Faida nilizozipata ni hizi:
1. Muda wa kufanya uzinzi umepungua. Niko busy na gamble.
2. Kwenye utafutaji pesa sina masihara
3. Point nambari 2 imenipelekea kujenga kwa haraka na kununua vyombo vya moto(usafiri).
4. Nimekuwa nikiwasaidia ndugu, marafiki na wazazi kwenye mambo ya pesa kwani kila nikipata pesa nyingi kidogo naona kama nimepata bure.
Hasara nilizozipata:
1. Uraibu. Nimefikia hatua mpaka nisipocheza casino sina raha. Mpaka kazini niko ofisini nacheza casino.
2. Sometimes napoteza pesa nyingi nilizozipata kwenye mishe zingine au nilizozipata kwenye mshahara au posho.
3. Kujamiiana kwangu ni adimu. Kujamiiana ni ile ya kushare mambo mbalimbali na jamii na si kufanya sex.
4. Akili yangu na mtazamo wangu vinaniambia maisha ni bahati, kitu ambacho si kweli.
5. Wito wangu wa mambo ya kiroho unadidimia.