FaizaFoxy nikupongeze kujitoa kuelimisha watu kwa na kutoa maarifa kwa umma.
Pili, humu ndani kuna watu wa kila aina, namaanisha kila aina, vumilia na hiyo ni mojawapo ya sifa za ukomavu.
Nna maswali mawili tu,
1. Tukirejea uchaguzi wa marekani uliomalizika kwa ushindi wa Trump kuibuka kidedea, Hilary alipatikana na kashfa ya matumizi mabaya ya email account yake, amejitetea na FBI baadae wakasema kwamba hazikuwa na madhara yeyote.
Kwa mtazamo wangu, kama sheria na taratibu zinaelekeza wazi kwamba mawasiliano yote yafanyike kupitia email ya kiofisi, na kama alikiuka, hilo halikua tayari doa kubwa kumfanya ajiengue kwenye kimyang'anyiro cha kugombeaji urais?
2. Unashauri nini kwa wajasiriamali wenye nia ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao lakini wanakwama kwa kukosa maarifa ya namna ya kuendesha shughuli zao kitaalamu ili kuongeza uzalishaji na tija? (Hapa nalenga fursa za masoko ya ndani na nje, ubora wa bidhaa, changamoto na ufanisi kwenye uzalishaji, ubora na uimara wa vikundi/ushirika/umoja wa hawa wajasiriamali unaweza kutumikaje vizuri kuweza kuaminika na taasisi za fedha wapate mitaji ya shughuli zao?
Natanguliza shukrani za dhati