FAIDA FUND (WHI) YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MOI KUHUSU UWEKEZAJI WA FEDHA

FAIDA FUND (WHI) YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MOI KUHUSU UWEKEZAJI WA FEDHA

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
c4d55d7d-d0cb-42ad-92ae-e0d6fa3400ff.jpeg
Mfuko wa Faida Fund, unaosimamiwa na Watumishi Housing Investment (WHI), umetoa mafunzo elekezi ya siku tatu kwa watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuweka akiba na kuwekeza fedha kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia Agosti 19 hadi 21, 2026, na yamejikita katika kuwajengea watumishi uelewa kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji, namna ya kujiwekea akiba pamoja na faida zinazopatikana kupitia uwekezaji wa muda mrefu.

Akifungua mafunzo hayo rasmi, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MOI, Bw. Orest Mushi, amewataka watumishi kuanza kujiwekea akiba na kuwekeza mapema ili kuwa na maisha bora baada ya kustaafu.

“Siku umeajiriwa ndiyo siku unapoanza kujiandaa kustaafu. Ili ustaafu kwa heshima na maisha yako ya kustaafu yawe mazuri, ni lazima uanze kuwekeza sasa. Tumeleta mafunzo haya ili kupanua wigo wa fursa za uwekezaji na kuwasaidia kujiandaa kwa maisha yenu ya baadaye,” amesema Bw. Mushi.

Kwa upande wake, Afisa Uwekezaji wa WHI, Bw. January Melkiado, amesema Mfuko wa Faida Fund unawapa watumishi fursa ya kuanza kuwekeza kwa kiasi kidogo, ambapo mchango unaweza kuanzia Shilingi 10,000.

Amesema michango hiyo inaweza kufanyika kwa kuridhia kukatwa moja kwa moja kwenye mshahara au kupitia vyanzo vingine vya mapato vya mwekezaji.
Bw. Melkiado ameeleza pia kuwa mtu anaweza kujisajili katika mfuko huo kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *152*00# na kufuata maelekezo yanayotolewa.

Amesema uwekezaji wa aina hiyo unampa mtu fursa ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kukuza fedha zake kwa ajili ya kutimiza malengo mbalimbali ya maisha.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwaongezea watumishi wa MOI uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu na faida za uwekezaji, pamoja na kuwahamasisha kutumia fursa zilizopo ili kujiandalia maisha bora ya baadaye na kipindi cha kustaafu.
 

Attachments

  • ff1f51ea-0ed7-468c-8892-d5bdc9008752.jpeg
    ff1f51ea-0ed7-468c-8892-d5bdc9008752.jpeg
    213.9 KB · Views: 8
  • c195c968-ffbe-4bdb-ad7b-4f759424bfd1.jpeg
    c195c968-ffbe-4bdb-ad7b-4f759424bfd1.jpeg
    190.2 KB · Views: 13
Inapaswa mjikite zaidi kwenye kuunga watu mifupa,...!majeruhi wa Bodaboda wanahitaji zaidi huduma yenu zaidi ya sisi tunavyowahitaji huku!

tunatambua uwepo wenu...! hata msipo comment chochote humu.
 
Back
Top Bottom