Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Kuta ziweje mkuu, au zinakuwa nene zaidi?
Hebu angalia hapa
IMG-20190204-WA0012.jpeg
received_1986623718025007.jpeg
IMG-20190222-WA0010.jpeg
 
Hii kwako haipendezei? Ama kweli uzuri upo machoni kwa mtu!
img-20180628-wa0056-jpg.807274
Jamaa wanazingua binafsi sijawahi kuwa na mchecheto na nyumba kama ilivyo sasa na hasa baada ya kuona aina hizi za nyumba wanaziita contemporized house design! Za kinyama sana.
 
Unanikumbusha waka gari zenye Auto transmission zilipoanza kuingia.
Watu walikandia hivi hivi, "Change is inevitable" mara oh gari za vilema blah blah leo kiko wapi!

Anyways, hivi conversion inawezekana kwa nyumba yenye pitched roof kwenda yenye flat roof?
 
Watu walikandia hivi hivi, "Change is inevitable" mara oh gari za vilema blah blah leo kiko wapi!

Anyways, hivi conversion inawezekana kwa nyumba yenye pitched roof kwenda yenye flat roof?

Inafaa ila nadhani itakua kazi kidogo maana lazima kuta ziongezwe. Conversion rahisi ni kutoka flat kwenda pitched.
 
Watu walikandia hivi hivi, "Change is inevitable" mara oh gari za vilema blah blah leo kiko wapi!

Anyways, hivi conversion inawezekana kwa nyumba yenye pitched roof kwenda yenye flat roof?
Inawezekana,ila itabidi kuwekwe njia za kutoa maji kwenye roof kushuka chini.
 
Wakuu naombeni turudi kwenye huu uzi




Mi naomba kujulishwa material ya huku kwenye kuta za nje nitumie rangi au nini ambayo haitabanduka kirahisi?

Pia naomba kujua niweke kozi ngapi za tofali toka kwenye lenta mpaka juu ili kuleta muonekano mzuri?

Ntashukuru kwa msaada wenu.
Kuta hakikisha zinapigwa white cement ya uhakika na rangi weather guard ya uhakika.
Tofali kutoka ring beam kozi tano mpaka sita. Nyumba ya KAWAIDA tatu ila hii minimum tano na mkanda juu. Mara nyingi inategemea na ukubwa wa nyumba.
 
Design hizi ni nzuri lakini naomba nieleweshwe je distance kati ya ceiling board na bati kwa ndani ikoje? Je inaweza kuwa na nafasi kiasi cha mtu/fundi kuingia pale ukarabati unapohitajika? mathalan fundi wa umeme au kufanya usafi au kuua wadudu kama panya wanaotanbaa juu ya dari? Au hapo fundi itambidi àcrow ili kuweza kuingia ndani ya ceiling?
Huwa hakuna kuingia kwenye dari. Hakikisha umeziba vizuri wadudu kama panya wasiingie.
Wiring inafanywa kwenye ukuta chini sio darini. Yaani connection za waya ni kwenye switch/socket chini. Juu zinapita waya nzima nzima so ukiweka gypsum hupandi tena shoti ya umeme unarekebisha chini.
 
Ila kama hio ulioweka mchoro wake inabidi uweke na mabomba ya kutolea maji maana mvua ikipiga hapo maji yanajaa juu ya roof kama swimming pool
Kule unapoona bati zimelala kuna gutter. Inaweza kuwa ya zege au bati gumu. Ya zege life guarantee, bati inalalia hapo inamwagika maji yanashushwa chini na pipe kubwa zinazochimbiw nusu along the wall nusu nje inazibwa na plaster inaibukia chini mwisho wa msingi. Mtu haoni maji yanatokea wapi.
 
Ana hoja ya msingi. Mzunguko wa tofali unaongeza gharama.
Nyumba ya KAWAIDA baada ya ring beam unazungusha kozi tatu,hii ni kozi tano mpaka sita. So kuna ongezeko la kozi 2-3. Nafikiri unajua bei ya mbao na mabati.
Ya kwangu roof ya KAWAIDA ningetumia mabati at least 100, hii nimetumia mabati 40+. Mbao ndio wala sisemi.
 
Back
Top Bottom