Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwahiyo huamini hizo aya ama?

Usiwe na wasi wasi, ondoa hofu. Hizo utajibiwa amma na mimi amma na mchangiaji mwengine yeyote, hii ni open forum. Nilichokuomba mimi ni link ya source ya uliyobandika hapa.

Kama unayolink na source nnakuomba iweke tu hapa itusaidie wengi la kama hauna au link na source ni wewe mwenyewe, sema tu hilo, wala lisiwe mtihani mkubwa kwako.
 
Mimi nime download Quran iliyotafsiriwa na sheikh barwan. Naipenda kwasababu imeweka na lugha ya asili pia imejitahidi Sana kutafsiri neno kwa neno.
 
Kajirutaluka heshima kwako, nipo ndani ya swala kabla imam kutoa salam, ushuzi ukanibana, naweza toa salam kabla imam ili swala ikamilike , maana nikimsubiri imam sitofika, mkuu unapojibu jaribu ku- quote kwa kutumia swali
Hauruhusiwi kumkhalifu imam unatakiwa umfuate mpaka mwisho wa sala. Hivyo kama umebanwa ujikaze mpaka swala ifike mwisho ukishindwa basi jiechie tu halafu urudie kuswali
 
Ninataka kujifunza kiarabu fasaha mtandaoni. Je kuna tovuti yoyote unaifahamu FaizaFoxy ?
Sijajuwa kiwango chako lakini unaweza kuanziaa website hii
Madinah Arabic Learn Arabic For Free

Na hapa utapata jumla ya cd 48 zenye video ambapo jamaa anafundisha a complete course ya arabic kama inavyofundishwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao wanategemea kufanya mafunzo yao kwa lugha ya kiarabu katika madina university. It is an excellent job
[DVD: Madinah Arabic]

I hope itakusaidia
 
Mimi nime download Quran iliyotafsiriwa na sheikh barwan. Naipenda kwasababu imeweka na lugha ya asili pia imejitahidi Sana kutafsiri neno kwa neno.
Nakushauri utumie tafsiri ambayo ipo katika mtandao wa alhidaaya ndio ambayo imekamilika kila kona. Hii ya Baruwan ina makosa ya kiufundi.
 
Mimi nime download Quran iliyotafsiriwa na sheikh barwan. Naipenda kwasababu imeweka na lugha ya asili pia imejitahidi Sana kutafsiri neno kwa neno.

Well, sidhani umezitoa kwenye tovuti ya Baruani kwa sababu fonts za Kiarabu ulizobandika hapa ni tofauti na zilizopo huko.

Anyway, nadhani siyo issue. Na ni matumaini yangu kuwa utapata majibu ya maswali yako baada ya muda mfupi.
 
Hapana udhu huatenguki kwa kubwanwa na haja au upepo kuwa makini. Kwa mujibu wa fiqhi ya kishafi mtu anaweza kuswali hata kama amebanwa na mkojo lakini ni makuruhu
 
Well, sidhani umezitoa kwenye tovuti ya Baruani kwa sababu fonts za Kiarabu ulizobandika hapa ni tofauti na zilizopo huko.

Anyway, nadhani siyo issue. Na ni matumaini yangu kuwa utapata majibu ya maswali yako baada ya muda mfupi.
Siwezi kudanganya tafadhali
 
Siwezi kudanganya tafadhali


Sijakuambia umedanganya, nimesema " sidhani kama umezitoa kwenye tovuti ya Baruani" (Barwani), tovuti ya Barwani (Qur'ani Tukufu) Fonts zake ni hizi:



KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

Si unaona tofauti?

Source: 112. SURAT AL-IKHLAS'

Labda umetoa kwenye tovuti nyingine.

Na nimesema, si kitu, In sha Allah utapatiwa majibu kutokana na maswali yako.
 
Aya hiyo tunaziamini kama tunavyoamini aya zingine. Na khabari ilotolewa hapo ni kweli na haki. Ufafanuzi wake ni kuwa wale ambao wataamini miongoni mwa mayahudi na manaswara yale ambayo wanayopaswa kuamini ikiwemo kuamini Allaah na kuamini mitume wake akiwemo Muhammad na wakafanya vitendo vizuri na wala wasibadilike mpaka wakafa basi hawatakuwa na khofu. Lakini hapo hawaingii wale waliompinga muhammad kwani wao aya inayowahusu ni suwrat al bayyinah aya ya 6 inasema "Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu kabisa wa viumbe"
 
Download hii
Quran -swahili
4.5
Utaona.na hii ndio naitumia mimi
 
( الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ )

الحج (40) Al-Hajj

Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.

Quran inatamka majengo manne ya ibada
Msikiti
Kanisa
Sinagogi
Hekalu
Na inasema jina la Mungu hutamkwa kwa wingi humo.
Swali je aya hii unaiamini?
Mungu gani anatamkwa kwa wingi hekaluni, kwenye sinagogi na kanisa?
Je Kwasasa kulingana na uelewa wako wa usomi unaamini kwamba jina la Mungu bado linatajwa kwa wingi katika majengo hayo ya ibada? Kama la kwanini na unavigezo gani?
Je unaamini kwamba Allah siku ya kiama watu kama wakristo, wayahudi hawatauridhi ufalme wake mpaka wawe waislamu?.
Sitaki matusi na naomba kama huwezi maswali nyamaza nami nitajua nalo ni jibu.
 
Reactions: dtj
Makosa yapi ya kiufundi. Je wameondoa maneno ya asili?
Hebu ndugu kuwa wazi khasa kipi unakusudia. Kwani kwa muislamu analazimika kuzikubali na kuziamini aya zote za Qur-aan kuwa ni haki itokayo kwa Allah.

Haifai kuitenga aya yeyote kwa kujua tafsiri yake,sababu au hikma ya kushuka kwake au kutokujua.

Hebu weka wazi nini unakikusudia huenda ikawa rahisi kupata jibu unalolihitaji
 
Hujajibu maswali
 
Hapa hampagusi kulikoni
 
Reactions: dtj
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…