JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alizungumzia kuhusu mpango wa Wanaume kuruhusiwa kuingia katika vyumba vya kujifungulia wakati wenza wao wanapokuwa katika mchakato wa kujifungua.
Kuna mambo ambayo yanaweza kutajwa kuwa ni faida au hasara za suala hilo kama ambavyo inafafanuliwa na wataalam wa afya:
Baadhi ya wataalamu wa Afya na Wanasaikolojia wamefafanua faida za wanaume kuwepo pamoja na wenza wao wakati wa kujifungua kwamba kutaongeza upendo, kuondoa upweke na kutamsaidia mwanamke kisaikolojia kupata faraja ya kupunguza uchungu wa kujifungua.
Wanasema uwepo wa mume utamsaidia mwanamke kupata hisia chanya na kujiona anathaminiwa na kujiamini zaidi kuwa mwenza wake yuko naye katika shida na raha.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Shedrack Mwaibambe anasema suala la mimba ni la wote wawili, uwepo wa wote katika chumba cha kujifungua utasaidia kuongeza uhusiano zaidi kati ya mume na mke na pia kuondoa hofu endapo kutatokea tatizo mume wake atakuwa pale kutoa taarifa kwa urahisi.
"Hii ni nzuri sana kama kweli unampenda mwenza wako utatamani umsindikize na itaongeza uaminifu, mwanamke anakuwa na imani kuwa hata kama nikichanika vibaya mume wangu yupo ataenda kutoa taarifa," amesema.
Wataalam: Kushuhudia mke akijifungua kumeathiri wengi
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Matilda Ngarina amewahi kunukuliwa akisema: “Hatua ya kujifungua inatisha. Ni wanaume wachache ambao wanaweza kushuhudia wenzi wao wakijifungua kisha wakaendelea kuwa katika hali ya kawaida kisaikolojia.
“Ni tukio la kuogopesha. Linahitaji ujasiri wa ziada. Wanaume waliojaribu kushuhudia wenzi wao wakijifungua 90% wameathirika kisaikolojia.”
Dkt Ngarina anaeleza baadhi ya athari za kisaikolojia walizopata wanaume hao, zimesababisha wengine kujikuta hawatamani tena kutungisha mimba.
“Wapo wanaume wengine waliochukua uamuzi wa kuomba wake zao wafungwe kizazi, ili kuwaepusha kuzaa tena na wengine walipoteza hamu ya kushiriki kwenye tendo la ndoa,” anasema.
Anasema wapo wengine ambao baada ya kukumbwa na athari hizo walijisalimisha kwa madaktari kuomba msaada, ambapo walikutanishwa na wataalamu wa masuala ya saikolojia na wakarejea katika hali yao ya kawaida.
Dkt. Ngarina anasema uamuzi wa kuzungumza na wataalamu wa afya mtu anapopatwa na matatizo, ni jambo muhimu kuliko kuruhusu athari ziendelee kutawala.
“Ukweli ni kwamba wanaume wengi hawana desturi ya kushiriki kwenye kliniki ili wapate elimu ya masuala ya afya na uzazi jambo ambao ni muhimu kusaidia kuwa na familia bora,” anasema.