Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwa matokeo uliyoyaonesha kwenye uzi wako, nakushauri rudia form III na IV. Nadhani kuna mpango wa kuisoma hiyo kwa mwaka mmoja na uwe dedicated na masomo ili upate matokeo mazuri. Matokeo yatakupa muangaza.
 
hata ukristo pia uko hivyo
Kuna tofauti nyingi za kiitikadi kati ya Ukristo na Uislam lakini tofauti kubwa ya Ukristo na Uislam ni pale Wakristo (wengi) wanapoamini Yesu ni Mungu.

Waislam tunaamini Yesu ni mtume wa Mungu, siyo Mungu.
 
Reactions: bbc

Mimi naamini Yesu ni Mwana wa mungu aliyetumwa na mungu kuja Duniani kukomboa ulimwengu
 
Kuna tofauti nyingi za kiitikadi kati ya Ukristo na Uislam lakini tofauti kubwa ya Ukristo na Uislam ni pale Wakristo (wengi) wanapoamini Yesu ni Mungu.

Waislam tunaamini Yesu ni mtume wa Mungu, siyo Mungu.
Mimi naamini Yesu ni Mwana wa Mungu aliyetumwa na Mungu kuja Duniani kukomboa ulimwengu
 
Mimi naamini Yesu ni Mwana wa Mungu aliyetumwa na Mungu kuja Duniani kukomboa ulimwengu
Waislam tunaamini Yesu ni mtume wa Mungu na si mwana wa Mungu. Pia Qur'an ina ujumbe huu muhimu sana kuhusu hilo...

Qur'an 4:171.
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha 171
 
Je kijana wa kiislam anaruhusiwa kuoa binti asiyekua muislam?
?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea huyo bint ni wa dini ipi. Maana Qur'an imetaja watu waliopokea vitabu kabla yetu. Sasa kujuwa ni wepi hapo kidogo kuna hitilafu za wanazuoni.

Binafsi nasema binti akiwa Mkristo, Myahudi, Msaba (sabeans) basi ruksa kijana wa Kiislam kumuoa na iwe jukumu la huyo kijana kumfahamisha Uislam ili watoto walelewe Kiislam.
 
Naam swadakta hiyo ndo kauli yenye nguvu عند العلماء
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali :

Sehemu nilipo ni mbali sana na msikiti, ni takribani km 25, na mwanaume ni wajibu kuswalia msikitini, je akiswalia nyumbani anapata daraja kama za mtu aloswalia msikitini kutokana na umbali ulivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
E naam hauwajibiki kuswali msikitini kwa umbali huo bila shaka ni mbali na utakuwa unaikalifisha nafsi yako na kujitia uzito,na Allah kasema
Swali :

Sehemu nilipo ni mbali sana na msikiti, ni takribani km 25, na mwanaume ni wajibu kuswalia msikitini, je akiswalia nyumbani anapata daraja kama za mtu aloswalia msikitini kutokana na umbali ulivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
وما جعل عليكم في الدين من حرج

[ AL -HAJJ - 78 ]
Wala hakuweka (Allah)juu yenu mambo mazito katika Dini.

Na katika hadithi swahihi Mtume wa Allah sala nasalamu ziwe kwake akasema

وأذا أمرتكم بشيء فأتو منه ما استطعتم
"Na nikiwaamrisheni jambo mlifanye kwa kadri muwezavyo."

Huwezi kusali umesimama kaa chini lakini uwe umesali,huwezi kukaa ulale lakini uwe umesali,msikiti uko mbali sali karibu au nyumbani lakini uwe umesali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijulishe tofauti ya kuoa/kuolewa na kuoana

Sent from my TECNO SA1 using JamiiForums mobile app
Neno la Kiswahili oana linamaanisha vitu viwili au zaidi vilivyoshabihiana, mfano viatu, ukichukuwa kiatu cha buti huwezi kukioanisha na raba ukavivaa.

Kuoa/kuolewa ni maneno ya Kiswahili yanayomaanisha maharusi wawili, mume huoa na mke huolewa kwa tamaduni za kimila au kizungu.

Kuoana ambayo ndiyo neno sahihi zaidi na ndiyo mfumo wa Kiislam. Kiarabu (ndiyo lugha mama kwa sharia za Kiislam) hutumika neno "zawaj" (to be a pair) ambalo linafanana zaidi na kuoana. Waislam tunaoana kisharia na hatuoi au kuolewa.
 
Swali :

Sehemu nilipo ni mbali sana na msikiti, ni takribani km 25, na mwanaume ni wajibu kuswalia msikitini, je akiswalia nyumbani anapata daraja kama za mtu aloswalia msikitini kutokana na umbali ulivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jitahidini sana hapo ulipo kupata ahali zako na majirani ili mpate "jamaa" hata ya kuanzia wawili.

Unaweza pia kupata jamaa ya wewe na ahali zako hapo nyumbani kwa kuanzia.

In Shaa Allah mkipata jamaa ya hapo nyumbani na majirani itakuwa mmepata kama wa msikitini na ndiyo itakuwa mwanzo mzuri wa kuanzisha msikiti.

الله أعلم
Allahu a'lam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…