JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Maji husaidia mmeng'enyo au usagaji wa Chakula na mara nyingine hutuliza Maumivu ya Kichwa endapo maumivu hayo yametokana na upungufu wa Maji mwilini. Kunywa Maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara nyingi zaidi
Pendezesha ngozi yako kwa kunywa Maji ya kutosha kwani yanasaidia kuboresha tishu za Ngozi na kuongeza unyevu. Maji yanaweza kusaidia kupunguza uzito kwasababu huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki mwilini
Uwezekano wa kupata Mafua, Mawe ya Figo, Matatizo ya Ini na Magonjwa mengine yanaweza kupunguzwa kwa kunywa Maji ya kutosha. Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa Misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.