Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Wanajamvi nahitaji ushauri,

Nimedunduliza nakaribia kuvunja kibubu cha ujenzi wa nyumba. nimeshachorewa ramani na makadirio ya gharama. leo kwa shauku kubwa nimemuonyesha ramani boss wangu akanishangaa kwanini nimechora ramani yenye paa la gharama kubwa namna hiyo😵 akaniambia flat roo ingegharimu robo tu ya gharama zote za paa hili (ramani yangu ina paa la kawaida tu).

Amenistua kwasababu mchora ramani alinihakikishia hii ramani ni ya nyumba nafuu kabisa.

Sasa wadau nisaidieni mawazo kw ayeyote anaejuaa faida na hasara za kujenga nyumba yenye flatroof kabla sijabadilisha mawazo nikaingia mkenge.

Natanguliza shukrani za dhati
Flat roof ni nzuri changamoto ni kwamba inahitaji finishing ya uhakika, garden nzuri kuzunguka nyumba otherwise itaonekana kama jumba lililoachwa na waarabu.
 
Hapo kwenye maintenance naomba ufafanue zaidi kwasababu zinatumika mbao na mabati kama nyumba nyingine sema hii roof inakuwa imefichwa na matofali.
Siyo mtaalam wa hii kitu lakini nimeelewa kwamba roof za namna hii kama kuna miti karibu basi yale majani yake yanayopukutika yanaweza kujaa huko juu na mvua ikinyesha yakalowana yanaozesha paa. Pia wanyama na ndege wanaweza kuweka makazi yao na bila shaka wakajisaidia huko (mf. Paka) . Hivyo lazima kuwe na access ya kufika juu mara kwa mara ili kusafisha.
 
Nyumba za hivi huku kwetu zinaonekana dunk sana mjengo mkubwa ukipaua hivi unaonekena u.ejenga slope ya watu Wa chini kabisa maana ufahari upon kwenye bati.
Pia wataona kama mskiti ...jengo la serekali....


Yote hayo ni mitazamo ya watu.
Vp kudumu kwa bati maana Ni lazima uweke below 10 nyuz ....uchafu unatua...unyevu....kutu vp
 
Flat roof ni nzuri changamoto ni kwamba inahitaji finishing ya uhakika, garden nzuri kuzunguka nyumba otherwise itaonekana kama jumba lililoachwa na waarabu.
Changamoto finishing...otherwise its gonna look like a warehouse.
 
Kuna gutter inatengenezwa inaunganishwa na bomba kutoka juu kwenda chini. Bomba zinachimbiwa ukutani zinaibukia chini level ya msingi.
Hizo gutter zilizounganishwa na bomba ikitokea zimeziba Kwa kujaa uchafu na kutoruhusu maji kupita itakuwaje? Haziwezi kupelekea nyumba kupata shida hasa tatizo hilo likiwa la muda mrefu???
 
Hizo gutter zilizounganishwa na bomba ikitokea zimeziba Kwa kujaa uchafu na kutoruhusu maji kupita itakuwaje? Haziwezi kupelekea nyumba kupata shida hasa tatizo hilo likiwa la muda mrefu???
Gutter ya zege na bomba kubwa.
 
Flat roof siku hizi hutii slab. Unatumia bati za kawaida tu
There you go, Bob...
FB_IMG_1526725538954.jpg
FB_IMG_1522690511389.jpg
FB_IMG_1522690484476.jpg
FB_IMG_1522690467697.jpg
 
Ebu weka hiyo ramani ulio chorewa hapa, then ndipo tunaweza tukakushauri.
Pia kumbuka hizi mambo za michoro kama haujui kuzisoma, tarajia kuingizwa kingi tu
 
Back
Top Bottom