Hadith zote ni hadithi na zitabaki kuwa hadith kwa maana halisi ya neno hadith.
Naamini, hakuna hata moja ambayo ni "hadith ya mtume" kama wengi wanavyotaka ifahamike. Hizo ni hadith (riwaya) za watu wengine walioelezea wanavyodhani au wanavyofikiri ilivyokuwa wakati wa Mtume au waliokuwa karibu na Mtume, zinaweza kuwa kweli au uongo. Zote za kuokoteza okoteza miaka takriban 200 baada ya Mtume Kufariki.
Mfano, Mimi nikwambie "Magufuli kasema hasaidii mtu ataesombwa na mafuriko Rufiji", hiyo hadith ni ya Magufuli au yangu namuongelea Magufuli?
Au Mimi nihadithie " nilimuona Nyerere kashuka kwenye gari anasalimiana na watu Lumumba", hiyo hadith ya Nyerere au yangu naelezea ya Nyerere?
Mimi nasema hizo ni hadith zangu si za Magufuli wala Nyerere.
Ingawa naamini kuwa hizo hadith zote si za Mtume Muhammad na kwa kuwa hizo hadith zote zipo na waliozikusanya na kuziandika wamejitahidi na hakuna kati yao aliyeandika kuwa hizi "hadith za mtume" (kama yupo basi kakosea) bali wanaandika "kahadithia fulani...". Waliandika kama historia tu, miaka takriban 200 baada ya Mtume Muhammad na masahaba (marafiki) zake kufariki.
Katika hizo hizo pia zote zinazopingana na mafundisho ya Qur'an sizikubali.
Zote zenye lugha isiyokuwa na adabu sizikubali.
Zote zote ambazo hukuti maudhui yake kwenye Qur'an sizikubali.
Umeelewa? Wajulishe na wenzako wanaojiita
Zurri na
safuher.