Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

we kopa tu, kila mtu huwa na malengo kabla ya kushika hela za mkopo....ukishakopa sasa ndio mambo huvurugika....we kopa tu mkuu
 
Hapa ni pagumu kwa mtumishi mkuu,huo muda wa kufanya hiyo biashara ni saa ngapi,unatoka nyumbani saa 12 asubuhi unarudi saa 2 usiku,ndio maana watumishi wengi mikopo yao wananunulia magari au kujenga nyumba,hao unaozungumzia wewe ni wafanyabiashara...
 
Kimfaacho mtu chake.
Kopa mzee hata ukiinywa sawa tu maana kesho yako huijui. Tena usisahau kuita chawa wakutosha ili ukifulia tusiache kukuita tajiri.
 
Kimfaacho mtu chake.
Kopa mzee hata ukiinywa sawa tu maana kesho yako huijui. Tena usisahau kuita chawa wakutosha ili ukifulia tusiache kukuita tajiri.
Kwa hiyo hapo na wewe umetoa ushauri?
 
Finacial literacy ni tatizo kubwa sana kwa wengi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Oooh hapo Sawa nimekupata nadhani huwezi chukua zaidi ya mara nne ulichoweka
 
ndio maana watumishi wengi mikopo yao wananunulia magari au kujenga nyumba

Sijajua ni kwanini watu wanaona kama mtu akikopa akajenga nyumba ya kuishi au kununua gari anakua amefanya kitu kibaya? Nyumba na gari ni BASIC NEEDS kwa maisha ya sasa, ni sawa na simu.

Mtu aliekopa akajenga nyumba ya kuishi, au akanunua gari ya kutembelea, na yule alie invest kwenye biashara, wote wanakua wamefanya mambo ya maana kimaisha!
 
MMmm
Mmmmh!!!
 
Mhh me naona nyingi jamani

Kwetu ni 5%
Na bado naikwepa nikikwama najikopea salary adv

Labda bado sijakolezwa vizuri na majukumu
Yakinikolea hata 18% itakuwa ndogo [emoji1787]

Kwenu wapi huko mnakopeshwa/kopesha kwa riba ya 5% nami nije kuchukua kibunda?
 
Ila ukichukua mkopo halafu ukanunua gari unapata faida gani? Ni kujiongezea umasikini tu.

Afadhali hata mkopo wa nyumba unaeleweka unafanya jambo la maana kuliko wa gari.
 
Mil 8 ni pesa ndogo kwa nani? Mkuu, hebu panua mawazo kidogo acha kujifungia kwenye box. Usidhani kwamba kwa vile wewe umebahatika kuwa na vijihela basi watu wote ni kama wewe. Kwa taarifa yako mil 8 ni hela nyingi sana kwa majority ya watanzania..!
Naona amejisahau huyu. Hata huyo anayepata mshahara mkubwa basi milioni 8 ni nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…