Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Ahsante kwa sifa njema ulizonipa na ahsante kwa maswali yako mazuri.

Maswali kama haya ndiyo tunayataka humu si wengine wanakuja na mizaha na kebehi na kejeli zisizoweza kutulea tija yoyote.

1) Suala la ulezi ni pana sana na tunaweza tukalijadili kwa marefu na mapana na tusifikie mwisho.

Nnawaomba wachangiaji wengine wote kwenye huu mjadala wa ulezi tujikite na tutoe maoni na mawazo yetu kwa kadri ya muono wetu ambayo nnatumai yatatusaidia sote na vizazi vyetu.

Hapo zamani kidogo wakati mimi nnakuwa mitaa ya Kariakoo kuna kitu nnakikumbuka ambacho sasa sikioni, sijuwi hilo lilikuwa suluhisho la malezi au la. Ni hivi; Kila mtu mzima, awe mzazi wako asiwe mzazi wako alikuwa ni mlezi na muangalizi wako ukipenda usipende, ilifikia hata unaweza kuchapwa kwa kuonekana unafanya utovu wa adabu mtaani na mtu usiyemjuwa.

Kuna siku nnakumbuka, mdogo wangu aliletwa nyumbani huku kakamatwaa mikono asikimbie, kesi yenyewe ilikuwa ni kakamatwa na huyo kijana mitaa ya upanga (enzi hizo upanga bado kuna kimsitu kidogo) na alikamatwa kwa kuwa ana winda ndege na manati na ulikuwa ni wakati wa shule na alikuwa amevaa uniform za shule. Yule kijana aliyemkamata hakupendezwa na hilo na akamshika akamwambia sikuachi mpaka twende kwenu, kufika nae nyumbani akaanza kuelezea kwanini kamleta vile, basi mama'ngu (Allah amrehemu) akamwambi yule kijana subiri, akaingia akatoa mkwaju akmwambia mchape hapa hapa atie adabu. Naam, akachapwa.

Nnakuelezzea hicho kwa uchache ili kuonesha jamii ilivyokuwa zamani, kila mmoja alikuwa na wajib wa kuhakikisha watoto wanakuwa wema. Leo hii yapo hayo?

Tutarudi kwenye mjadalahuu wa ulezi nimelipenda swali lako, napenda wachangiaji tuchangie kwa wingi kwenye hili.

2) Hili sina majibu ya haraka ila nnasema AlhamduliLlah.

3) Umma wa Kiislam hauna unapokosea ila nguvu nyingi zinatumika kuupiga vita Uislam directly na indirectly, hii ni duniani na hasa imelengwa zilipo jamii za Kiislam kwa wingi.

Yasome haya, kisha ufikirie:

A) Nchi zenye Waislam wengi hususan za Mashariki ya kati, utakuta ving'amuzi vinakamata channel za ngono zaidi 100 na ni bure, kilichofanywa ni kuwafanya kama mjione mna akili sana ya ku hack ving'amuzi kumbe ni njama za kuwafanya muingie kwenye mkumbo na tamaduni hasi.

b) Tazama pwani ya Afrika mashariki inavyojazwa mahoteli ya kitalii kwenye fukwe zake ambako 99% ya wakazi wake ni Waislam. Cha kushangaza 99% ya hizo hoteli ni za Wataliano. Imeanzia Malindi, Kenya inashuka hadi kujaza Zanzibar na sasa inashuka Mafia, na kuelekea kusini ya pwani yote.

Jee, ni biashara tu? Ni maswali ya kujiuliza.

Natumai kuanzia hayo inabidi tujifikirie na tuendeleze mjadala.

Nnaamini wao wanapanga lakini hakuna shaka kuwa mbora wa wapangaji ni Allah Subhana wa Taala.
JazzakaAllah khairy.asante kwa majibu yako.Allah akuhifadhi
 
Naomba kuuliza nini kifanyike ili kuboresha elimu yetu hapa tz?
 
je, ni kweli dini ya kiislamu ina mafungamano na makundi / matukio ya kigaidi?
......fa wewe !!
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Update 1: Tafadhalini tuulize maswali kiheshima . Heshima ni kitu cha bure na hii JF yetu pendwa inasomwa na wengi, tujiheshimu.
 
Bibi,mimi nina swali moja!
Ni neno lipi hapa ndiyo sahihi?:
a)hili au ili?
b)ndio au ndiyo?
c)kwa hiyo au kwahyo?
d)hilo au ilo?
e)hile au ile?
f)hovyo au ovyo?
G)hapa au apa?


Nimerudi tena nnaona hatukupata wachangiaji wa kusaidia kwenye hili. si kitu, tuliishia b).

c) kwa hiyo
d) hilo
e) ile
f) hovyo
g) hapa
 
Nilikuambia kila aaminie ataokolewa

Wewe unaleta mambo ya torati plus kuran ambayo sisi hatuwezi kuconfirm kwasababu ya lugha iliyotumiwa


Mbona zote hizo tafsiri zake zipo?


Kwa hiyo wewe huiamini hata taurati iliyopo kwenye Biblia? Au haujuwi kuwa ipo humo?
 
NINI CHANZO CHA SIMBA KUFANYA VIBAYA KATIKA MICHEZO YAKE


Watajirekebisha.

Ndiyo kawaida ya michezo, inategemea mambo mengi na natumai wataalam wa soka waliopo Simba wanalifanyia kazi.

Mume wangu ni mpenzi sana wa soka, yeye huwa anasema "mpira unachezwa zaidi nje ya uwanja kuliko zile dakika 90 za uwanjani".
 
screpa
Hujajibu swali langu kwenye post namba 66.
Je nini kifanyike ktk shule za kiislaam ili zifanyenye vizuri kama shule za kikristo?

Je una ushauri gani kwa waislaam wanaolalamika kuwa wanatengwa ktk elimu na nafasi za juu ktk uongozi?

wewe ni mwanamke wa kiislam na Allah amekujaalia umepata elimu tena ktk masomo ya science
je huwa unahamasisha bint wa kiislaam kusoma masomo ya sayansi na kuendelea na elimu ya juu ktk jamii inayokuzunguka?
 
Je nini kifanyike ktk shule za kiislaam ili zifanyenye vizuri kama shule za kikristo?

Je una ushauri gani kwa waislaam wanaolalamika kuwa wanatengwa ktk elimu na nafasi za juu ktk uongozi?

wewe ni mwanamke wa kiislam na Allah amekujaalia umepata elimu tena ktk masomo ya science
je huwa unahamasisha bint wa kiislaam kusoma masomo ya sayansi na kuendelea na elimu ya juu ktk jamii inayokuzunguka?


Mimi Tanzania nimeona shule moja tu ya Kiislam, ile ipo Chang'ombe (sijuwi inaitwaje).

Lakini kama unamaanisha shule za Waislaam, basi nadhani zipo zinazofanya vizuri sana na mojawapo ni FEZA.

Shule zisizofanya vizuri waende wakaone FEZA wanaweza vipi?

Tena mkubwa wa hiyo shule ya FEZA (sijuwi kama bado yupo FEZA au kastaafu) Ni Dr. Madati, viongozi wa shule zingine za Kiislam wangemfata huyu wachote alichonacho. Huyu mtu ni kichwa sana tena nnashangaa Waislam kwanini hawamtumii vilivyo na ilhali shule ya FEZA haina mjadala kwa wanafunzi wake kufanya vizuri.

Naam. Nnalifanya hilo la kuhamasisha watoto wa Kiislam na wasio wa Kiislam kusoma soma, soma, soma, wake kwa waume kila siku.

Wasio Waislam leo ni Waislam wa kesho na nnawahamasisha sana kwani nnaamini wasio Waislam waliosoma ni rahisi sana wao kuelewa kuwa "wanaingizwa mkenge" kuliko wasio soma au wenye elimu kidogo.
 
