Ohooo. Naona umekwepa la "mwizi", kitu ambacho umeandika wewe mwenyewe. Naona pia umekwepa la "maisha ya kaburini" kitu ambacho ukinishutumu kutokukifata, unarudi na porojo ambazo nimeshazijibu huko.
Bado nasubiri kutoka kwako aya za Qur'an zinazoongelea "maisha ya kaburini".
Sasa nasuburi pia ya " mwizi" kupigwa mawe. Au ulikosea?
Unasubiri ya kupogwa mwizi mawe hadithi au aya?
Kama unasubiri aya hutoipata ndani ya Qurani.zipo hadithi zinathibitisha jambo hilo.
Ninachokuambia kwamba kuzikataa hadithi ni upotevu na kwenda kinyume na Qurani,na wewe unazikataa hadithi na mafundisho ya mtume huyataki jambo ambalo limekemewa na Qurani.
Qurani ni mafundisho ya Allah na hadithi ni mafundisho ya mtumi,wewe huzitaki unadhani una salama hapo,sasa hivi ninachokuambia ni ujumla wa mambo kwamba kuzikataa hadithi sahihi ni upotevu.
Wewe si ndo unakataa mafundisho ya mtume yaliyothibiti,au huyakatai wewe?
Mfano wa hadithi inayosema mzinifu aliyeowa auwawe ni hii
ﻦِ ﻣَﺴْﻌُﻮﺩٍ ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪُ ﻋﻨﻪ ﻗﺎﻝَ : ﻗﺎﻝَ ﺭﺳُﻮﻝُ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : ( ( ﻻَ ﻳَﺤِﻞُّ ﺩَﻡُ ﺍﻣْﺮِﺉٍ ﻣُﺴْﻠِﻢٍ ﺇﻻّ ﺑﺈﺣْﺪَﻯ ﺛَﻼَﺙٍ : ﺍﻟﺜَّﻴِّﺐُ ﺍﻟﺰَّﺍﻧﻲ، ﻭَﺍﻟﻨَّﻔْﺲُ ﺑﺎﻟﻨّﻔْﺲِ، ﻭَﺍﻟﺘَّﺎﺭِﻙُ ﻟِﺪِﻳِﻨِﻪِ ﺍﻟْﻤُﻔَﺎﺭِﻕُ ﻟِﻠْﺠَﻤﺎﻋَﺔِ ) ) . ﺭَﻭَﺍﻩُ ﺍﻟْﺒُﺨَﺎﺭِﻱّ ﻭَﻣُﺴْﻠِﻢٌ
toka kwa Ibn Mas'uud ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ambaye alisema: Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ kasema:
((Damu ya Muislamu haipasi kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anaeeacha dini na akajifarikisha na jama’ah (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake))
[Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Hii hadithi sahihi haijapatapo kudhoofishwa na mwanachuoni yeyote yule juu ya usahihi wake na inatueleza kwamba mzinifu aliyeowa adhabu yake ni kifo,lakini Qurani huikuti hii hukmu,ipo ya bakora mia.
Wewe unaweza kuipinga hii hukmu ya hadithi kwa kuwa haipo kwenye Qurani?
Ukiikataa basi jua wewe ni katika waleee waliotajwa na aya hii
ومن يشاقق الرسول من بعد ما تبين له الهدى ويتبع غير سبيل المؤمنين نوله ما تولى ونصله جهنم وساءت مصيرا
[ AN-NISAAI - 115 ]
Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu.
Uongofu wa hadithi umedhihiri wazi wazi juu ya usahihi wake na himmu yake.