Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Haya maswali au darasa...

Okay mie naanza.
Faiza, ni kitu gani unakiogopa mno hapa duniani ukiacha muumba wako.

Swali jingine.. ni tukio gani la kijasiri ushawahi lifanya na hutolisahau
 
Hayupo a maswali au darasa...

Okay mie naanza.
Faiza, ni kitu gani unakiogopa mno hapa duniani ukiacha muumba wako.

Swali jingine.. ni tukio gani la kijasiri ushawahi lifanya na hutolisahau
Nnaogopa kuvunja sheria za nchi.

Nimeshawahi kuruka urefu wa zaidi ya meters 100 (kama sikosei ni 111) kwa kutumia kamba maalum (bungee jumping ) katika daraja la reli la Victoria, mto Zambezi mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.

Sitosahau maisha yangu na niliapa sitorudia tena.
 
Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:

Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Mashaallah
 
Unanishauri nini kuhusu katabia kangu kakupenda wanawake wazuri tu, wanawake wabaya sina hisia nao kabisa hata nimkute yupo kama alivyo zaliwa.
"HONGERA SANA KWA KUTUELIMISHA KATIKA NYUZI MBALIMBALI HUMU JAMVIN"
 
Kwa nini Waislamu wanafanya maamuzi kwa niaba ya Mungu.Kwa mfano ukikashifu Uislamu utaadhibiwa na Waislamu badala ya kumwachia Mungu.Ina maana Mungu wa Waislamu hana uwezo?

Muislam hafanyi kazi ya Mungu, Muislam hapendezwi Mungu kukashifiwa na wasio amini. Pia Waislam ni wastahamilivu na wenye kusubiri sana. Jinsi Waislam wanavyokashifiwa wangekuwa hawana subira basi dunia hii pasingekalika.

Isitoshe, kisasi ni haki.

Ukiona mtu kaukashifu Uislam na Waislam wakamchukulia hatua huyo mtu basi ujuwe kavuka mipaka.

Na hilo si kwa Waislam pekee, tunaona hata kwa wasio Waislam wanachukua hatua kali kwa kukashafiwa wao.

Ukiona mtu anakashifiwa Mungu wake na yeye anachekelea tu ujuwe huyo hana imani na Mungu wake.
 
Unanishauri nini kuhusu katabia kangu kakupenda wanawake wazuri tu, wanawake wabaya sina hisia nao kabisa hata nimkute yupo kama alivyo zaliwa.
"HONGERA SANA KWA KUTUELIMISHA KATIKA NYUZI MBALIMBALI HUMU JAMVIN"
Nnakushauri tafuta mzuri mmoja muoane. Wazuri hawaishi utaekwisha ni wewe.
 
Mod huyu mwanamke/mwanaume anajaza server ya JF.
Hapa anatafuta umaarufu tu na kick za kipumbavu.
 
Kwa nini dunia nzima Waarabu ndio wa pili wa mwisho kwa ujinga baada ya Waafrika wakati ustaraabu ulianzia Uarabuni.
Hiyo tafiti ulifanya wewe au asiyewapenda Waafrika?

Hapo kwenye Waarabu na Waafrika pamenichanganya kidogo au huyo mtafiti alikuwa haelewi kuwa Waarabu wengi ni Waafrika.
 
Mod huyu mwanamke/mwanaume anajaza server ya JF.
Hapa anatafuta umaarufu tu na kick za kipumbavu.
Kwani JF walikwambia wana ration ya data input kwenye server zao?

Au hauelewi kuwa JF ni "user's generated content site" na ni furaha na fahari kwao kila tunavyochangia mada kwa wingi? Kama ulikuwa huelewi hilo hebu scroll chini ujisomee JF wanasemaje.

Kiki nnaitafuta na nimeipata. Vipi, inakuumiza?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kwani JF walikwambia wana ration ya data input kwenye server zao?

Au hauelewi kuwa JF user's generated contents na ni furaha na fahari kwao kila tunavyochangia mada kwa wingi?

Kiki nnaitafuta na nimeipata. Vipi, inakuumiza?
We una roho mbaya sana na post zako wakati wa uvamizi wa Alshab huko garisa ulichekelea kimoyomoyo na ukafungua multiple ids ukachangia.
You are a destructive woman...nafsi yako inakusuta.
unapenda kutafuta kick za kijinga.
 
Weka ushahidi kama u mkweli.

Umekushinda ufataani wa server sasa unakuja na ufataani wa Alshabab ?

Watu tumemuona King Kiki itakuwa kiki za kijinga ?
 
Back
Top Bottom