Uchaguzi 2020 Faida zitatazotokana na upinzani kumweka Tundu Lissu au Bernard Membe kugombea Urais

We kweli Tindo. Manake bwana mtu aliye tila-lila akikabiliana na tindo itakuwa ni kwishney. Mie nipo kwetu Idukilo huku Shinyanga kaka! Nirushiane ka milini basi uone kama sijakurudishia!

Na kuheshimu boss, rudisha hela ya mzee wa watu usijepata laana.
 
Kuna wengine ni wana ccm mkisikia hoja hatari kwa ccm mnajifanya mnapinga. Lissu, Nyalandu, Membe wakiwa wamoja mtikisiko utakuwepo.
 
Je chama dola kinajua kuhusu nguvu ya umma?

Watz wanapaswa waelewe mabadiliko ndio maendeleo.

Inatakiwa Safu ya Viongozi wa kisiasa wabadilishwe waje wengine na mawazo mengine. Wapinzani wakichukua madaraka watakuja na Baraza lao la mawaziri na watasafisha wale viongozi ambao wamekuwa wakiteuliwa walewale Kila siku kwa kubadilishiwa vyeo...

Safisha safisha ya uongozi itagusa wakuu wa mikoa, wilaya na Viongozi ktk mashirika na taasisi za serikali... Hapa nchi itapata watu wapya na mawazo mapya ya maendeleo...

Naamin wapinzani wakichukua nchi Tume ya uchaguzi itakuwa huru, katiba mpya ya Warioba itapitishwa...

Mikataba mibovu itafumuliwa na kutafutiwa suluhisho la win win situation...

Ufisadi uliofanywa na makada wa CCM utawekwa adharani na wahusika kuchukuliwa hatua...
 
Umesema kweli kabisa!
 
Mh Lisu ndo habari ya mjini
 
Wanao faidi keki ya Taifa mzunguko wake ni uleule 'mnyororo unao zunguka'
 
Sure
Sure, halafu MATAGA ndio wanaandika na kutoa huu ushauri.Nadhani kuna watu "mbongo" zao zilikosa virutubisho vya maziwa ya mama.

CDM bora isimamishe mgombea hata asie popular,kuliko kuchukua kichomi kama Membe....hawa walipokuwa CCM hawakuwahi kupigania ustawi wa demokrasia,leo huo ufinyu wa demokrasia unawatafuna wanataka kuja kutaka kupenyea huku.😃
 
CHADEMA wame-implode, kama ambavyo NCCR baada ya 1995 na CUF baada ya 2010 walivyopitia.
 
6 July 2020
Lindi, Tanzania

MEMBE baada ya kurudisha kadi ya CCM/tutajiunga na chama tutagombea uongozi wa juu tutashinda
Bernard Carmillus Membe akiwa kijijini kwake Rondo mkoani Lindi kusini mwa Tanzania aongea mazito baada ya kuiacha CCM kwa kurudisha kadi ya uanachama.

Alihudumu chini ya Rais Jakaya Kikwete kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kwa miaka 10. Pia alipata kuwa mbunge wa CCM jimbo la Mtama mkoani Lindi. Alihudumu kama afisa mwambata wa ubalozi wa Tanzania kwa miaka 10 huko Canada ktk bara la Marekani ya Kaskazini. Pia alipata kuwa Afisa Mchambuzi wa ripoti ktk Kurugenzi ya Usalama na Intelejensia wa Taifa TISS katika Ofisi ya Rais.

Hali ya kisiasa mikoa ya Lindi na Mtwara na kwingineko Tanzania kwa ujumla inaonesha waTanzania wapo tayari kwenda na Bernard Membe ili kuweza kuweka sawa masuala ya kama kilimo, uvuvi, mifugo, gesi na Maendeleo ya Watu.
Source : Gilly Bonny Online TV
 
kwa katiba hii ya sasa, upinzani msijisumbue.
Mngekaa kando tu kama mlivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hamtashinda chochote labda Zanzibar tu
 
kwa katiba hii ya sasa, upinzani msijisumbue.
Mngekaa kando tu kama mlivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hamtashinda chochote labda Zanzibar tu
Hapana waache wafurukute, ccm hawatakiwi kuokota ushindi sebuleni hawana budi waupiganie.
Joto lipashwe jingi tu angalau watu wapate adabu.
 

Yaani katika pita pita zangu huku forum kwa leo hii ndo pointi ya msingi sana kwa wapinzani, sielewi na hainingii akilini unamruhusu membe kugombea na sio mpinzani, yaani kama upinzani ndo utendelea ivi ivi mnachukua watu wa ccm alafu wanagombea kutakua hamna maaana halisi ya upinzani
 
Nadhani chadema kama chama cha siasa walisha jipanga vizuri huwa wanatumia utafiti kufikia maamuzi mengi. 'They have gone through the ups and downs Tundu Lissu is the best optin'
 
Amini nakwambia, upinzaniukimsimamisha TUNDU ANTIPASS LISSU, CCM wanakimbia ikulu. Amini maneno yangu. Hoja na hulka ya Lissu CCM hawawezi kukabilana nazo, narudia HAWAWEZI
 
Amini nakwambia, upinzaniukimsimamisha TUNDU ANTIPASS LISSU, CCM wanakimbia ikulu. Amini maneno yangu. Hoja na hulka ya Lissu CCM hawawezi kukabilana nazo, narudia HAWAWEZI

Tundu lissu anaweza kua hazina lakini baada ya magufuli, unajua waatu hawana imani na ccm ila watu wanampenda magufuli ina maaana baada ya magufuli kumaliza mda wake, itakua ni ngumu sana ccm kupata mwenye hio spidi ya magu! ina maaana upinzani mkicheza karata zenu vizuri kujiimarisha hiki kipindi magu anamalizia mda wake 2025 mkimnyanyua lissu mmemaliza mchezo ila kama mnawaza kuchukua nchi hii oktoba hio sahau na wala usipoteza mda wako! watu wako kwenye mpango wa kumlazimisha aongeze mda hata awamu ya pili haijaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…