Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

shukhrann.

ok, back to the topic...

kandambili na njuti haziwezi kuoana.

ni kipi kinachokufanya usiolewe ila kuoana????

Kwa sababu kandambili na njuti haziwezi kuoana, kama ulivyojibu.

Mimi sijaolewa na mume wangu, tumeoana na ndiyo tukawa "pair" au kwa Kiswahili jozi au kwa Kiarabu "jawz".
 
Nilikuwa najiuliza sababu za kutokwa povu kiasi hicho..
Kumbe tatizo uarabu. Jitahidi uondoe maneno yote ya kiswahili yenye asili ya kiarabu.
Lakini kumbuka wazungumzaji halisi wa lugha ndio wanaoifahamu zaidi
Kutohoa maneno ya Kiarabu kuwa ya Kiswahili sio kigezo kuwa kiswahili ni Kiarabu.Maneno mengi ya kiswahili asili yake ni Kibantu.Kiswahili pia kina maneno ya kiingereza,kijerumani na kireno,lakini ni maneno ya kutohoa kama ilivyo kwa Kiarabu.Kwa hivyo kwa vyovyote vile kiswahili sio Kiarabu wala Kijerumani au Kiingereza.
 
Ni kweli ila neno lililotoholewa kutoka kireno,wazungumzaji halisi wa kireno ndio wanaojua zaidi matamshi sahihi ya neno hilo
 
Mbona uko selective sana ktk kujibu naona kuna maswali fulani yanapata kipaumbele sana kupewa majibu.
Wasiwasi wangu ni pale utakapotoa mrejesho mwingine kuwa unataka maswali yabadilike wakati maswali utakayoyahitaji huyajibu.

Ntarudi...
 
Hivi hili ulielewa kwenye post namba moja? :

"Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu. "
 
Nna shahada ya kwanza ya Electronics Engineering, Major in Telecommunications (Canada, 1982).
Nini umuhimu wa simu ya mezani hapa kwetu Tanzania kwa mfanya biashara (ofisi/kiwanda) na mtu binafsi(nyumbani) katika zama hizi za utandawzi na simu za kiganjani, ukitilia maanani magharibi bado wanazitumia kwa wingi
 
Mimi nnatumia sana nje ya Tanzania. Kwa mfano, ukitumia within Calgary simu za "mezani" ni bure, hakuna kulipia na zipo highly efficient hata kwa data transmission.

Kwa Tanzania sijui kama ni bure kwa sasa au zina gharama nafuu.

Besides, njia ya simu hizo za wires until recently zilikuwa zina uwezo wa data communications kwa haraka zaidi kuliko wireless.
 
Back
Top Bottom