Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwanza kabisa hongera sana FaizaFoxy wewe ni mmoja ya member wa JF ninaowakubali sana kwa kujenga hoja na uvumilivu hapa JF,nakumbuka huko nyuma ulipigwa ban tukakuombea kwa Mod wakufungulie,Maswali yangu

1.Unafikiri vyama vya siasa vya upinzani vinakosea wapi ili kuiondoa CCM ?

2.Tanzania ni maskini licha ya rasilimali nyingi tulizonazo na wanasiasa wanatudanganya kila wakati wa uchaguzi,kwa mtazamo wako ni mambo gani tunapaswa kuyapa kipaumbele ili tuweze kusonga mbele ?

3.Umekuwa mmoja ya watu ambao mnalalamika sana waislamu wananyimwa fursa kwenye teuzi mbalimbali za serikali,huoni kama chanzo cha tatizo ni kwamba waislamu hawajaweka kipaumbele kwenye elimu dunia na pia wamekuwa hawana umoja kama walivyo wakristu ?

1. Vyama vya siasa vya upinzani vinaongelea sana "watu" na "matukio" havina "ideas" mpya yoyote. Hilo ndiyo kosa lao kubwa.

2. Tanzania si masikini bali Watanzania ni masikini na umasikini wetu ni wa akili. Hapa nnaungana na Lowassa kwa kumnukuu tu, "elimu, elimu, elimu". Watanzania inabidi tufumuwe kabisa mfumo wetu wa elimu uliopo sasa na tuliourithi ukoloni. Mfumo mzima umeelekea katika kutengeneza watumwa mambo leo na si katika kutengeneza "ma bosi" wa kesho.

3. Nnakuomba pitia hapa: Waislam wa Tanzania na tatizo la udini katika Wizara ya Elimu
 
Unasema kweli kwamba miaka 38 uko kwenye ndoa? Basi shikamoo mamdogo. But you behave quite different from your true age!!!! "Kama ni kweli!!!"

Naam, ni ukweli kabisa.

Unanionaje "behaviour" yangu? Wakati hapa unayoyaona ni maandiko tu.
 
Utaweza kunijibu haya maswali.
1. What is philosophy in your life.
2. What is time?
3. Which one is more power, love or fear.
4. Are you religious or spiritual
5. Are you confrontational?
6. Jina lako lina maana gani? Na unaamini vipi maana yake sababu zipi zilizofanya ukapewa jina lako halisi la kuzaliwa, na kwa misingi ipi.

Ni hayo tu.
 
Hapana, usichanganye mada. Wazaramo wana lugha mama yao, nacho ni Kizaramo.

Jinni ni jina linalotokana na lugha ya Kiarabu, kumbuka hilo. Kwa hiyo kubadili jina ni ujinga tu. Kamusi ya Kiswahili imeandikwa na watu kama mimi na wewe na kama wameandika "jini" basi sina budi kusema uelewa wao kwa jina hilo ulikuwa ni finyu kama wako.

Jina si neno, neno linaweza kuwa jina pia na jina linaweza kuwa neno pia. Lakini Jinni kwa maana halisi inavyotumika hapa ni jina.
Wewe ungekuwa mwalimu hufai hata kufundisha mbwa.Mimi si mwalimu wa kiswahili lakini mtu yeyote aliesoma kiswahili vizuri hawezi kukubaliana na utumbo wako kuhusu hilo tu dogo neno jini.Wewe andika kama unavyotaka lakini kama ungekuwa mtihani lazima hapa ungekula mweleka.Kwenye mada ya TEZI DUME pia uliemtumia kueleza nae amechapia kwa kudanganya wasomaji kueleza vitu vya uongo.Rejea ufafanuzi nilioutoa ndio sahihi.Halafu elewa kuwa wewe huwezi kujua vitu vyote duniani,na lazima ukubali kukoselewa kwa sababu kufanya hivyo ni sehemu ya kujifunza,ni Mungu pekee ndiye anaejua kila kitu.
 
Hata hivi sasa siwezi wala sijuwi kufundisha mbwa. Hongera wewe unaeweza kufundisha mbwa, "birds of a flock...".

Umekazana "neno jini", Jinni ni jina la kiumbe kama vile Binadam. Kumbuka hilo.