Japo swala langu hujanifafanulia vzr ninlo lingine tena, tuna mifugo mf. Ng'ombe ya kifamilia inakaa shmu moja yupo baba ndo kiongoz wa kaya , na ktk zizi moja kila mmoja ana ng' ombe wake (zinakaa kifamilia), je zaka yake inakuaje hpo?
 
Japo swala langu hujanifafanulia vzr ninlo lingine tena, tuna mifugo mf. Ng'ombe ya kifamilia inakaa shmu moja yupo baba ndo kiongoz wa kaya , na ktk zizi moja kila mmoja ana ng' ombe wake (zinakaa kifamilia), je zaka yake inakuaje hpo?


Swali lako lipo post namba ngapi, nilipitie tena.
 
Japo swala langu hujanifafanulia vzr ninlo lingine tena, tuna mifugo mf. Ng'ombe ya kifamilia inakaa shmu moja yupo baba ndo kiongoz wa kaya , na ktk zizi moja kila mmoja ana ng' ombe wake (zinakaa kifamilia), je zaka yake inakuaje hpo?

Somo la Zaka

PAMOJA na kuwa zaka ni miongoni mwa nguzo tano za Kiislamu, lakini pia ni kiungo muhimu kati ya tabaka la matajiri na masikini, kwani utekelezaji wa nguzo hii unaleta ufanisi katika kuziba mwanya uliojitokeza kati ya matabaka mawili haya. Somo hili litasaidia kuwaelimisha Waislamu umuhimu wa zaka na jinsi ya kutekeleza nguzo hii muhimu.

Maana ya zaka:

Neno zaka maana yake ni baraka, utakaso, ziada na wema, mambo ambayo upatikanaji kwa kukusanywa viwango maalumu vya mali kutoka kwa wenye uwezo na kupewa watu wanaohitaji. Tofauti kubwa iliyopo kati ya zaka na sadaka ni kuwa, zaka ni tendo la lazima ambapo sadaka ni tendo la hiari (hisani).

Hukumu ya kutoa zaka:

Kutoa zaka ni jambo la lazima kwa Muislamu mwenye uwezo uliotajwa na sheria ya Kiislamu, Muislamu huyo akiacha kutoa zaka huwa ni mkosa anayestahili kuadhibiwa mbele ya Mungu.

Mali ipasayo kutolewa zaka:

Kitu chochote kile kinachomilikiwa na kutumika kwa maslahi ya binadamu ni mali ipasayo kutolewa zaka, hata hivyo, kuna mambo maalum yanayozingatiwa katika mali hiyo kama vile uzalishaji, kufikia lengo maalum na kupitiwa na muda wa mwaka.

Aina za zaka:

Kuna aina nyingi za zaka, zifuatazo ni baadhi ya aina hizo:

Zaka ya Akiba, mali yoyote iliyowekwa kama akiba mahali popote pale kwa lengo la kuihifadhi hutolewa zaka. Utaratibu wa zaka hii huwa kama ifuatavyo:

Iwe na thamani isiyopungua thamani ya gramu 85 za dhahabu safi (525,000/= Tsh).

Kinachotolewa ni asilimia 2.5 ya mali yote.

Iwe ina umri wa mwaka mmoja tokea imewekwa au kutolewa zaka.

Zaka ya mifugo - Muislamu anayemiliki ng’ombe 30 anapaswa kutoa ng’ombe mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja, na yule anayemiliki ng’ombe 40 atoe ng’ombe mwenye umri wa miaka miwili, utaratibu huu utumike katika kila kundi la ng’ombe 30 na ng’ombe 40, pia inaruhusika kutoa thamani ya ng’ombe waliotajwa. Kuhusu mbuzi na kondoo atatoa katika kila mbuzi au kondoo 100 mnyama mmoja anayehusika au thamani yake. Jambo muhimu ni kuzingatia muda wa mwaka moja tokea kunzishwa kwa ufugaji au kutolewa kwa zaka.

