Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kosa kubwa la umma kabla ya mengine ni ujinga. Ujinga ndio umezaa mengine yoote. Ujinga ndio umezaa magaidi. Umezaa washirikina wengi tu tena wengi wao ndio maimamu. Umezaa watu wasiojiweza. Kuna maswali ya kujiuliza kabla ya kutaja sababu za nje je makafiri ndio wanaotuzuia tusisome dini? Je ndio waozuia wanawake wasijistiri? Ndio wanaolazimisha tuishi maisha ya kipagani? Ndio wanatufanya tuipuuze mila ya nabii Ibrahimu alayhis salaamu na kufuata mila za hayawani? Ujinga. Na hapa ujinga nnaokusudia ni wa kutokusoma dini
 
Kama ambavyo umefanya jitihada za kupata elimu dunia nzuri ndivyo unavyotakiwa kujitahidi kusoma elimu akhera. Umetumia miaka 17 za zaidi kusoma dunia vipi utaijua dini kwa kusoma article kwenye mtandao? Ulishasikia mtu amekuwa injinia au daktari au mwalimu kwa kusoma articles? Kusoma mwenywe kwenye mtandao ni hatari maana mtandao umejaa mazuri na mabaya kibao na wengi wamaeangamia kwa kujifunza wenyewe mfano kwa kujiunga na ugaidi au kuwa waislamu poa. Unatakiwa ukae mbele ya mwalimu akufundishe. Utenge muda kwa ajili ya hili utumie mali yako kulifanikisha jili. Elimu ya dunia uliyoipata itakusaidia kwa miaka mochache tu utayoishi lkn elimu ya Akhera ndio itayokusaidia kwenye maisha yako mengine. namuomba Allaah akusahilishie na akubariki
 
Japo swala langu hujanifafanulia vzr ninlo lingine tena, tuna mifugo mf. Ng'ombe ya kifamilia inakaa shmu moja yupo baba ndo kiongoz wa kaya , na ktk zizi moja kila mmoja ana ng' ombe wake (zinakaa kifamilia), je zaka yake inakuaje hpo?
Zake yake itatolewa kwa pamoja maadamu wanakaa zizi moja. Mtamchagu ngombe mmoja na kumtoa kisha wao watamthaminisha huyo ngombe mfano gharama yake ni milioni moja. Kisha watachangia gharama kwa kuzingatia idadi ya ngome wa kila mtu. Mfano kwenye ngome 100 mmoja ana 20 atachangia asilia 20 za gharama, mwingine 30 atachangia asilia 30 na mwingine 40 atachangia asilimia 40. Mfano ikiwa ngombe alochaguliwa ni wa huyu mwenye ngome 20 hawa wenzake watampa yeye michango yao. Na Allaah ni mjuzi zaidi.
 
Naomba unijuzu ktk swala ya msafiri, ww umetoka ugenini unaelekea nyumbani ( maksz yko) ukanuia kukusanya mfano swala ya dhuhur na laswiri ,ukafka ktk wakati wa swala ya al- asri je hzi swala unaziswalije?
Ukishafika nyumbani utaunganisha adhuhur na alasiri lakini utasali rakaa nne nne hutapunguza rakaa
 
Usahihi ni kuzisali zote kwa pamoja rakaa nne nne kwa kuanza na dhuhr kisha alasiri. Mtu anaruhusiwa kukusanya swala ya dhuhr na alasir au magharib na ishaa hata kama sio msafiri hasa anapokuwa na sababu za msingi mfano daktari anafanya upasuaji na.mida ikagongana au wanafunzi muda wa swala ndio pamewekwa mtihani. Atakusanya lakini hatopunguza
 

Ma sha Allah.

Darsa linachangamka.
 
Deviated cult just ignore them
 
Njoo pm nina mfanyakazi mwenzangu aliugua kama hivyo akashindwa kutembea kabisa kama mwaka lkn alitibiwa na sasa anachapa kazi ntakuunganisha naye
 
Faiza, what is developmental perspective research please?


Developmental Perspective Research ni dhanna ya tafiti za kuelewa/kumfanya binaadam kuanzia utotoni akuzwe/akuwe kwa kujengwa kwa kina cha tafiti.

Tafiti zinaendelea kila kukicha na "papers" nyingi zimeandikwa kuhusu hayo.

Miaka ya nyuma huko China walikuwa na dhanna na walienda mbali zaidi katika tafiti hadi kufikia kuweka vituo vya kulelea na ili kutimiza na kutaka kujenga taifa lenye maendeleo ya kila aina wakabuni vituo vya kulelea watoto na kuwakuza na kuwajenga vile walivyopanga.

Mfano, "forecasts" zilipoonesha kuwa miaka 25 ijayo watahitajai wahandisi kadhaa, madaktari kadhaa, madereva kadhaa, wakulima kadhaa...

Basi walichukuliwa watoto wangali wachanga na kuanza kulelewa kuwa mkulima amma mhandisi na kadhalika, katika kituo mahsusi, basi kuanzia michezo yake, maongezi yake, mafunzo yake, watu wanaomzunguka yote yanaongelea kilimo tu, hali kadhalika kwa dereva, mhandisi, rubani na wengineo. matokeo hayakuwa mema sana.

Nchi za magharibi wao approach yao ni ya "on going research" kwa hayo, na kuzitumbukiza hizo researches (tafiti) katika maisha ya kila siku ya kuanzia mtoto anapozaliwa. Hakuna njia mojawapo bali ni mchanganyiko wa tafiti.

Unaweza kusoma zaidi hapa: Developmental Perspective: Definition & Explanation - Video & Lesson Transcript | Study.com

Napenda pia kukujulisha kuwa Uislam umeongelea kwa kina na umeainisha malezi na makuzi ya wototo miaka 1,400 iliyopita na hakuna hata mmoja katika wakosoaji wote wa Uislam aliyepinga namna ya malezi ya watoto yanavyofundishwa Kiislam. Soma zaidi: http://www.reviewofreligions.org/11414/parenting-child-development-an-islamic-perspective/
 


Vipi tutatuwe tatizo hilo?
 
Vipi tutatuwe tatizo hilo?
Dawa ya ujinga ni kuwekeza kwenye elimu sahihi ya dini. Kimsingi kuna elimu ya dini ambayo kila mmoja yampasa kuijua na akitojua anapata dhambi. Hii ni elimu ambayo atamfanya mtu awezw kumuabudu muumba inavyopaswa na kuweza kujua hukmu za mambo yote ya msingi yanayoyazunguka maisha yake. Hii isomwe kuanzia udogoni. Mwanafunzi akifika chuo kikuu awe ni mtu anayejitambua misingi yote ya dini na miamala ya kijamii. tusiwe ma scarecrow wengi kama wa sasa ambao hawakuandaliwa na hawajiamini hata kufanya uadilifu tu mtu aogopa. Hii ni elimu ya lazima. Halafu kuna elimu za ubobezi katika mambo mbalimbali kama lugha nk hayo sasa yawe ni kw masheikh. Ukitaka kupima kiwango cha ujinga angalia namna watu wanavyotekeleza ibada ya kila siku mara yano sala.
 
Mie naomba kuuliza swali, nasikia Mtaa wa Bibi Titi Mohamed uliitwa hivyo toka miaka ya nyuma kisha kupewa jina la Mtaa wa UWT baada ya kesi yake ya uhaini na alipokuja samehewa ukarudishiwa jina Bibi Titi Mohamed.
Je awali ya hayo yote huo mtaa ulikuwa unajulikana kwa jina gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…