Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Kitumburee

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
142
Reaction score
88
Wanajamvi nahitaji ushauri,

Nimedunduliza nakaribia kuvunja kibubu cha ujenzi wa nyumba. Nimeshachorewa ramani na makadirio ya gharama. Leo kwa shauku kubwa nimemuonyesha ramani boss wangu akanishangaa kwanini nimechora ramani yenye paa la gharama kubwa namna hiyo😵 akaniambia flat roo ingegharimu robo tu ya gharama zote za paa hili (ramani yangu ina paa la kawaida tu).

Amenistua kwasababu mchora ramani alinihakikishia hii ramani ni ya nyumba nafuu kabisa.

Sasa wadau nisaidieni mawazo kw ayeyote anaejuaa faida na hasara za kujenga nyumba yenye flatroof kabla sijabadilisha mawazo nikaingia mkenge.

Natanguliza shukrani za dhati
 
Flat roof, kama utakuwa unaamanisha paa ambalo halijainuka sana.

Faida.
-utatumia material chache hasa mbao ila

Hasara
- tegemea corrosion ya bati baada ya mda
- kama ukiwa mikoa yenye joto tegemea ndani kutakuwa na joto sana
 
Flat roof ni nzuri. Unatumia mabati machache na mbao chache. Gharama inaweza kuwa robo ya roof ya kawaida.
Screenshot_2018-05-11-17-03-58.png
 
Mkuu dadavua kidogo kuhusu hiyo flat roof maana kuna flat unaweza tumia sheets (bati) yaan slope inakua ndogo sana na parapet wall kwa pembeni,
Alafu kuna flat roof ya slab, yaan unamwaga zege katika roof yako, hapa utakuna na changamoto ya drainage so laZima utumie pipe kukusanya maji (rain water) , pia utapaka materials kama bitumen, Moyal proof juu ya slab kuzuia leakage
 
Flat roof siku hizi hutii slab. Unatumia bati za kawaida tu
 
Huyo boss wako itakuwa kaona weevu! 🙄🙄🙄 Na siku za hivi karibuni jiandae kisaikolojia kupokea warning letter zinazofululiza bila sababu maalum!
Mambo ya maendeleo sio ishu za ku expose sana ofisini.
Kuna jamaa yangu alikuwa procurement kwenye kampuni yetu. Akanunua gari kali sana ila ya bei nafuu.
Nilimkataza sana asije nayo ofisini yeye hukunisikia. Alipoanza kuja nayo kazini, hakumaliza mwezi wakamuundia zengwe wakamfukuza kazi.
 
Kwa vile umeomba ushauri basi wacha tushauri.

Flat roof ni cheaper sana kuliko pitched roof, lakini kama kutakua na leakage ili ufanye maintenance basi pitched roof ni cheaper kuliko flat roof,
Pia kwa life span , flat roof ni kuanzia 10 -15 years, ukipita huo mda basi inaanza kusumbua,
Kama nipo kwenye nafasi yako ningechagua pitched roof
 
Kwa vile umeomba ushauri basi wacha tushauri....
Flat roof ni cheaper sana kuliko pitched roof, lakini kama kutakua na leakage ili ufanye maintenance basi pitched roof ni cheaper kuliko flat roof,
Pia kwa life span , flat roof ni kuanzia 10 -15 years, ukipita huo mda basi inaanza kusumbua,
Kama nipo kwenye nafasi yako ningechagua pitched roof
Inaanzaje kusumbua baada ya huo muda? Fafanua please.
 
Back
Top Bottom