Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

we kopa tu, kila mtu huwa na malengo kabla ya kushika hela za mkopo....ukishakopa sasa ndio mambo huvurugika....we kopa tu mkuu
 
Wataalam wa mikopo wanakwambia usikope kununua gari ya kutembelea maana gari liability haliingizi chochote Bali litakufanya pia utoe hela mfukoni ili kulihudumia kwa hiyo litakunyonya zaidi, kama unataka kununua gari basi nunua ya biashara eg hiace, coaster, kirikuu, tipper etc ili ilete hesabu pia hata kujenga nyumba ya kuishi kwa mkopo hawashauri pia labda ujenge ya biashara let say guest house, vyumba vya biashara n.k. Jana niliiona video moja ya MO anasema watu wanakosea kwa kukopa hela then wanajenga nyumba ya kuishi kwa nin hiyo hela usiifanyie biashara na wewe ukaendelea kupanga nyumba yenye gharama ndogo then biashara ikikua na kuanza kuingiza faida ya kutosha ndio unajenga nyumba kwa kutumia faida unayoipata
Hapa ni pagumu kwa mtumishi mkuu,huo muda wa kufanya hiyo biashara ni saa ngapi,unatoka nyumbani saa 12 asubuhi unarudi saa 2 usiku,ndio maana watumishi wengi mikopo yao wananunulia magari au kujenga nyumba,hao unaozungumzia wewe ni wafanyabiashara...
 
Kimfaacho mtu chake.
Kopa mzee hata ukiinywa sawa tu maana kesho yako huijui. Tena usisahau kuita chawa wakutosha ili ukifulia tusiache kukuita tajiri.
 
Kimfaacho mtu chake.
Kopa mzee hata ukiinywa sawa tu maana kesho yako huijui. Tena usisahau kuita chawa wakutosha ili ukifulia tusiache kukuita tajiri.
Kwa hiyo hapo na wewe umetoa ushauri?
 
Finacial literacy ni tatizo kubwa sana kwa wengi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Riba ya mkopo full

Hiyo 5% ni riba ya mkopo utakaochukua kwa muda wote wa marejesho yako..

Ni saccoss ya ofisi hiyo ndo tunakopeshwa kwa riba ya 5%
Mf. Nakopa 10M
10,000,000 riba ya 5% ni 500,000.. so nitakuwa nina jumla ya deni la 10,500,000/= machaguzi ya kukatwa kwa muda wa miezi 12/18/24 ni yako.


Cc Financial Freedom
Oooh hapo Sawa nimekupata nadhani huwezi chukua zaidi ya mara nne ulichoweka
 
ndio maana watumishi wengi mikopo yao wananunulia magari au kujenga nyumba

Sijajua ni kwanini watu wanaona kama mtu akikopa akajenga nyumba ya kuishi au kununua gari anakua amefanya kitu kibaya? Nyumba na gari ni BASIC NEEDS kwa maisha ya sasa, ni sawa na simu.

Mtu aliekopa akajenga nyumba ya kuishi, au akanunua gari ya kutembelea, na yule alie invest kwenye biashara, wote wanakua wamefanya mambo ya maana kimaisha!
 
MMmm
Sijajua ni kwanini watu wanaona kama mtu akikopa akajenga nyumba ya kuishi au kununua gari anakua amefanya kitu kibaya? Nyumba na gari ni BASIC NEEDS kwa maisha ya sasa, ni sawa na simu.

Mtu aliekopa akajenga nyumba ya kuishi, au akanunua gari ya kutembelea, na yule alie invest kwenye biashara, wote wanakua wamefanya mambo ya maana kimaisha!
Mmmmh!!!
 
Mhh me naona nyingi jamani

Kwetu ni 5%
Na bado naikwepa nikikwama najikopea salary adv

Labda bado sijakolezwa vizuri na majukumu
Yakinikolea hata 18% itakuwa ndogo [emoji1787]

Kwenu wapi huko mnakopeshwa/kopesha kwa riba ya 5% nami nije kuchukua kibunda?
 
Kwa mtumishi wa umma, hakuna kitu chochote unachoweza kufanya bila kukopa. Hata gari tu ya milioni 8 huwezi kusema ukusanye mishahara mpaka itimie hiyo hela. Cha maana ni kuwa na malengo na kuhakikisha unapokopa pesa hiyo unaipeleka kwenye lengo husika.
Ila ukichukua mkopo halafu ukanunua gari unapata faida gani? Ni kujiongezea umasikini tu.

Afadhali hata mkopo wa nyumba unaeleweka unafanya jambo la maana kuliko wa gari.
 
Mil 8 ni pesa ndogo kwa nani? Mkuu, hebu panua mawazo kidogo acha kujifungia kwenye box. Usidhani kwamba kwa vile wewe umebahatika kuwa na vijihela basi watu wote ni kama wewe. Kwa taarifa yako mil 8 ni hela nyingi sana kwa majority ya watanzania..!
Naona amejisahau huyu. Hata huyo anayepata mshahara mkubwa basi milioni 8 ni nyingi
 
Back
Top Bottom