Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Nimeritad maana nimeujua ,hata wewe ukitoka nje ya boksi utaritad na kumpokea Yesu awe Bwana na mwokozi wa Maisha yakoKuzaliwa na Waislam hakumaanishi unaujuwa UISLAM.
Ungeujuwa Uislam usingethubutu kuritadi.
Sasa rudi ulete hadith siyo porojo.
Nimekupa hadithi umezikataa ,Hauujuwi Uislam.
Leta hizo hadith tukufundishe au kiri hauna uulize kingine.
Huu siyo uzi wa porojo.
Hadith zote ni hadithi na zitabaki kuwa hadith kwa maana halisi ya neno hadith.
Naamini, hakuna hata moja ambayo ni "hadith ya mtume" kama wengi wanavyotaka ifahamike. Hizo ni hadith (riwaya) za watu wengine walioelezea wanavyodhani au wanavyofikiri ilivyokuwa wakati wa Mtume au waliokuwa karibu na Mtume, zinaweza kuwa kweli au uongo. Zote za kuokoteza okoteza miaka takriban 200 baada ya Mtume Kufariki.
Mfano, Mimi nikwambie "Magufuli kasema hasaidii mtu ataesombwa na mafuriko Rufiji", hiyo hadith ni ya Magufuli au yangu namuongelea Magufuli?
Au Mimi nihadithie " nilimuona Nyerere kashuka kwenye gari anasalimiana na watu Lumumba", hiyo hadith ya Nyerere au yangu naelezea ya Nyerere?
Mimi nasema hizo ni hadith zangu si za Magufuli wala Nyerere.
Ingawa naamini kuwa hizo hadith zote si za Mtume Muhammad na kwa kuwa hizo hadith zote zipo na waliozikusanya na kuziandika wamejitahidi na hakuna kati yao aliyeandika kuwa hizi "hadith za mtume" (kama yupo basi kakosea) bali wanaandika "kahadithia fulani...". Waliandika kama historia tu, miaka takriban 200 baada ya Mtume Muhammad na masahaba (marafiki) zake kufariki.
Katika hizo hizo pia zote zinazopingana na mafundisho ya Qur'an sizikubali.
Zote zenye lugha isiyokuwa na adabu sizikubali.
Zote zote ambazo hukuti maudhui yake kwenye Qur'an sizikubali.
Umeelewa? Wajulishe na wenzako wanaojiita Zurri na safuher.
Hayo majina uliowataja kwenye hizo hadithi zako wote hawakuwahi kuandika KISWAHILI.Nimekupa hadithi umezikataa ,
Kama...ni za uongo wewe ndiwe unatakiwa uzikanushe kwa kuleta halisi
Hiyo ndio kanuni
Uislamu naujua ,na niliukana ndani ya msikiti mji mwema kigamboni mbele ya shekh .Nimezaliwa humo na kukulia madrasa ,
Muombe Mungu akuoneshe Njia ya kweli na Uzima .....usijifungie ndani ya boksi
Kama hizi hadithi ni uongo au napotosha leta za ukweli ,
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, "Ye yote mwenye kutukana, basi huyo amejambiwa na Shetani katika Mdomo wake." (Fat'hul Baary J. 10, Uk. 176)
SHETANI ANALALA KWENYE PUA ZA WAISLAMU:
Amesimulia Abu Huraira (r.a) Mtume (s.a.w) alisema “Mmoja wenu anapoamka kutoka usingizini, basa atawadhe na apandishe maji puani, na apenge mara tatu, kwa sababu shetani alilala ndani ya tundu za pua yake” (Bukhari, Hadithi na. 516, juzuu ya 4)
Kasema Mtume (s.a.w) “Anamwijia mmoja wenu shetani katika sala, basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi yule mtu inamwijia fikiria ya kuwa umemtoka upepo (kajamba) nae haukumtoka, basi akiona hali hiyo asiondoke kwenye sala mpaka asikie sauti ya kumtoka huo upepo au anuse harufu yake”. (KITABU CHA MKWELI MWAMIU, JUZUU YA 1 -2 HADITHI NA. 74, UK 42)
| Reference | : Sahih Muslim 2785 |
| In-book reference | : Book 52, Hadith 1 |
| USC-MSA web (English) |
Bado nasubiri ulivyosema uongo wako ulioizulia Qur'an kuhusu Aya za adhabu ya kaburi. Nasubiri. Unaona haya kukiri kuwa hujaziona? Usione haya ulidanganywa na hadith za uongo....Hujui dini na ndio maana maswali yangu unayakimbia.
Bado nasubiri ulivyosema uongo wako ulioizulia Qur'an kuhusu Aya za adhabu ya kaburi. Nasubiri. Unaona haya kukiri kuwa hujaziona? Usione haya ulidanganywa na hadith za uongo....
Una mengi ya kujifunza. Soma kijana...
Qur'an 2:
256. Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 256
257. Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. 257
Onana na imam wa hapo msikitini. Sura moja ya mistari saba inakuchukuwa siku ngapi kufundishwa ukaielewa? Sura hii tu inakutosha kujifunza na kuanzia kuswali, mengine atakuelekeza imam...Naendaje na huku sijui kiarabu
Kasome nilikujibu. Uliongezea maneno yako nikakupa ya uso.Sasa kama hujibi maswali yangu na aya moja tu nimekuwekea lakini umeshindwa, hii inakuwa haina maana na nakuwa napoteza muda tu.
