kwenye kampuni/biashara yoyote na anaweza kuweka masharti kwa kuzingatia malengo na uwezo wake.Uwekezaji kama Business angel sio kama wa kwenye SOKO la hisa ambao unasimamiwa na mamlaka ka CMSA au DSE bali huu ni makubaliano ya watu wawili watatu n.k.Makubaliano hayo yanakuwa na masharti ambayo yatasimamiwa na wote wawili kwa kusingatia vigezo na masharti yaliyowekwa.Kwa kawaida Business angel anaingia makubaliano ambayo huwa yanaitwa MOU(Memorandum of Understanding) ambapo hukubalina kwamba atawekeza kiasi gani kwenye biashara na kwa masharti gani na haki zake ni zipi na wajibu wake ni upi na wajibu wa anayemiliki biashara ni upi n.k.
Hata hivyo ni muhimu ukapata ushauri wa kitaalamu kuhusu sheria na masuala ya fedha ili kuhakikisha kwamba Makubaliano mnayoingia yanakuwa na maslahi ya pande zote na yanazingatia haki usawa na sheria za kibiashara.
Business Angels Wanapatikana wapi?
Business angels wanapatikana katika club za biashara,makundi ya kijamii lakini pia unaweza kumuapproach mtu wewe binafsi kwa kutegemea kiwango cha PESA umachohitaji na uwezo wake ili awekeze katika wazo/biashara yako.Ni muhimu kuizngatia kwamba uwekezaji unaweza kuwa guaranteed na dhamana kama bond na unaweza kumfanya muwekezaji awe BOARD member wa kampuni na hata unaweza kuwa unamlipa faida/riba kwa kipindi fulani kwa kutegemeaarrangement zako.Business angels ni RISK TAKERS na mara nyingi huwekeza ziada ya PESA zao kwani tayari wanakuwa na ukwasi wa ziada.Wazo lako linapomvutia na akaamini katika uwezo wako anaweza kukuabli kuwekeza kwako.
Uwekezaji wa Business Angel unafanyikaje?
Uwekezaji wa business angel unaweza kufanyika in a lumpsum yaani ingizo la pesa la mara moja au malipo ya mara kwa mara.PERIODIC payment.Malipo ya mkupuo ni yale yanayoenda katika uwekezaji mkubwa kama kununua mashine n.k.Uwekezaji wa Periodic ni ule unaoenda katika gharama za uendeshaji-OPERATING COSTS.Lakini pia uwekezaji huu unaweza kufanya kama HISA(EQUITY) au deni(DEBT).Haya yote huamuliwa katika hatua za mwanzo za kuingia makubaliano ya uwekezaji.
Anayehitaji muwekezaji anapaswa kuandaa andiko kwa ajili ya kuonesha wazo lake na potential ya wazo lake.Lengo hapa ni kumwonesha muwekezaji kwamba wazo lako linafaa.Ni kama unavoandaa yale maandiko ya mashindano ya uandishi wa business plan.Tofauti yake hapa ni kwamba inakuwa ni serious business inayohitaji serious mind.Katika andiko lako lazima useme unahitaji PESA kiasi gani,kwa kipindi,kwa matumizi gani.Ni lazima uonesha hali yako ya kifedha ya sasa na mipango yako ya kifedha na ni lazima uonesha muwekezaji atanufaikaje na wewe utanufaikaje(Profit share).Lazima uonesha RISKS na namna ambazo umepanga kuzikabili zikiwamo(Financial Risk,Operational risks n.k.)
Karibuni tujadili zaidi kuhusu UWEKEZAJI wa ANGELS INVESTORS na namna ambavyo unaweza kunufaika nao kibiashara.
PS
FURSA KWA WANAOHITAJI BUSINESS ANGELS
Je unahitaji muwekezaji katika biashar/mradi wako Je tayari unao mpangi wa biashara pamoja na maelezo ya wazi kuhusu mradi wako.Unahitaji muwekezaji mmoja wawekezaji wengi.Je wazo lako lina TIJA kwako,kwa jamii,mazingira na kibiashara.Kama JIBU lako ni ndio basi tutumie email fupi ikielezea wazo lako in BRIEF na kuonesha TIJA iliyomo katika wazo lako,thamni na kiasi cha uwekezaji unachohitaji na matumizi yake.Tuma andiko lako kwenda masokotz@yahoo.com.Iwapo wazo lako litakidhi viwango tutawasiliana nawe kwa ajili ya hatua inayofuata na kama linahitaji maboresho pia tutakupa mwongozo wa nini cha kuboresha.
Baada ya mchakato huo tutakualika katika PITCHING session ili uweze kuelezea wazo lako kwa wawekezaji(Business Angels )Zingatia kwamba gharama za kushiriki katika Pitching zitakuwa Juu yako.Pitching hufanyika katika MIKOA ya Dar es Salaam,Dodoma,Morogoro na Arusha.Utajulisha eneo la PITCHING kabla ya TAREHE ya TUKIO.
Kwa wale ambao wanapenda KUWA business Angels kwa sasa hatuna nafasi ya LEAD INVESTORS hata hivyo iwapo unahitaji kushiriki katika PITCH session ambapo unaweza kupata nafasi ya kuwekeza iwapo IDEA itaachwa na LEAD investors basi unaweza kutuma PIA email kwenda masokotz@yahoo.com.ukieleza eneo lako ambalo ungependa kuwekeza,kiwango chako cha uwekezaji na muda wa uwekezaji.
I wapo unapenda kushiriki katika PITCH session kama Mtazamaji(Observer) tuma email kwenda masokotz@yahoo.com ukieleza interest yako ni katika industry gani.Zingatia kwamba Sessions hizi ni PRIVATE na hivyo MASOKO pamoja na LEAD INVESTORS wanayo haki ya kuruhusu au kuzuia mtu kushiriki.