FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
-
- #1,201
Kwanza kabisa hongera sana FaizaFoxy wewe ni mmoja ya member wa JF ninaowakubali sana kwa kujenga hoja na uvumilivu hapa JF,nakumbuka huko nyuma ulipigwa ban tukakuombea kwa Mod wakufungulie,Maswali yangu
1.Unafikiri vyama vya siasa vya upinzani vinakosea wapi ili kuiondoa CCM ?
2.Tanzania ni maskini licha ya rasilimali nyingi tulizonazo na wanasiasa wanatudanganya kila wakati wa uchaguzi,kwa mtazamo wako ni mambo gani tunapaswa kuyapa kipaumbele ili tuweze kusonga mbele ?
3.Umekuwa mmoja ya watu ambao mnalalamika sana waislamu wananyimwa fursa kwenye teuzi mbalimbali za serikali,huoni kama chanzo cha tatizo ni kwamba waislamu hawajaweka kipaumbele kwenye elimu dunia na pia wamekuwa hawana umoja kama walivyo wakristu ?
1. Vyama vya siasa vya upinzani vinaongelea sana "watu" na "matukio" havina "ideas" mpya yoyote. Hilo ndiyo kosa lao kubwa.
2. Tanzania si masikini bali Watanzania ni masikini na umasikini wetu ni wa akili. Hapa nnaungana na Lowassa kwa kumnukuu tu, "elimu, elimu, elimu". Watanzania inabidi tufumuwe kabisa mfumo wetu wa elimu uliopo sasa na tuliourithi ukoloni. Mfumo mzima umeelekea katika kutengeneza watumwa mambo leo na si katika kutengeneza "ma bosi" wa kesho.
3. Nnakuomba pitia hapa: Waislam wa Tanzania na tatizo la udini katika Wizara ya Elimu