Faida 10 za kumshukuru Mungu

Faida 10 za kumshukuru Mungu

Nilete ushahidi wa nini mzee umeambiwa mimi wakili wa Mungu?

Wewe kama huamini sawa na mimi kama naamini sawa as longer as kila mmoja ana nafsi yake ana ufahamu wake siioni haja ya mimi kukushikia kidedea uamini uwepo wake
Sawa sasa shukuru kivyako hukoo usituleteee bangi zako
 
Ukishataka katikati ya watu kutaka wakuthibitishie kile wanachokiamini wao huku ukijua kabisa siyo fantasy yako huko tayari ni kukosa amani,wewe huna amani na hutokaa uwe na amani kwa sababu unajisikia hatia kila likitajwa neno ”Mungu”

Nikimwambia mwenzangu kwamba Mungu kweli yupo ana amejionyesha kwangu tukaonyesha kufurahia wewe kinakuuma nini hadi utufate tuthibitishe uwepo wake?
Mkuu japo sio yangu ila Unaposema kitu hasa humu ujue sio kanisani ama msikiti lazima kihojojiwe tu , tatzo la nyie waumini mnatakiwa kuamini tu pasipo uthibitisho humo makanisani na misikitini kwa sababu ndio hivyo imani iliyo hakuna uhakika ni kuamini tu .
 
Nathibitishaje ni maneno ya kiimani yasiyo na uthibitisho?

Mf:wewe hapo ukiwaza kichwani kwamba lile deal tulilozungumza leo kesho lina-tick nikakwambia thibitisha kama ni kweli utaweza kuthibitisha?
Uwepo wa mungu ni nadharia tu unapaswa kuamini hivyo , ukidai ni kwel thibitisha, hauwezi kufa na imani yako hakuna tatizo.
 
Mkuu japo sio yangu ila Unaposema kitu hasa humu ujue sio kanisani ama msikiti lazima kihojojiwe tu , tatzo la nyie waumini mnatakiwa kuamini tu pasipo uthibitisho humo makanisani na misikitini kwa sababu ndio hivyo imani iliyo hakuna uhakika ni kuamini tu .
Conclusion kwamba hakuna uhakika unaitoa wapi wakati wewe siyo mtu wa dini?

Hapa ndipo naposhindwa kuwaelewa atheist wa kibongo.
 
Conclusion kwamba hakuna uhakika unaitoa wapi wakati wewe siyo mtu wa dini?

Hapa ndipo naposhindwa kuwaelewa atheist wa kibongo.
Toa uhakika kama mtu wa dini ili tusiite imani tena tujue kabisa.
 
Tarehe 31 Desemba ni siku ambayo watu wengi hukusanyika makanisani kumshukuru Mungu. Zifuatazo ni faida 10 za kumshukuru Mungu:

1. Huimarisha Imani: Kumshukuru Mungu hutufundisha kutambua uaminifu Wake na kuimarisha imani yetu, tukijua kwamba anafanya kazi kwa manufaa yetu.

2. Hutupa Amani ya Moyoni: Shukrani huondoa mawazo ya wasiwasi na huzuni, na kutuachia amani ya kiroho inayotokana na kumtegemea Mungu.

3. Huongeza Furaha: Watu wanaoshukuru wana furaha zaidi kwa sababu wanathamini hata mambo madogo ambayo Mungu amewatendea.

4. Hutuleta Karibu na Mungu: Shukrani huimarisha uhusiano wetu na Mungu kwa kutufanya tutambue ukuu na upendo Wake maishani mwetu.

5. Huinua Nafsi Zetu: Kumshukuru Mungu hutusaidia kuona maisha katika mtazamo chanya, hata katika changamoto, na hutufanya tujihisi wenye thamani.

6. Hulinda Moyo Usipotoshwe: Moyo wa shukrani hutusaidia kuepuka kiburi na kujiona kuwa sisi ndio chanzo cha mafanikio yetu, badala ya kumtambua Mungu.

7. Hufungua Milango ya Baraka: Shukrani ni kitendo cha imani kinachomfanya Mungu kufungua milango ya baraka zaidi maishani mwetu.

8. Hutuongezea Uvumilivu: Tunaposhukuru kwa yale tuliyonayo, tunapata nguvu za kustahimili majaribu huku tukisubiri Mungu kutimiza ahadi Zake.

9. Hutufundisha Roho ya Unyenyekevu: Shukrani hutufundisha kuwa wanyenyekevu kwa kutambua kwamba kila kitu tunachopata kinatoka kwa Mungu.

10. Ni Njia ya Kutoa Ushuhuda kwa Wengine: Tunapomshukuru Mungu hadharani, tunawashawishi wengine kumwamini na kumtumikia Mungu kwa kuona jinsi alivyotutendea mema.

"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." (1 Wathesalonike 5:18).

Baada ya kuzijua faida hizo, naamini kesho utajiunga na Wakristo wengine kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyotutendea mwaka huu. Sio kesho tu, siku zote kumbuka kumshukuru Mungu, ujionee faida hizo.
Kweli kabisa🙏
 
Thibitisha unachokisema na sio maneno haya ya kiimani tu ambayo tuliletewa kama kitangulizi cha ukoloni.
Daktari anapokuambia katumie dawa flani kwa ugonjwa wako ili upone.Utaiamini dawa au daktari? Hatusubiri matokeo kuwa na imani.
 
Mungu gani ameshindwa na anashindwa kutoa uhai/uzima kwa maelfu ya watoto wachanga na wanawake wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa na majanga mbalimbali ya asili maeneo mbalimbali duniani!!!

Vita huko Gaza zimeua maelfu ya watoto na wanawake na huyo Mungu wenu mchovu, mdhaifu na mjinga hajasaidia chochote!!View attachment 3188907

Kimbunga Chido, kimeua Maelfu ya watu Msumbiji na Kisiwa cha Mayotte. Na huyo Mungu wenu mchovu na mdhaifu hajasaidia chochote. Halafu mnakuja hapa kumpa sifa uchwara Mungu mkatili, muuaji, muovu na bandidu asiye na msaada wowote kwa watu wake!!!View attachment 3188909View attachment 3188910

Huyo Mungu kama yupo hafai kabisa anastahili kufurushwa!!!!
La! Mungu akurehemu
 
.
 

Attachments

  • images - 2024-12-30T225705.396.jpeg
    images - 2024-12-30T225705.396.jpeg
    21.6 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241231-001835.jpg
    Screenshot_20241231-001835.jpg
    45.7 KB · Views: 2
Daktari anapokuambia katumie dawa flani kwa ugonjwa wako ili upone.Utaiamini dawa au daktari? Hatusubiri matokeo kuwa na imani.
Huu ujinga tulishaujibu tatafuta mada za hivi ukarudie majibu huko.
 
Back
Top Bottom