Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Maneno yepi? hebu ya "quote" kwa "context" yake.
"aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuawa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote"
 
FaizaFoxy, jibu posts 56 na 244, hii ni mara ya pili kukuomba ujibu. Ubarikiwe Kaka
 
Sasa wewe unajibu kama nani yake? Na aisee nimemuuliza yeye na hii Elimu ya faiza umeijulia wapi wacha kutafuta Kiki....
Namjua mwanzo mwisho huyo mama, hana degree labda ya open, ni mtu amezaliwa kijijini mwetu, usitake niseme mengi bwana
 
Nina Tatizo la Uti wa mgongo,tatizo hilo ni Pingiri za uti wa mgongo ile ya chini kukauka ule uroto wake au tunaita Ute Ute wa kwenye joint zake"!
Nilipima kwenye MRI pale Muhimbili na dawa hawana nilipewa za kupunguza maumivu tu nazo hazikusaidia chochote lkn pia nilienda Hosp za Regency,Tumaini.Apollo,Saint Benard lkn kote ni vile vile na nikawakuta Madaktari wale wale sasa natafuta tiba za asili nimeambiwa zinaponyesha sbb mimi sijavunjika!
Mwenye kujuwa Wataalam wa Asili wa hili tatizo anisaidie haraka maana napata maumivu ya Mwili muda wote!
 
Kasome post namba 43.

Licha ya hiyo, kuna kozi nyingi sana na seminars nyingi sana za taaluma mbali mbali nimepitia sehemu nyingi duniani. Lakini katika yote hayo hakuna taaluma niliyoipata zaidi na iliyonifunguwa ubongo na macho kama Qur'an, kusafiri na kujisomea mwenyewe kila nnapopata nafasi.
[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Wanaopigana vita na vurugu ni Waislamu "ZAIDI".Note a comparative form must be related with another article.Kwa hiyo nchi nilizozitaja ni lazima ni linganisha na nchi zingine zote duniani.Ni ukweli usiopingika kuwa mahali popote walipo Waislamu vita na vurugu ndio mahali pake.Eleza sababu kwa nini Waislamu hawapendi amani kama ambavyo dini yao ina-justify.Wewe ndio utakuwa ulienda kusomea ujinga.
 
Faiza, kwa kuwa umeishi kwenye nchi nyingi zilizoendelea na umebahatika kupata elimu nzuri na mafanikio. Unatoa ushauri gani kwa vijana wa Tanzania kuhusu fursa zinazopatikana nje ya mipaka ya Tanzania?

Umesema kwa sasa unafanya shughuli ya ufugaji na miongoni mwa hiyo mifugo ni samaki, je, unafuga samaki kwa ajili ya biashara, kitoweo? Kama ni biashara soko lake lipoje maana nataka kuanza huu ufugaji baada ya kuufanyia utafiti wa kina.

Kweli nje kuna fursa nyingi sana lakini, nnawashauri vijana wa Kitanzania kabla ya kukurupuka kwenda nje wasome kwa bidii sana, amma wasomee fani yoyote (vocational training) amma wasome elimu ya juu na ikiwa watatoka kwenda nje basi watoke amma kwa kufata elimu ya ziada amma kwa kufanya kazi ambazo tayari wanazijuwa na wamezitafuta kuanzia huku, yaani anakwenda nje kifuwa mbele na ana ujuzi wake na wasikurupuke.

Nchi zingine zinatowa kabisa mafunzo kwa vijana wao wanaotaka kwenda nje kutafuta maisha, nadhani na Tanzania wangefanya mikakati hiyo ili iwasaidie vijana wanaotaka "kuzamia".

Mfano Canada, hata ukiingia kwenye website ya "immigration" yao utakuta wameweka kabisa watu wanaowahitaji na kama unakidhi vigezo basi huna tatizo kabisa. Una apply na kuondoka kiulaini kabisa, nnawashauri pitieni kwenye tovuti ya ubalozi wa Canada.

In sha Allah, moja katika mikakati ninayofikiria kuianzisha Tanzania ni hilo la kuwawezesha vijana kwenda Canada kihalali na kisheria. Tatizo mimi siwezi kufanya kazi hizo kwa muda mrefu kwa sasa na nitahitaji watu wa kufanya hizo kazi na mimi ntawasimamia kwa "remote".

Kuhusu kufuga, nilianza kufuga kama kitoweo tu, maana nnaishi shamba muda mrefu nikiwa Tanzania, lakini mifugo inazaliana na kujijenga yenyewe kuwa "commercial" kwa kuwa imefikia nnazalisha zaidi kidogo ya matumizi yangu.

Ufugaji wa samaki ni mzuri sana, mimi nilianza kama mchezo mchezo tu lakini sasa nnawauza na wana demand sana. (quantities zangu si kubwa). Nnauhakika samaki wana soko zuri tu kwani watu wanakuja kuchukuwa kwangu Mkuranga kilo shillingi 7,000 na mara nyingi huwa sina wa kuwapa. Na wananishauri niweke kambare watachukuwa kwa 8,000 lakini bado sijaanza kuwaweka.

Nnakushauri anza tu, work hard na "mambo yatajipa".
 
Naomba urafiki wa kalamu ila mimi kafir siyo mwislam utanikubali?

Dah! umenikumbusha zamani sana "urafiki wa kalamu" na "kutafuta mchumba" kupitia magazeti.

Ngoja nikupe kisa kimoja kuhusu kutafuta mchumba:

Mume wangu kuna siku alifanya utani kwa rafiki yake, akachukuwa picha yake akaituma kwenye magazeti Tanzania kuwa huyo rafiki yake anatafuta mchumba, na kina dada walivyoona mtu yuko nje, baada ya wiki mbili yule jamaa alipata barua zaidi ya 2,000 kwa wakati mmoja. Ilikuwa ni vichekesho, yeye mwenyewe hajatuma kutafuta mchumba na hajuwi nini kinaendelea mwishowe ikabidi akubali matokeo tu, akaanza kuwa analeta barua tuzisome na tujibu.

It was fun.

Siku hizi mambo yote ni hapa hapa JF, huu ni zaidi ya urafiki wa kalamu, kama hivi tunaulizana, tunafundishana, tunapapurana. Yote kheri hii.

Karibu sana.
 
Wanaopigana vita na vurugu ni Waislamu "ZAIDI".Note a comparative form must be related with another article.Kwa hiyo nchi nilizozitaja ni lazima ni linganisha na nchi zingine zote duniani.Ni ukweli usiopingika kuwa mahali popote walipo Waislamu vita na vurugu ndio mahali pake.Eleza sababu kwa nini Waislamu hawapendi amani kama ambavyo dini yao ina-justify.Wewe ndio utakuwa ulienda kusomea ujinga.

Waislam kwa sasa hivi wapo dunia nzima, kama kuna sehemu hakuna Waislam basi nnahisi hata Wakristo watakuwa hawapo.

Jee, katika muono wako huoni hiyo ikawa ni "divide and rule"?

Nime google "What wars are going on right now?" na jibu nililopata ndiyo hili:

Rwanda, Somalia, Angola, Sudan, Liberia, and Burundi are among those countries that have recently suffered serious armed conflict. War has caused untold economic and social damage to the countries of Africa. Food production is impossible in conflict areas, and famine often results.

Unaonaje?

Source: Bofya hapa

Hauna maswali mengine ya "general knowledge" zaidi ya haya ya dini? Maana kuna watu wengine yanawapa mushkel, na ni vyema tukawapa fursa kwa maswali mengine, au unaonaje?
 
Back
Top Bottom