Faida na hasara nilizozipata kutokana na CASINO za mtandaoni

Faida na hasara nilizozipata kutokana na CASINO za mtandaoni

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mimi ni mlevi wa online CASINO hasa kutoka play Master na Meridian Bet.

Nimeanza kuzicheza 2018 hivi.

Nilizikuta tu mtandaoni bila kuelekezwa na mtu, nikajiunga na kuanza kucheza kwa dau dogo dogo la mia mia ila sasa hivi nacheza dau kubwakubwa.

Faida nilizozipata ni hizi:
1. Muda wa kufanya uzinzi umepungua. Niko busy na gamble.
2. Kwenye utafutaji pesa sina masihara
3. Point nambari 2 imenipelekea kujenga kwa haraka na kununua vyombo vya moto(usafiri).
4. Nimekuwa nikiwasaidia ndugu, marafiki na wazazi kwenye mambo ya pesa kwani kila nikipata pesa nyingi kidogo naona kama nimepata bure.

Hasara nilizozipata:
1. Uraibu. Nimefikia hatua mpaka nisipocheza casino sina raha. Mpaka kazini niko ofisini nacheza casino.
2. Sometimes napoteza pesa nyingi nilizozipata kwenye mishe zingine au nilizozipata kwenye mshahara au posho.
3. Kujamiiana kwangu ni adimu. Kujamiiana ni ile ya kushare mambo mbalimbali na jamii na si kufanya sex.
4. Akili yangu na mtazamo wangu vinaniambia maisha ni bahati, kitu ambacho si kweli.
5. Wito wangu wa mambo ya kiroho unadidimia.

Nilipanga niache 30 Nov 2020, nimeshindwa. Nilipanga niache 31. December yaani leo nimeshindwa pia. Ila wife ananiambia nisiache kwakuwa anaona pesa ndani hazikauki. Mimi sitaki hii hali maana ni ulevi kamili.

Siku nikipata pesa nyingi huko casino nitaacha rasmi.

Niombeeni nizipate ili niache
 
Milioni na ushehe. Kuna wakati upepo ukiwa mzuri napata laki moja hadi tatu kwa siku mfululizo. Yaani kwakweli karibu kila siku lazima nishinde laki au niliwe laki ndio natulia

Mkuu unamaanisha milioni na ushee ndo kiasi kikubwa ulichowahi kushinda? Ok tufanye milioni 2, kwaiyo hiki ndio kiasi kikubwa ulichowahi kushinda au umekosea kuandika mkuu?
 
Upo kwenye game gani, mimi ninapambana na live roulette ijapakuwa inanichapa chapa sometimes
Nacheza magame yale ya Playson na Amatic mara nyingi
Mkuu upo na casino ipi meridian?
Meridian nacheza casino kama tatu hivi ila real na zinazotema ila ninayoipenda na inayotema Sana ni Golden 7
 
Mkuu unamaanisha milioni na ushee ndo kiasi kikubwa ulichowahi kushinda? Ok tufanye milioni 2, kwaiyo hiki ndio kiasi kikubwa ulichowahi kushinda au umekosea kuandika mkuu?
Yaani nazungumzia kwa siku moja. Kwahiyo hapo unaweza kukuta siku tatu mfululizo unapiga M na ushee kila siku.
 
Back
Top Bottom