Vipi, nikuletee mbwa wangu unifundishie?
 
Wewe ungekuwa mwalimu hufai hata kufundisha mbwa.Mimi si mwalimu wa kiswahili lakini mtu yeyote aliesoma kiswahili vizuri hawezi kukubaliana na utumbo wako kuhusu hilo tu dogo neno jini.Wewe andika kama unavyotaka lakini kama ungekuwa mtihani lazima hapa ungekula mweleka.Kwenye mada ya TEZI DUME pia uliemtumia kueleza nae amechapia kwa kudanganya wasomaji kueleza vitu vya uongo.Rejea ufafanuzi nilioutoa ndio sahihi.Halafu elewa kuwa wewe huwezi kujua vitu vyote duniani,na lazima ukubali kukoselewa kwa sababu kufanya hivyo ni sehemu ya kujifunza,ni Mungu pekee ndiye anaejua kila kitu.
Halafu wewe umeathirika mno na mfumo wa elimu ya Kiarabu ambao hauna tija katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia,na ndiyo maana Mwarabu anamtegemea Mzungu kwa kila hitaji katika maisha yake yote.
 
Hata hvi sasa siwezi wala sijuwi kufundisha mbwa. Hongera wewe unaeweza kufundisha mbwa, "birds of a flock...".

Umekazana "neno jini", Jinni ni jina la kiumbe kama vile Binadam. Kumbuka hilo.

Vipi, nikuletee mbwa wangu unifundishie?
Nioneshe kwanza hayo majini(siiti majinni)yanapatikana wapi ili tuweze ku-visualise physically yakoje.Hayo ni mambo yakufikirika hakuna binadamu yeyote anaeweza kumwona jini.Wale wote wanaodhaniwa wana majini ukweli wa mambo huwa wamepata mental breakdown.
 
Daulat Islamiya, usiangalie eti tangu hujazaliwa hujaona hiyo sio pointing kabisa , angalia historian ya uislam tangu zama za Mtume swalalahu alayh wassalaam , pia lazima utambue kwamba sio kila anayejiita muislam basi yupo ktk njia sahihi wakati fikra Na mienendo ya kiislamu haifuati Na lazima ujiulize ni kwann Siku ya hukumu waislam watakuwa wamegawanyika ktk makundi 73 km sijakosea Na kati ya hayo moja tu ndio kitakalo salimika , je unafikiri ni kundi gani? Ukirudi ktk Quran Na hadithi za mtume bila shaka utakuwa ndio nusra ya muislamu Siku hiyo Na je ndani ya Quran Na Sunna kuna sehemu utawala wa kidemokrasia umehalalishwa? Bila shaka hakuna hivyo demokrasia ni haramu Na Allah kaahid kabla ya kiama kusimama dola ya kiislamu itakuja kusimama tena
Hili ni tatizo la kujua machache ukafikili unajua mengi.Ni janga kwa wengi.Unaongelea vitu vingi na vikubwa vinavyohitaji uelewe mpana wa kiislamu.
Katika nchi ambazo si za kiislamu,Uislamu unaangalia utawala wa haki,kama kuna haki na watu wanaruhusiwa kuabudu dini inavyosema,waite demokrasia,ubepari,ujima nk dini haikupinga hili. Kuna nchi nyingi za ulaya na marekani zina sheria nyingi ambazo zimetajwa kwenye dini kuliko nchi zinazijiita za kiislamu; mfano haki za binaadamu.tafuta somo/kitabu cha 'makasida sharia' utaelewa zaid haya masuala,pia kuna mwanazuoni wa ki egypt kwa sasa yupo Canada anaitwa JASSER AUDA huyu ni msomi aliekubuhu na ni mwalimu wa sharia mfuatilie utajifunza mengi.
Salaam
 
Tyupa
Vipi juu hapo, unaongea mwenyewe unajijibu mwenyewe, umechanganyikiwa?

Makubwa!
Siwezi kuchanganyikiwa na vitu vyepesi kama hivi ila nina mashaka na wewe unaejidai kulingana na Mungu kwa kujua kila kitu wakati ni mwepesi sana.
 
Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:

Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Kwa maelezo hayo kutoka kwenye Qur'an huoni kama yana halalisha mauaji ?
 
Back
Top Bottom