Faida za kiafya zitokanazo na kunywa maji ya kutosha

Faida za kiafya zitokanazo na kunywa maji ya kutosha

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
IMG_20210512_025327_852.jpg


Maji husaidia mmeng'enyo au usagaji wa Chakula na mara nyingine hutuliza Maumivu ya Kichwa endapo maumivu hayo yametokana na upungufu wa Maji mwilini. Kunywa Maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara nyingi zaidi

Pendezesha ngozi yako kwa kunywa Maji ya kutosha kwani yanasaidia kuboresha tishu za Ngozi na kuongeza unyevu. Maji yanaweza kusaidia kupunguza uzito kwasababu huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki mwilini

Uwezekano wa kupata Mafua, Mawe ya Figo, Matatizo ya Ini na Magonjwa mengine yanaweza kupunguzwa kwa kunywa Maji ya kutosha. Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa Misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.

IMG_20210512_025330_655.jpg
 
Damu peke yake ina uzito wa lita 5 mwilini so kunywa maji mengi kupita kiasi wkt mwili haufanyi shughuli nzito ni kuupa moyo kazi ya ziada na kusababisha matatizo ya moyo.Kama haufanyi kazi nzito kunywa maji Lita 1.5 mpk 2 kwa siku inatosha sana-Prof Janabi-mtaalam wa magonjwa ya moyo Muhimbili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom