( الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ )
الحج (40) Al-Hajj
Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.
Quran inatamka majengo manne ya ibada
Msikiti
Kanisa
Sinagogi
Hekalu
Na inasema jina la Mungu hutamkwa kwa wingi humo.
Swali je aya hii unaiamini?
Mungu gani anatamkwa kwa wingi hekaluni, kwenye sinagogi na kanisa?
Je Kwasasa kulingana na uelewa wako wa usomi unaamini kwamba jina la Mungu bado linatajwa kwa wingi katika majengo hayo ya ibada? Kama la kwanini na unavigezo gani?
Je unaamini kwamba Allah siku ya kiama watu kama wakristo, wayahudi hawatauridhi ufalme wake mpaka wawe waislamu?.
Sitaki matusi na naomba kama huwezi maswali nyamaza nami nitajua nalo ni jibu.