Faida ya Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) kabla ya kodi ilipanda kwa asilimia 201 hadi kufikia shilingi bilioni 44.81 mwaka 2024

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
IMEELEZWA a kuwa Faida ya Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) kabla ya kodi ilipanda kwa asilimia 201 hadi kufikia shilingi bilioni 44.81 mwaka 2024, kutoka hasara ya shilingi bilioni 44.42 mwaka 2023, huku faida baada ya kodi ikiongezeka kwa asilimia 170 hadi shilingi bilioni 32.62 kutoka hasara ya shilingi bilioni 46.28.
IMG_20250526_142600_055.jpg

Mafanikio haya yalichangiwa na ongezeko la mapato halisi ya riba kwa asilimia 19.02 hadi shilingi bilioni 120.90, na mapato ya riba yalipanda kwa asilimia 16.93 kufikia shilingi bilioni 178.86. Hata baada ya gharama za riba kuongezeka kwa asilimia 12.79, mapato yalizidi gharama, hivyo kuimarisha matokeo ya kifedha.

Aidha, mapato mengine ya kiuendeshaji yaliongezeka kwa kiwango kikubwa cha asilimia 378.56 hadi kufikia shilingi bilioni 10.47, hatua iliyosaidia kupandisha mapato ya uendeshaji na kuondokana na hasara ya mwaka uliopita. Jumla ya mali za TCB zilipanda kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi trilioni 1.74, na amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 23.03 hadi kufikia shilingi trilioni 1.17, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa imani ya wateja. Uwiano wa mikopo chechefu uliongezeka kidogo hadi asilimia 3.08, lakini bado uko ndani ya kiwango cha juu cha asilimia 5 kinachokubalika na Benki Kuu ya Tanzania.
IMG_20250526_142547_581.jpg

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Wanahisa (AGM) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bw. Adam Mihayo, alisema benki imejidhatiti kuendelea kutumia teknolojia ya kidijitali kuleta mageuzi ya huduma, hasa kwa kuwafikia wajasiriamali wadogo na wa kati. “Kwenye mwaka huu wa fedha, tunalenga kuendelea kuboresha ufanisi katika kutumia fursa zinazotolewa na teknolojia ya kidijitali, kwa lengo la kuwezesha ukuaji wa sekta hii ambayo ni nguzo kuu ya uchumi wa taifa,” alisema.
IMG_20250526_142652_396.jpg

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCB, Bw. Martin Kilimba, alibainisha kuwa benki itaendelea kujizatiti kutoa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedha kwa Watanzania. “Katika mwaka huu wa fedha, tunakusudia kuendelea kuboresha ufanisi wetu… Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, na kutumia fursa zinazoletwa na teknolojia ya kidijitali,” alisema Bw. Kilimba, akisisitiza dhamira ya benki hiyo kuchangia kwa dhati maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 
IMEELEZWA a kuwa Faida ya Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) kabla ya kodi ilipanda kwa asilimia 201 hadi kufikia shilingi bilioni 44.81 mwaka 2024, kutoka hasara ya shilingi bilioni 44.42 mwaka 2023, huku faida baada ya kodi ikiongezeka kwa asilimia 170 hadi shilingi bilioni 32.62 kutoka hasara ya shilingi bilioni 46.28.
View attachment 3346473
Mafanikio haya yalichangiwa na ongezeko la mapato halisi ya riba kwa asilimia 19.02 hadi shilingi bilioni 120.90, na mapato ya riba yalipanda kwa asilimia 16.93 kufikia shilingi bilioni 178.86. Hata baada ya gharama za riba kuongezeka kwa asilimia 12.79, mapato yalizidi gharama, hivyo kuimarisha matokeo ya kifedha.

Aidha, mapato mengine ya kiuendeshaji yaliongezeka kwa kiwango kikubwa cha asilimia 378.56 hadi kufikia shilingi bilioni 10.47, hatua iliyosaidia kupandisha mapato ya uendeshaji na kuondokana na hasara ya mwaka uliopita. Jumla ya mali za TCB zilipanda kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi trilioni 1.74, na amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 23.03 hadi kufikia shilingi trilioni 1.17, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa imani ya wateja. Uwiano wa mikopo chechefu uliongezeka kidogo hadi asilimia 3.08, lakini bado uko ndani ya kiwango cha juu cha asilimia 5 kinachokubalika na Benki Kuu ya Tanzania.
View attachment 3346472
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Wanahisa (AGM) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bw. Adam Mihayo, alisema benki imejidhatiti kuendelea kutumia teknolojia ya kidijitali kuleta mageuzi ya huduma, hasa kwa kuwafikia wajasiriamali wadogo na wa kati. “Kwenye mwaka huu wa fedha, tunalenga kuendelea kuboresha ufanisi katika kutumia fursa zinazotolewa na teknolojia ya kidijitali, kwa lengo la kuwezesha ukuaji wa sekta hii ambayo ni nguzo kuu ya uchumi wa taifa,” alisema.
View attachment 3346474
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCB, Bw. Martin Kilimba, alibainisha kuwa benki itaendelea kujizatiti kutoa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedha kwa Watanzania. “Katika mwaka huu wa fedha, tunakusudia kuendelea kuboresha ufanisi wetu… Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, na kutumia fursa zinazoletwa na teknolojia ya kidijitali,” alisema Bw. Kilimba, akisisitiza dhamira ya benki hiyo kuchangia kwa dhati maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Awamu ya wazee wa kulinda Legacy kina Gwajiboy benki zilikuwa zinapata hasara na kujifia.
 
Haya majitu usiyaamini, majizi matupu . Yanahubiri uongo.
Angali UDART hàpa yalikuwa yanatangaza faida kila leo! Majizzi matupu
 
Attachments

  • 6244436-6da0a816af9b40a9bafe3b2d73e11f8-1.mp4
    14.2 MB
Back
Top Bottom