Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Ibrahim Kauli,na wewe acha kupotosha watu kuhusu utamkwaji na uandishi sahihi wa neno MAJINI.Kwa mujibu wa kanuni za sarufi maumbo na matamshi neno MAJINI linatakiwa liandikwe kama hivi nilivyoandika bila double N,yaani ni makosa kuandika MAJINNI kwa kutofautisha maji na mapepo.Sarufi matamshi na maumbo kwa kutumia KIIMBO neno moja linaweza kuleta maana nyingi kutokana na kupanda na shuka kwa kutamaka baadhi ya silabi.Km Barabara ukitamka bila kupanda utakuwa una maana ni njia ya magari,eg ajali nyingi zinatokea kwa sababu barabara ni mbovu,na ukitamka kwa kupanda na kushuka utakuwa na maana ya sawa sawa e.g. umempiga barabara yaani umempiga sawa sawa.Vivyo hivyo MAJINI ukitamka bila kupanda utakuwa una maanisha maji ya kuoga au kunywa,lakini ukitumia KIIMBO yaani utamke kwa kupanda na kushuka utamaanisha mapepo.Kwa hiyo kwenye Kiswahili fasaha hakuna neno Majinni.

Umejifundisha Kiswahili shuleni, nimezaliwa na Waswahili, Kiswahili ni lugha mama kwangu na Jinni, si neno ni jina (noun).
 
1. Refer to post #11
2. Pwani na Dar akiwa Tanzania.
3. Ni mwanamke, haoleki na hajaolewa bali ameoana na mumewe kwa miaka takriban 38 sasa, AlhamduliLlah.
4. Hatawaliki wala hatawali ni "mutual consent" baina yake na mshirika wa maisha yao "shirkatil hayaa".
5. Ameonelea sadaka mojawapo ni kugawa ayajuayo na amejikita zaidi kwenye hilo kwa sasa.
6. Bado ni mwanafunzi kwa ilm zote na anajifunza kila kukicha.

Ahsante kwa mengine yote.
Asante ff kwa kunijibu
 
Nadhani unachokifanya hapa hujibu hoja bali unatoa vihoja ili thredi ifikishe pg elfu 10.

Nnaona umeshindwa kunukuu uongo ulionizulia sasa unakuja kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Na wewe roho inakuuma kwa mimi kujaza page? Kama unaweza panda juu nenda ukazibe.
 
Kwanza kabisa hongera sana FaizaFoxy wewe ni mmoja ya member wa JF ninaowakubali sana kwa kujenga hoja na uvumilivu hapa JF,nakumbuka huko nyuma ulipigwa ban tukakuombea kwa Mod wakufungulie,Maswali yangu

1.Unafikiri vyama vya siasa vya upinzani vinakosea wapi ili kuiondoa CCM ?

2.Tanzania ni maskini licha ya rasilimali nyingi tulizonazo na wanasiasa wanatudanganya kila wakati wa uchaguzi,kwa mtazamo wako ni mambo gani tunapaswa kuyapa kipaumbele ili tuweze kusonga mbele ?

3.Umekuwa mmoja ya watu ambao mnalalamika sana waislamu wananyimwa fursa kwenye teuzi mbalimbali za serikali,huoni kama chanzo cha tatizo ni kwamba waislamu hawajaweka kipaumbele kwenye elimu dunia na pia wamekuwa hawana umoja kama walivyo wakristu ?

FaizaFoxy ,nasubiri majibu
 
Ibrahim Kauli,na wewe acha kupotosha watu kuhusu utamkwaji na uandishi sahihi wa neno MAJINI.Kwa mujibu wa kanuni za sarufi maumbo na matamshi neno MAJINI linatakiwa liandikwe kama hivi nilivyoandika bila double N,yaani ni makosa kuandika MAJINNI kwa kutofautisha maji na mapepo.Sarufi matamshi na maumbo kwa kutumia KIIMBO neno moja linaweza kuleta maana nyingi kutokana na kupanda na shuka kwa kutamaka baadhi ya silabi.Km Barabara ukitamka bila kupanda utakuwa una maana ni njia ya magari,eg ajali nyingi zinatokea kwa sababu barabara ni mbovu,na ukitamka kwa kupanda na kushuka utakuwa na maana ya sawa sawa e.g. umempiga barabara yaani umempiga sawa sawa.Vivyo hivyo MAJINI ukitamka bila kupanda utakuwa una maanisha maji ya kuoga au kunywa,lakini ukitumia KIIMBO yaani utamke kwa kupanda na kushuka utamaanisha mapepo.Kwa hiyo kwenye Kiswahili fasaha hakuna neno Majinni.
sawa mkuu nimekuelewa ila umeelewa maana ya post yangu
 
Umejifundisha Kiswahili shuleni, nimezaliwa na Waswahili, Kiswahili ni lugha mama kwangu na Jinni, si neno ni jina (noun).
Kwa hiyo noun si neno?Tafadhali rejea kamusi ya Kiswahili utapata usahihi wa neno husika.Pia kuzaliwa na Waswahili sio kigezo cha kujua kanuni za matumizi sahihi ya Kiswahili.Ingekuwa hivyo Wazaramo wote shuleni wangekuwa mabingwa wa lugha ya Kiswahili.
 
