Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Nitolee wazimu wako, kwanza sijamwambia wewe ni mzinzi nimemwambia acha uzinzi, hata tuwapo katika nyumba za ibada mbona tunaambiwa acha uzinzi kwani wana maana waumini woote ni wazinzi? Hilo ni neno la kukumbushana kama si mzinzi sioni sababu ya kuling'ang'ania
 
Wewe kimwanamke una "UNAFIKI" na ni dhambi mbaya sana.

Ukimwambia mtu (maajabu zaidi usiyemjua) kuwa acha uzinzi...maana yake huyo mtu ni mzinzi.

Ukimwambia mtu acha wizi...means huyo mtu ni Mwizi

Ulikuwa na uhakika na uzinzi wa huyo uliyemwambia acha uzinzi?

Ulimkuta katika uzinzi?

Jibu hayo maswali.

Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app
 
Nilimkemea kutokana na uandishi wa statement yake , sasa mineshasema na kama radhi nilishamuomba haya niambie na wewe unataka nini sasa!?
 
FaizaFoxy naomba unipatie majibu mujarab ya maswali haya:

- Uligraduate 1982, Bsc in electronic engineering, specialised in Telecommunications.

Naamini kwa wakati huo kulikuwa na wasomi wachache sana wa course hiyo hapa nchini.

JE: uliwahi kufikiria kuanzisha Firm yako au kuisaidia Tanzania kwa elimu yako kwa namna yoyote?

Au ulipoolewa ukaamriwa na mumeo utulie ndani na kumpikia pamoja na kumtunzia watoto kama wanawake wengi wa kiarabu wanavyoishi baada ya ndoa?

JE, Unazungumziaje uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania?

Huoni kama kwa Elimu, hekima yake na huruma angefaaa kabisa pia kuwa Rais wa URT?

Je huyo Mheshimiwa ameolewa? Unaweza kutuwekea picha ya Mumewe (I also understand about privacy but she is an icon)


Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app
 
Swali langu umeruka Kwa nini dunia nzima wanaopigana vita na vurugu ni Waislamu zaidi e.g. Libya,Somali,Yemen,Syria,Iraq,Afghanistan,Uarabuni nk.
Nitalijibu, usiwe na haraka ni swali zito sana linataka subra.
 

Nilipomaliza masomo yangu sikuwa na mpango wowote wa kuja kufanya kazi Tanzania kwani nilikuwa tayari nnaishi Canada kwa miaka mingi kabla na baada.

Mimi sikuolewa, tumeoana na mume wangu.

Sijawahi kutokufanya kazi toka tuoane na mume wangu mpaka nilipostaafu kazi za kuajiriwa labda breaks za hapa na pale za maternity na kuhama nchi, kazi za mume wangu zilimfanya ahamishwe mara kwa mara nchi nyingi duniani.

Nnaona hapo kwenye kuolewa na kutokufanya kazi umewa single out "wanawake wa Kiarabu" pekee. Binafsi nnawajuwa wengi wasio Waarabu ambao hawafanyi kazi baada ya kuolewa. Na kila niwaonapo nnatamani sana nami ingekuwa hivyo, kuwapa family yangu 100% ya attention yangu. AlhamduliLlah haikuwa hivyo lakini sasa najaribu kulipiza kwa wajukuu.

Kuhusu Bi Samia Suluhu ntakujibu baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…