Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Hawavai kwa ajili ya waarabu bali wanavaa kwa ajili ya dini yao.

Kwa hvyo hata wakiwachukia bado wanasonga mbele kwa sababu hawamfuati muarabu wanaifuata dini

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha


But Uislam si dini, it's a CULT.
 
Hamna shida kama ilivyo kwa baadhi ya watu wanafuata uzungu na ukristo.

Bila shaka hao wapo kila pande.

Kinachoangaliwa uislamu unasemaje,uislamu hausemi watu wafate waarabu,bali waislamu huwenda ikawa baadhi yao ndo wanafata waarabu.

Sasa tunajadili katika wewe unataka kumjadili anayetakiwa kufuata katiba
Wanafuata vyote.

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Mimi sijaona sehemu sijajibu,labda tu hukuridhishwa na vile wewe unataka kujibiwa.comment nyingi siwezi kupitia huko wakati najua nimeshakujibu.

Nasubiri wewe unijibu swala langu la kukata mkono
Pitia uzi juu kidogo utayakuta. Usiwe na haraka, nenda soma taratibu ujibu.

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Mimi sijaona sehemu sijajibu,labda tu hukuridhishwa na vile wewe unataka kujibiwa.comment nyingi siwezi kupitia huko wakati najua nimeshakujibu.

Nasubiri wewe unijibu swala langu la kukata mkono

ukiacha kuchagua jua umechagua 1
Haya, nitakuja kukuonesha wapi hujajibu. Sasa jibu hili...

 
Haya, nitakuja kukuonesha wapi hujajibu. Sasa jibu hili...
Siwezi nikajibu hili swali kwa sababu linahitajika kwanza ujibu swali langu lilee na KUKATA KIGANJA BADALA YA MKONO. Hili swala ukilijibu sasa na mimi ndo nitajibu kuhusu adhabu ya kaburini.

Usitake kupeleka mjadala point B wakati point A hatujaimaliza,hatuwezi kuingia point B wakati point A bado haijakaa sawa.nilotaka kujua kwamba unapinga maisha ya kaburini na wala sikutaka turefushe mjadala wakati kuna mjadala ungine.

Hayo maswali ya nyuma unayodai sijakujibu ndo uyaweke kwa sababu ndiyo maswali yanaendana na mada.

Wakati huo na mimi nasubiri jawabu lako juu ya suala hili.

"MTUME ALIKOSEA KUKATA WATU VIGANJA KWA KUWA QURANI INASEMA MKONO?"



ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Hiki uliingilia kati ukanishutumu shutuma kubwa sana ya kuipinga Qur'an.

Au hauna aya, unakwepa?
 
Hiki uliingilia kati ukanishutumu shutuma kubwa sana ya kuipinga Qur'an.

Au hauna aya, unakwepa?
Aya zipo zitaki kuweka hapa kuna mjadala wa nyuma haujaisha.nikiweka aya tutaanza kujadili aya hizo kiupana wakati mada haijaisha.

Kama tatizo nilikushutumu basi natarajaa kwamba NILIKOSEA KUKUSHUTUMU mama yangu badala yake hukuipinga Qurani(kwa mujibu)

Nimetarajaa ili nikusafishe na tuhuma hiyo ambayo tutakuja kuithibitisha kwa aya mbali mbali wakati ambao huu mjadala tumeumaliza.

AYA ZIPO,HADITHI ZIPO.

lakini tuu tutaendaje Point B wakati point A bado hatujaifikia.

Niwekee maswali ambayo unahakika sikukujibu hapo nyuma niyajibu alafu swali langu nawe ulijibu Tujue tunaanzia wapi.

kuhusu maisha ya kaburi nimeshajua huamini kwa sababu hijaona katika Qurani,sawa wewe hujaona na tutakuja kujadili hilo lakini baada ya kumaliza pooint A ambayo inatakiwa tuijadili kikamilifu japo kwa uchache wake.

WEKA MASWALI HAYO AMBAYO SIKUYAONA.
JIBU SWALI LANGU.
 
Hadithi ambazo hazilingani na Qur'an siziamini.

Nipe aya uishereheshe na hadithi au maulamaa naweza kukuelewa.
 
Hadithi ambao hazilingani na Qur'an siziamini.

Nipe aya uishereheshe na hadithi au maulamaa naweza kukuelewa.
Nimekuambia jibu swali langu la mkono na kiganja.

Alafu leta maswali unayodai kwamba sijayajibu.

Alafu hapo ndo tunaingia kwenye maisha ya kaburi.

Ulinambia swali langu umeliona nisiwe na haraka utajibu.

Na mimi nategemea hilo jibu tuendelee na mazungumzo,wewe unataka tuingie ndani ya mada ingine.

Tatizo nini?,nimekubali nilikupa tuhuma nzito na nimekiri ili turudi katika maudhui yetu,bado nasubiri majibu ya swali langu.

Na wewe uweke swali lako ambalo unasema sikukujibu hapa hapa hadharani.

Naimani wanaofuatilia ni wengi kwa hiyo tuwe hapa kwa ajili ya kuelimishana.mtu akikosea akubsli kakosea.

Nimekubali NILIKOSEA KUKUSHUSHIA TUHUMA NZITO haya basi tuendelee na maudhui yale ya mwanzo
 
Aya hiyo haina tatizo na wala kukatwa kiganja au mkono si tatizo wote ni mkono.

