FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #1,021
Shukran sana kwa ushauri mzuri.
1) Hivi Nchi za Rwanda, Congo, Burundi nk zilitawaliwa na France na Belgium kwa wakati mmoja au kwa nyakati tofauti au ikoje? Kwa nini ushawishi wa France kwa Mataifa hayo ni Mkubwa baada ya ukoloni kuliko Belgium kwa Mataifa hayo?
Naam, tuanze kwanza kuona kwa uchache historia ya karibuni ya ukoloni wa nchi hizo, tukianzia na Rwanda:
Rwanda
Ruanda- Urundi
Germany East Africa (Deutsch-Ostafrika) 1887-1914
Kumbukumbu za kihistoria zinaanza na utawala wa kifalme uliojulikana kama Ufalme wa Mwami (aka Mfalme) Rwabugiri .
Mzungu wa kwanza kufika Rwanda alikuwa ni Mjerumani, Count Von Gotzen ambae alitembelea medani ya Mwami Rwabugiri mnamo mwaka 1894, baada ya mwaka mfalme akafariki na kukaanza mvutano wa nani awe mrithi wa ufalme huo. Wakati Rwanda bado wapo kwenye kizazaa cha kushindania nani arithi, Wajerumani wakitokea Tanganyika, wakaingia nchini humo mwaka 1897 na kutangaza kuwa sasa huo ni utawala wa Kaiser wa Ujerumani.
Wakati huohuo wakatangaza (wakaamua) kuwa utawala wa Burundi nao ni wa Kaiser na ndipo pakajulikana kama Ruanda Urundi na kuwa Germany East Africa (Deutsch-Ostafrika), Rwanda, Burundi na Tanganyika.
Koloni la Ubelgiji (Belgium)
...Itaendelea