Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
182
Habari wakuu, mimi ni mtumishi wa Umma ambapo nina fursa za kukopa benki mkopo wa muda mrefu na mfupi na siku hizi benki nyingi zimeongeza muda wa mkopo hadi miaka 8.
Nilikuwa naomba mawazo yenu kuhusu faida za mkopo wa muda mrefu na muda mfupi ingawa nafahamu kuwa changamoto kubwa ya mkopo wa muda mrefu ni riba kuwa kubwa, Je zipi faida nyingine?
 
Hakuna faida za mkopo.
Hio miaka utakayokopa utapata tabu sana.

Kwa mtumishi wa umma, hakuna kitu chochote unachoweza kufanya bila kukopa. Hata gari tu ya milioni 8 huwezi kusema ukusanye mishahara mpaka itimie hiyo hela. Cha maana ni kuwa na malengo na kuhakikisha unapokopa pesa hiyo unaipeleka kwenye lengo husika.
 
Habari wakuu, mimi ni mtumishi wa Umma ambapo nina fursa za kukopa benki mkopo wa muda mrefu na mfupi na siku hizi benki nyingi zimeongeza muda wa mkopo hadi miaka 8.
Nilikuwa naomba mawazo yenu kuhusu faida za mkopo wa muda mrefu na muda mfupi ingawa nafahamu kuwa changamoto kubwa ya mkopo wa muda mrefu ni riba kuwa kubwa, Je zipi faida nyingine?
Ila mradi tuu ukope kwa ajili ya shughuli mhimu.otherwise mkopo bila mpango wowote wa mhimu jinsi ya kutumia mkopp kupata fedha ni sawa na kaburi.

mkopp wa muda mrefu faida yake utakatwa instalment ndogo kila mwezi

Hasara yake mkopo unavyokuwa wa muda mrefu riba inaweza kuwa sawa na principle(riba na mkopo kuwa sawa)
 
Habari wakuu, mimi ni mtumishi wa Umma ambapo nina fursa za kukopa benki mkopo wa muda mrefu na mfupi na siku hizi benki nyingi zimeongeza muda wa mkopo hadi miaka 8.
Nilikuwa naomba mawazo yenu kuhusu faida za mkopo wa muda mrefu na muda mfupi ingawa nafahamu kuwa changamoto kubwa ya mkopo wa muda mrefu ni riba kuwa kubwa, Je zipi faida nyingine?
Kabla ya kukopa mkopo wowote, uwe wa muda mrefu au mfupi, jiulize kwanza hizo pesa unataka kuzifanyia nini? Muda wa mkopo utategemea na kiasi cha mkopo unachotaka kutokana na malengo yako, lakini pia uwezo wako wa kulipa kila mwezi.

Kama huna jambo la maana la kufanya ni unataka tu kukopa kwavile benki wameongeza muda, au wamekushawishi, ndugu yangu utaumia. Mkopo ni mzuri sana kwa mtu mwenye malengo ila kama huna malengo utauona mchungu.
 
Mhh me naona nyingi jamani

Kwetu ni 5%
Na bado naikwepa nikikwama najikopea salary adv

Labda bado sijakolezwa vizuri na majukumu
Yakinikolea hata 18% itakuwa ndogo 🤣
Hiyo asilimia 5 ni kwa mwezi au kwa mwaka?
 
kwa uandishi wako inaonyesha unakopa ili ukajenge nyumba ya kuishi kijijini kwenu
 
Back
Top Bottom