1. Naam, nnasoma sana tena sana, mpaka imekuwa tabia kuwa sipati usingizi mpaka nijisomee, na ni hivyo kwa miaka mingi sana sasa.

2. Kusema kweli katika vitabu vyote nilivyosoma hakuna kinachonishangaza na kushindwa kuchoka kukisoma kama Qur'an. Ni kitabu cha ajabu sana ambacho sijawahi kuchoka kukisoma na kila nikisoma nnakutana na ufumbuzi mpya.

Besides Qur'an. nnasoma kila aina ya vitabu, hususan vya "non fiction", kimoja ambacho nnaweza ku ki recommend ni cha "how to", kinaitwa How to win friends and influential people cha Dale Carnegie. Kingine ni cha history kinachoitwa Empires of The Monsoon cha Richard Seymour Hall, vitabu vingine nilivyotokea kuvipenda na ningependa vijana wavisome ni The Perfumed Garden cha Sheikh Nefzawi kilichotafsiriwa na Sir Richard Burton , bila kusahau Alf Lela u Lela au Arabian Nights: One Thousand and One Nights kilichotafsiriwa pia na Sir Richard Burton.

3. Vijana nnawaasa wajiwekee hata saa moja kwa siku ya kujisomea, besides, kusoma kutawapa uelewa mpana sana tena sana. Wawachane na kusoma udaku, unawaharibia mawazo mapana.
The Perfumed Garden ... NImekisoma hicho kitabu kitambo, kwa kwlei ni kizuri na kinafunda haswa.

Kaka ...
 
FaizaFoxy namn gani naweza kuwekeza katika dhahabu ?? kwa ajiri ya wakati ujao

Njia nzuri na salama ni kwenda kununuwa moja kwa moja kwa masonara ambayo itakuwa ni ghali kiasi lakini ni akiba. Wanawake wengi sana hupendelea kununuwa kwa masonara vyombo vya dhahabu kwani huwa wanavitumia kwa kuvivaa na huwa ni akiba pia. Hivyo ndiyo walivyofanya wazee wetu.

Kwa siku hizi ukitaka kununuwa dhahabu ya kutosha basi unaruka kwenda Dubai, sheria za huko hautakuta sonara wa kudanganya-danganya na soko la dhahabu ni kubwa sana kuna ushindani wa hali ya juu.

Huko utakuta kuna vipande (vinoo) kabisa vya dhahabu vya kila saizi vinauzwa, na wengi hununuwa kujiwekea akiba.

Hapa kwetu Tanzania unaweza kuchukuwa kibali rasmi cha kununuwa dhahabu na ukaenda sehemu zinazozalisha dhahabu kama Chunya ukajinunulia wanavyoita "vikole", ukija mjini ukimpata sonara unaemuamini anakuyeyushia na kukuwekea vinoo. Hii ndiyo njia ya kununua kwa urahisi kama hutaki kuitumia mwenyewe kwa kujipamba.
 
Kwa hiyo noun si neno?Tafadhali rejea kamusi ya Kiswahili utapata usahihi wa neno husika.Pia kuzaliwa na Waswahili sio kigezo cha kujua kanuni za matumizi sahihi ya Kiswahili.Ingekuwa hivyo Wazaramo wote shuleni wangekuwa mabingwa wa lugha ya Kiswahili.

Hapana, usichanganye mada. Wazaramo wana lugha mama yao, nacho ni Kizaramo.

Jinni ni jina linalotokana na lugha ya Kiarabu, kumbuka hilo. Kwa hiyo kubadili jina ni ujinga tu. Kamusi ya Kiswahili imeandikwa na watu kama mimi na wewe na kama wameandika "jini" basi sina budi kusema uelewa wao kwa jina hilo ulikuwa ni finyu kama wako.

Jina si neno, neno linaweza kuwa jina pia na jina linaweza kuwa neno pia. Lakini Jinni kwa maana halisi inavyotumika hapa ni jina.
 
Back
Top Bottom