Zaka ya mavuno - Kila kinachovunwa kutoka ardhini au baharini kinapaswa kutolewa zaka mradi tu mavuno hayo yana uzito usiopungua kilo 653 (gunia sita na nusu), kinachotolewa ni kilo 65.3 iwapo kilimo hakikutegemea gharama za kitaalamu, vinginevyo mkulima atapaswa kutoa kilo 33 tu kwa kila kilo 653 anazozivuna.

Zaka ya biashara - Mali yoyote iliyotengezwa kwa ajili ya uzalishaji inapaswa kutolewa zaka mradi tu ina thamani isiyopungua shilingi 525,000 za Kitanzania. Kinachotolewa ni asilimia 20% (1/5) ya faida iliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja.

Zaka ya machimbo - Kila kinachochimbwa ardhini au kukusanywa kutoka baharini miongoni mwa madini kinapaswa kutolewa zaka, kinachotolewa ni asilimia 20% ya thamani ya madini yaliyochimbwa au kukusanywa.

Wanaostahiki kupewa zaka:

Qur’an tukufu imetaja jamii nane za watu wanaostahiki kupewa zaka, nao ni hawa wafuatao:

Mafukara: Hawa ni watu ambao hawamudu kupata mahitaji yao ya lazima kila siku.

Masikini: Hawa ni watu ambao hawamudu kupata mahitaji yao ya lazima kwa uhakika.

Wenye madeni: Mtu au kikundi cha watu wenye madeni wanastahiki kupewa sehemu ya zaka ili waweze kulipa madeni yao.

Watumishi wa zaka: Watu wanaotumika kukusanya na kusambaza zaka wapewe sehemu ya zaka hiyo kwa lengo la kuwafanya wasiwe na tamaa dhidi ya mali wanayoifanyia kazi.

Harakati za ukombozi: Mtu au kikundi cha watu kinachotaka kujikomboa kutoka utumwani au kutawaliwa kimabavu wanastahiki kupewa sehemu ya zaka ili kufanikisha lengo lao.

Wanaosilimu: Watu wanaoingia katika dini ya Kiislamu wanastahiki kupewa zaka ili waweze kulingana na maisha yao mapya ya Kiislamu.

Wanaopatwa na maafa: Watu waliopatwa na maafa wanastahiki kupewa sehemu ya zaka ili waweze kufarijika dhidi ya maafa yaliyowapata.

Wanaoendeleza dini ya Kiislamu: Kila anayeshughulika na miradi ya kuiendeleza dini ya Kiislamu kama vile kufundisha, kujenga Misikiti, shule na hospitali anastahiki kupewa zaka ili kufanikisha malengo hayo.

Hitimisho:

Wataalamu wengi wa Kiislamu wameelezea umuhimu wa kuwa na chombo maalum cha kukusanya na kusambaza zaka badala ya kila tajiri kujitolea zaka kwa utaratibu wake binafsi, hali hii haipendezi wala haileti ufanisi mzuri katika kuuendeleza Uislamu.

Chanzo: An-nuur Na. 181
 
ANGALIA UNAVYOZUNGUKA KIVULI CHAKO MWENYEWE;
"lakini Kama unamaanisha shule za waislaam,basi nadhani zipo zinazofanya vizuri sana mojawapo ni feza"---HAPA NDIO NAANZA KUFAHAMU KUMBE KUNA SHULE ZA WAISLAAM ZINAZOFANYA VIZURI NA ZISIZO FANYA VIZURI.
"shule zisizofanya vizuri waende wakaone feza wanaweza vipi?"----OOH! KUMBE,SASA MBONA MNAWACHUKIA NECTA BURE TU,KUMBE TATIZO NI MANAGEMENT ZENU WENYEWE?.
MWISHO,KWAHIYO UNAWASHAURI WAMFUATE DK.MADATI ILI WASIWE WAMWISHO KILA MWAKA EEH! Basi msimchukie ndalichako na management yake wakati tiba ni kumfuata dk.madati wa feza awape mwongozo jinsi gani ya kupunguza div 0 na 4
 
Back
Top Bottom