Isitoshe, hukumu ya kukatwa mtu mkono haijaanzia wakati wa Mtume Muhammad salla Allahu alayhi wa salaam, hukumu hiyo ipo hata kwa waliokuwa na vitabu kabla ya Qur'an, Qur'an imekuja kuyakinisha. Kwa hiyo mkono ukatwe wapi ni mambo yaliokuwa yakifanyika kabla.

Kama hiyo haitoshi, hadithi hiyo haifarikishi mtu. Kama ulinisoma vizuri huko juu, nilisema hadithi zinabaki kuwa hadithi tu siyo wahyi na ambao zinafarikisha Waislam tuachane nazo.

Au huwa hunisomi kikamilifu?

Kwanza hilo la kukatana mkono ni somo ambalo hata miezi mitatu hatutalimaliza tukiiingia kwenye lugha na balagha. Siendi huko kwa sasa natumai jibu langu umelisoma, sasa rudi kwenye swali ulilolirukia la "maisha ya kaburini" ambayo mimi siamini kuwa yapo. Nipe aya kama ulivyosema kuwa "zipo".
 
KWA HIYO MWIZI AKIIBA UKAUKATA MKONO MZIMA HAKUNA TATIZO KWA KUWA HAKUNA TOFAUTI?

Umetumia dalili ipi kutuaminisha kwamba makusudio ya mkono katika aya ile ni kiganja,kwa ada ipi?

 
KWA HIYO MWIZI AKIIBA UKAUKATA MKONO MZIMA HAKUNA TATIZO KWA KUWA HAKUNA TOFAUTI?

Umetumia dalili ipi kutuaminisha kwamba makusudio ya mkono katika aya ile ni kiganja,kwa ada ipi?
Da hunisomi.

Aya inasema mkono. Na kiarabu mkono ni popote kwenye mkono lakini hukumu hiyo haikuanza wakati wa Mtume Muhammad sala Allahu alayhi wa salaam. Yeye kaikuta na Qur'an imekuja kuyanikisha.

Kwa hiyo kama walikatana viganja ndicho walichokuta. Hakuna utata hapo. Au wakikatana mkono hakuna utata pia. Sijui unanielewa?

Hebu rudia kunisoma tena nikichokijibu bila papara.
 
Ndo mana nauliza kwamba akikatwa mtu mkono mzima kwa kuiba sio kosa? Sasa ilikuwa useme ndio au hapana.

Lakini pia kwa mujibu wa majibu yako maana yake kuna hadithi unazikubali kumbe wakati huo mimi nilikuwa nipo hapa kudhania kwamba huzikubali hadithi zote ama storia yeyote nje ya Qurani

Kumbe kuna hadithi unazikubali ambazo zimeipambanua hyo Qurani.

Ama sivyo nimedhania ?
 


Sasa unanipangia majibu? Ajabu hii kwa mtu mwenye uzoefu wa minakasha, kumbe wazoefu huwa mnapangiana majibu? Sijajuwa.

Hivi huwa unakurupuka bila kunisoma au vipi?

Narudia, kama walikatana viganja ndicho walichokuta. Hakuna utata hapo. Au wakikatana mkono hakuna utata pia. Sijui unanielewa?

Kuhusu hadithi ambazo si Qur'an zinabaki kuwa hadithi kama zilivyo riwaya na si wahyi. Kwa maana si maneno ya Mwenyezi Mungu.

Sizikubali hadithi zote kuwa ni maneno ya Allah. Zinabaki kuwa simulizi za watu wanazohadithia na zinabaki kuwa vyanzo kizuri cha historia. Kama ipo ambayo hainiingii akilini huwa sikubaliani nayo, hususan zile zinazo wafarakanisha Waislam.

Hayo yanahusiana na aya uliyoileta? Au hujaelewa majibu yangu? Kuwa Qur'an imekuja kuyakinisha, kukatana mkono kulikuwepo tangu kwa waliopewa vitabu kabla ya Qur'an.

Nini hapo huelewi?

Nasubiri aya ya Qur'an ya "maisha ya kaburini" kutoka kwako.
 
Habar madam
Napenda kujua je kulala bila nguo kwa wanandoa ni sawa na je ina faida gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar madam
Napenda kujua je kulala bila nguo kwa wanandoa ni sawa na je ina faida gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tupu zetu inapaswa zisitiriwe wakati wote kasoro wakati wa kuoga, kwenda haja au kuingiliana wanandoa.

Madhara ya kulala bila kujistiri ni pamoja na wadudu, mtu akaingia kwako ghafla, binaadam unaweza kuumwa ghafla wanaokuja kukusaidia ukawatia huzuni.

Pia inabidi tuone haya kwa viumbe wanaotuona na tusiowaona kama malaika na majinni.

Na kikubwa zaidi ni kumuonea haya Mwenyezi Mungu Muumba wetu anaetuona.
 
Kama walikatana viganja ndicho walichokuta walichokuta wapi?

Kama walichokuta katika vitabu vya kale ina maana mtume alikuwa hafati Qurani?

Kama walichokuta kwenye Qurani si ndo tunarudi pale pale kwamba wewe hadithi unazikubali kishingo upande kwa sababu hujanipa dalili ya kuonyesha kwamba hakuna tofauti ya kiganja na mkono.

Bali unazungumza vile ubongo unavokutuma.
Qurani imeshushwa ifuatwe na huyo mtume,hukmu ya kukata kiganja haimo katika Qurani na wewe unaikubali.

Sasa unaikubali vipi hiyo hikmu ambayo imo kwenye hadithi ilhali hadithi huzikubali?

Alafu usikimbilie hiyo mada kwa kuikwepa kwepa hii,huko tutafika,naona una hamu sana tufike huko.hapa kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…