Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

FaizaFoxy kwa nini wapenda kuumbua watu haswa wanapokosea kiswahili?

unaffikiri ni kwa nini wanajamii forum wanapenda kukushambulia haswa kwenye swala la udini?

kwa nini wewe ni mkali?una stress?how old are you?


Kuhusu swali lako la kwanza, pitia hapa: Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kuhusu swali lako la pili, sijayaona hayo mashambulizi, mimi huona mijadala inakuwa mikali kwa sababu nnayowaeleza yanawaingia. Na huwa hawataki kuusikia huo ukweli wana "panic". Ukweli unauma.

Mimi si mkali. Waulize wana JF wa siku nyingi wananielewa.

Sina stress.

Hilo swali lako la mwisho, pitia hapa: Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa
 
1. Kuna ubaya gani watu kujua umri wako?
2. Idadi ya watoto ulionao?
 
Kasome post namba 43.

Licha ya hiyo, kuna kozi nyingi sana na seminar nyingi sana za taaluma mbali mbali nimepitia sehemu nyingi duniani. Lakini katika yote hayo hakuna taaluma niliyoipata zaidi na iliyonifunguwa ubongo na macho kama Qur'an, kusafiri na kujisomea mwenyewe kila nnapopata nafasi.
Hujasoma Bible neno la uzima
 
nmeona niulize hili



ukifungua account ya dolla au pound nikawa naweka dola 100 kila mwezi kwa muda wa miaka mitano je unaamini dola itashuka au shilingi itapanda thamani?


Nnakushauri, wekeza kwenye shillingi. Shillingi itapanda thamani. Na Allah ndiye ajuae zaidi.

Lakini ni vizuri zaidi ukiwekeza kwenye dhahabu.
 
Yaani hapa jf kwa huyo faiza hata tualikane members wote majukwaa yote tuanze kubishana nae wote mtaomba poo, Kwanza nachompenda faiza haongei bila ushahidi, Kila kitu atakupa kwa ushahidi labda ulete ubishi wako tu, huyu ni mmoja wa member wachache sana nnao wakubali hapa
 
This thread is full of * especially from foxy herself.

1. Ufaulu Mzuri ni kuwa mwislam

2. Mwanaume akiwahi kufika kileleni basi anazaliwa mwanaume, akiwahi mwanamke anazaliwa mtoto wa kike

3. Waislamu wanafelishwa na NECTA.
 
Faiza, hujajibu swali langu, nimeuliza hivi 'who are the real children of Israel?'' labda nizungumze ninachohitaqji, kuna uvumi kwamba waisrael wa leo sio wale waliotajwa kwenye vitabu vitakatifu na kwamba waliopo wamepachikwa na marekani kulinda interests zake pale middle east, sasa wenyewe ni wepi. Nadhani sasa utanijibu
 
Mara kwa mara tumekuwa na kusikia neno JIHAD likihusishwa na kuwafanyia mambo ya kikatili dhidi ya binadamu wenye imani tofauti na imani ya Kiislam..

Naomba kujuzwa yafuatayo kulihusu neno JIHADI:-

1. Maana ya neno JIHAD, asili na malengo yake ni ipi.?

2. Je, JIHAD ina faida / hasara, kama ina faida ni zipi na kama hasara ni zipi?

3. Ni watu wa aina gani wanapaswa kutekeleza JIHAD au ni kwa mtu yeyote yule?

4. Nitaitofautisha vipi JIHAD na Ugaidi?

Mwisho; Lengo kuu la JIHAD ni lipi katika huu ulimwengu?

1- Jihad ni kujitahidi. Juhudi. Kwa Muislam anatakiwa ajitahidi katika kila jambo alifanyalo. Iwe kusoma, kufanya kazi, kufanya biashara, kulingania mema na kukataza mabaya. Kwa kifupi, kila tulifanyalo tuwe tunajitahidi sana kulifanya katika njia zilizo bora na tulizowekewa wazi na Allah.

2. Jihad kwa maana hiyo kwenye namba moja, ina faida kubwa sana.

3. Kwa mtu yeyote yule ni lazima awe na jitihada kama ilivyo kwenye namba moja hapo juu.

4. Jihad ni kujitahidi, ugaidi ni "terror" kutisha watu (nielewavyo mimi).

Lengo kuu la Jihad ni kuwa na maisha bora kama uonavyo kwenye namba moja.
 
Faiza, hujajibu swali langu, nimeuliza hivi 'who are the real children of Israel?'' labda nizungumze ninachohitaqji, kuna uvumi kwamba waisrael wa leo sio wale waliotajwa kwenye vitabu vitakatifu na kwamba waliopo wamepachikwa na marekani kulinda interests zake pale middle east, sasa wenyewe ni wepi. Nadhani sasa utanijibu
Unaona sasa....!! Hapa umeuliza vizuri kabisa lakini kwa ule uulizaji wako wa awali; hapakuwa na namna nyingine zaidi ya kukupa maandiko!!!!!
 
Lile jibu langu vipi?
Sina ubia na FF katika huu uzi lakini next time unapouliza kama ulivyofanya hapa; unatakiwa ku-quote hilo swali ambalo uliuliza manake kwa jinsi ulivyouliza; unatarajia jibu gani zaidi ya "jibu la swali lipi?!" Manake sioni ni namna gani ataanza kurudi nyuma kutafuta hilo swali!!!
 
Mi napenda ulivyojibainisha na unavyoweza kuhimili kejeli za mtandaoni. Nashukuru kwa fursa hii.

What does motivate you?

Huko nje ya jf wewe ni mwanamke wa aina gani?
Niko nasoma kitabu cha kiswahili ambacho kina maneno magumu, nikikutumia pm kukuuliza maana ya maneno utanijibu?
 
Back
Top Bottom