Habari wakuu, mimi ni mtumishi wa Umma ambapo nina fursa za kukopa benki mkopo wa muda mrefu na mfupi na siku hizi benki nyingi zimeongeza muda wa mkopo hadi miaka 8.
Nilikuwa naomba mawazo yenu kuhusu faida za mkopo wa muda mrefu na muda mfupi ingawa nafahamu kuwa changamoto kubwa ya mkopo wa muda mrefu ni riba kuwa kubwa, Je zipi faida nyingine?
Habari za jioni wakuu
Nimeamua kuanzisha uzi huu ili iwe ni chanzo cha kujifunza mawili matatu kwa watumishi wa umma kuhusu mikopo inayotolewa na benki mbali mbali kwa watumishi wa umma.
Kumekuwa na malalamiko na vilio kwa watumishi wa umma kuhusu mikopo wanayopewa na benki. Wengi wao wanalaumu mikopo hiyo kuwa ni kandamizi na haipo kwa lengo la kuwa saidia bali ipo kuwakandamiza na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.
Ukichunguza kwa undani zaidi utagundua tatizo sio mikopo inayotolewa na benki bali shida ipo kwa sisi watumishi kutokuwa na elimu juu ya namna bora ya kukopa.
Kwanza tufahamu ya kwamba benki za biashara zipo kutengeneza faida na kuzifanya ziendelee kuwepo sokoni.
Miongoni mwa bidhaa (products) zinazowafanya kupata faida na kuendelea kubaki sokoni ni hii mikopo kwa watumishi wa umma.
Kwa hiyo mtumishi wa umma unapokwenda kukopa benki afisa mikopo wa benki hiyo atakupa chaguo (option) ambayo itakuwa na faida zaidi kwa benki.
Chukulia mtumishi ana mshahara wa kuchukuwa nyumbani (take home) wa 700k, kwa mtumishi asiekuwa na elimu ya mikopo akifika benki atamuuliza afisa mikopo kwa mshahara wa 700k naweza kukopa kiasi gani??
Hapa afisa mikopo atakachoangalia kwanza ni option ipi itaingizia benki faida kubwa zaidi?
Ataanza kupiga mahesabu, kwanza ataangalia ni kiasi gani katika mshahara wa mtumishi kinakopesheka kwa kuzingatia sheria ya 1/3 ya mshahara ibaki kwa mtumishi , atagundua 2/3 ya 700k ni kama 460,000 hivi, kwa hiyo hapo mda wa chini atamuambia kwa miaka mitano una uweko wa kukopa hadi 19M, makatao yote itakuwa around 443,000 kwa mwezi.
Mtumishi aiekuwa na elimu ya milopo anaangalia mshahara wake wa 700k anajikuta inabakisha 270,000. Anamuuliza afisa mikopo nikichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane je?
Anaambiwa ukichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane kila mwezi utakatwa 325,000. Anakubali kuchukuwa 19M kwa miaka nane kwa sababu tu makato ni madogo.
Asicho kijuwa ni kuwa akichukuwa mkopo wa 19M kwa miaka mitano aliyotajiwa na afisa mikopo atakuwa ameipatia benki faida ya around 7,600,000 na akichukuwa kwa miaka nanae atakuwa ameipatia benki faida ya 12,160,000.
Kumbuka mtumishi huyu anachukuwa mkopo huu lengo lake kubwa ikiwa ni kuendeleza ujenzi wa kiawanja chake, kwa hiyo anachukuwa hiyo 19M ndani ya miaka nane anaishia kwenye kufunga linta.
Tunalopaswa kulielewa kwa sisi watumishi wa umma ni kuwa:
-Mkopo unaozidi miaka miwili na nusu hapo ni kujiumiza na unachokifanya ni kuinemeesha benki na kumfanya afisa mikopo kuongezwa cheo.
Ni vizuri kwa mtumishi wa umma kabla ya kwenda benki kwa ajili ya kukopa awe ameshatayarisha mpango wa mkopo. Usisubiri benki wakupangie wao, watakuumiza kwa kukupa option ya muda mrefu.
-Mtumishi wa umma jitahidi ukopebkwa awamu mgawanyiko zenye muda mfupi mfupi.
Chukulia hii 19M ambayo mtumishi mwenye take home ya 700k ambae alichagua kukopa kwa miaka nane, njia bora ni kuanza na 9.5M kwa miaka miwili na nusu tu ambapo atatakiwa kulipa 11.5M kwa makato ya 380,000 kwa mwezi. Riba ya miaka miwili na nusu atakuwa around 1,900,000.
Baada ya kuisha miaka miwili na nusa anachukuwa 9.5M nyengine. Hapo riba ya miaka mitano itakuwa ni 3,800,000 badala 7,600,000 kwa muda ule ule wa miaka mitano.
Mwisho tusiwe na tabia za kulalamika kwa matatizo tunayoyatengeneza wenyewe, tutafute elimu ya mambo tunayoyafanya ili kuwa na matikeo bora zaidi.