Hili ni tatizo la kujua machache ukafikili unajua mengi.Ni janga kwa wengi.Unaongelea vitu vingi na vikubwa vinavyohitaji uelewe mpana wa kiislamu.
Katika nchi ambazo si za kiislamu,Uislamu unaangalia utawala wa haki,kama kuna haki na watu wanaruhusiwa kuabudu dini inavyosema,waite demokrasia,ubepari,ujima nk dini haikupinga hili. Kuna nchi nyingi za ulaya na marekani zina sheria nyingi ambazo zimetajwa kwenye dini kuliko nchi zinazijiita za kiislamu; mfano haki za binaadamu.tafuta somo/kitabu cha 'makasida sharia' utaelewa zaid haya masuala,pia kuna mwanazuoni wa ki egypt kwa sasa yupo Canada anaitwa JASSER AUDA huyu ni msomi aliekubuhu na ni mwalimu wa sharia mfuatilie utajifunza mengi.
Salaam
Hili ni somo pana sana. Tunapolijadili tuwe makini tusichupe mipaka.
Ukitaka kujua tatizo liko wapi jaribu kufatilia toka kuanguka dola ya kiislamu. Dola ya kiuthmaan(daulat uthmaaniya). Ilianzisha jamaatul islaamiya ya Abuu Aala almauduud,baadae ikaja ikhwaanul muslimiin wote hawa lengo lao ni kusimamisha na kurudisha dola ya kiislamu. Wamekuja hizbu tahriir nao lengo likiwa hilo hilo.
Lakini jiulize kwanini hawafanikiwi?
Toka kuanguka dola ya uthmaan mwaka 1923 kama sijasahau hadi leo kwanini hawafanikiwi?
Mtume sala na salaam ziwe juu yake alitumia miaka 23 tuu kuweka misingi na kusimama dola ya kiislamu,kwanini sisi tunashindwa?
Ukiangalia kuna wanaotumia njia za kidemokrasia,wapo wanaotumia njia za vita lakini hakuna mafanikio.
Hii inamaanisha njia hizo zinazotumika si sahihi. Demokrasia ni njia tafauti tena yenye kupingana kabisa na misingi ya uislamu. Vita vinavyoitwa jihadi leo hii pia si njia sahihi ya kurejesha khilafa.
Tukitaka kufanikiwa ni lazima kwanza tujiangalie wapi tulijikwaa na kisha turejee kwenye njia sahihi aliyoipita Mtume wetu.
Dola ya kiislamu haitafutwi. Hakuna siku Mtume alisimama kupigania kuanzishwa dola ya kiislamu.
Bali yeye alifundisha tauhiid. Ilipokita kwenye mioyo ya watu wakaiishi hiyo tauhiid kimaneno na kimatendo. Wakawa waumini wa kweli. Allah akwapa zawadi ya kuwa makhalifa.
Hiyo ndio ahadi ya Allah kwa wale walioamini na kutenda yalio mema kuwa atawafanya makhalifa katika ardhi.
Hivyo tukitaka ukhalifa tuachane na demokrasia. Vita vya kijinga na makundi ya kishenzi kwa kisingizio cha dola ya kiislamu, kisha tupambane kuisimamisha tauhiid. Kisha watu wawe waumini wa kweli. Kikauli na matendo. Khilafa itasimama tena bila tone la damu