Silei ujinga bi mkubwa. Jibu maswali yangu kisha nikuwekee nyingine. Itifaki izingatiwe tu.
Bi mkubwa wewe ni muongo, yale maelezo yamefafanua ile aya, ndio maana ulipo kataa nikakuuliza utuambie wewe sasa lile tamko la "...adhabu mara mbili" lina maanisha nini, mpaka sasa hujajibu hili swali.Kasome nilikujibu. Uliongezea maneno yako nikakupa ya uso.
Nikakwambia hakuna adhabu ya kaburi hapo. Unataka kulazimisha?
Qur'an ipo waziwazi.
Wewe Acha ujinga. Utafafanua vipi Aya isiyo na adhabu ya kaburi useme ni adhabu ya kaburi? Qur'an imekamilika hautakiwi uongeze yako.Bi mkubwa wewe ni muongo, yale maelezo yamefafanua ile aya, ndio maana ulipo kataa nikakuuliza utuambie wewe sasa lile tamko la "...adhabu mara mbili" lina maanisha nini, mpaka sasa hujajibu hili swali.
Nikakuuliza tena swali dogo, kikao cha mwisho kabla ya kutoa salamu katika sala huwa unakisomaje ? Hili nahisi mpaka kesho huwezi kulijibu.
Swali lingine ni kuhusu hadithi, hili nimeoma ndio umelijibu sasa hivi. Sasa wewe katika mizani ya Uislamu wewe sio Muislamu, maana unaipinga Qur'aan wazi wazi.
Swali lingine, ibada zako huwa unazifanyaje bi mkubwa ?
Sasa hapa kwangubi mkubwa lazima utaumia, na laiti kama ungekuwa unajibu maswali,hili jambo lingekuwa limeisha kitambo sana.
Wewe Acha ujinga. Utafafanua vipi Aya isiyo na adhabu ya kaburi useme ni adhabu ya kaburi? Qur'an imekamilika hautakiwi uongeze yako.
Soma Qur'an inakufundisha nini...
Qur'an 6:
19. Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha. 19
20. Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao. Wale walio zikhasiri nafsi zao hawaamini. 20
21. Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi. 21
Saidianeni kwanza kutafsiri neno hili inapoanza hiyo hadithi...
ﻫﺬﺍ ﺍﻟﺤﺪﻳﺚ ﺭﻭﺍﻩ ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
Semeni Kiswahili chake nini?
Nacheka tulia, nikufundishe. Wewe si ulidai na kukataa ule ufafanuzi wangu. Sasa katika ile aya lile tamko "....adhabu mara mbili" lina maanisha nini ? Hili ndio swali langu.
Sasa usikimbie swali.
Shukran sana. Nadhani na Vijana, Zurri na safuher walioogopa au walioshindwa hata kujaribu kujibu hilo watapitia kusoma. Ahsante sana kwa kuwasaidia lakini kidogo umekosea tafsiri ya neno ﺭﻭﺍﻩ nalo si "ilivyoandikwa" bali ni "ilivyosimuliwa".
Bi mkubwa acha porojo jibu swali langu nililo kuuliza. Nakusaidia tena hapa nakuwekea tarjama ya aya.Usije ukakimbia wewe tu.
Ingawa hujaiweka tena hiyo Aya lakini naifahamu.
Anza kupata darsa...
Kwanza elewa kuwa Aya hiyo inaongelea adhabu mara tatu si mara mbili pekee. Kasome vizuri kisha urudi useme umeziona mara mbili pekee unazozitajataja au mara tatu ninazokufundisha mimi?
Tuanzie hapo.
Bi mkubwa una hangaika sana.Shukran sana. Nadhani na Vijana, Zurri na safuher walioogopa au walioshindwa hata kujaribu kujibu hilo watapitia kusoma. Ahsante sana kwa kuwasaidia lakini kidogo umekosea tafsiri ya neno ﺭﻭﺍﻩ nalo si "ilivyoandikwa" bali ni "ilivyosimuliwa".
Kwa hiyo tafsiri sahihi ya maneno hayo ni "Hadith hii ilisimuliwa na Al-Bukhari".
Sasa kama inasema "ilisimuliwa na ..." Ina maana Bukhari ndiyo mwandishi?
Bi mkubwa acha porojo jibu swali langu nililo kuuliza. Nakusaidia tena hapa nakuwekea tarjama ya aya.
Anasa Allah aliye juu :
“Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanafiki; na katika wenyeji wa Madiynah pia wapo waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa” (at Tawbah : 101).
Haya jibu swali langu sasa.
Tena naona raha kweli kuwapa darsa hapa. Nafahamu linawaingia, na bado.Bi mkubwa una hangaika sana.
Usione haya hujaziona adhabu mara tatu hapo?
Porojo? Mimi au wewe uliyeziona mara mbili Tu na unapachika eti ni adhabu za kaburi. Khaaa; Nakushangaa sana kijana kutaka Qur'an iwe kama utakavyo wewe kwa sababu ya hadith ya uongo.
Sasa hapo kaburi lako liko wapi kijana?
Nenda kaanzie Aya ya 73 ukielewe hicho kisa. Hakuna adhabu ya kaburi hapo. Halafu hiyo uliyoiweka siyo Qur'an kijana ni 'tarjama" tu. Unarudia makosa yale yale ya wasio na kitabu "original" kijana.
Narudia, hakuna hapo adhabu ya kaburi. Usijidanganye. Tafuta kingine.