Ndengaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,831
- 14,259
Tanzania tu Gari ndio Anasa, nchi za wenzetu Gari ni zawadi ya Mtoto kuingia high school (Miaka 15) Halafu mwigulu anatuambia sisi ni nchi tajiri ndio maana tunakopesheka.Kwanza tuanze na faida.
Sio siri kumiliki gari kunaimarisha hadhi yako hapo kitaani kwako. Unaonekana wa tofauti mwenye hadhi ya juu. Si ajabu watu wakamwacha mjumbe au balozi wa mtaa wakaja kwako wakidai eti uwasaidie pesa au kusuluhisha migogoro yao.
Unaonekana una fedha na uwezo hata kama ni apeche alolo.
Unaonekana mwenye furaha na amani hata kama kiukweli kwa ndani una huzuni ya moyo na masikitiko.
Unaonekana mwenye kujiamini hata kama ukweli haiko ivo.
Hasara kubwa ya kuwa na gari ya kutembelea ni hii hapa.
Gari ya kutembelea haiingizi pesa yoyote badala yake inakutaka utumie pesa yako kwa ajili ya kununua mafuta, spea na kugharamia matengenezo mbalimbali.
Kifupi kama una pesa ya mawazo au pesa yako ni ya ngama ni heri uachane kabisa kufikiria kumiliki gari au vinginevo nunua gari ya biashara ikuizingie pesa.