Hapa hamna kiti zaidi ya chai tu kama watu wengi naowajua waocheza hizi betting za mipira na casino za online.
Wengi ni waongo waongo sana kujisifia wanashinda na hili nilihakikisha.
Nilikuwa nikiazima simu zao au laptop zao, chap chap naingia ile sehem zilikotunzwa password za mitandao wanayoingia, nazipiga picha kwa simu yangu alafu baadae naingia kucheki walichotoa.
Hahahah huwezi amini wale wote waliokuwa wanajisifia walikuwa wanapigwa si kitoto, mtu kama ni betting mikeka mingiiii sana imechanika hivyo hivyo kwa wanaocheza casino online.
Uongo ni moja ya tabia za hawa watu.
Leta ushahidi wa hata hizo milioni unazoshindaga twende sambamba.
Sishauri mtu acheze hii michezo hasa hizo casino maana hizo ndio mbaya zaidi, unashindana na computer ambayo ina akili nyingi ya kula pesa yako, imesetiwa vitu vingi sana inaweza kukuonjesha buku 2 ili ujione we mjanja na kujiamini uweke pesa nyingi alafu ina fyeka, haina utofauti na yale mamashine ya wachina