Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Hebu nijaribu kuleta maana kwa Kiswahili, inasemaje?

Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambae hakidhuru kitu chochote Mbinguni wala Ardhini kutokana na jina lake. Nae Mwenyezi Mungu ni Msikivu na ni Mjuzi.

Kwa haraka haraka nikiangalia hii Dua inaingia kote, kote.

Nikiwa na maana, unamuomba Mwenyezi Mungu kuepusha na Mabalaa.

Kwahiyo kwa kumuombea Mtoto sidhani kama kuna chochote cha kubadilisha
Hukupatia ktk kufasiri neno "ma'a" huwezi kufasiri kuwa ni kutokana!!
 
Swala la Mali mamy n jingine inabidi utafte mwenye ilmu zaidi atakusaidia me nimekusaidia napopafaham kuhusiana Na kukomboa talaka
Dah... Hii ni simple tu.. . mlikuwa na mkataba wa ndoa na siyo ubia wa Mali...kama uliwekeza basi utapata kwa kiasi ulichowekeza... I love Islam nikaa so perfect and iko clear sana[emoji13] [emoji13]
 
Faizafoxy eti kwa tamaduni za dini ya kiislamu mwanamke hua anachaguliwa mchumba??

Uislam haukatazi mtu ku recommend mchumba kwa fulani. Mwisho wa siku anaeoa na kuolewa ndiyo wenye kauli ya mwisho ya kuoana.
 
Astaghfirullah, Astaghfirullah, Astaghfirullah.

Wewe jamaa acha kupotosha.

Nimeamua kupunguza kipengele cha pumba zako ili niparekebishe hapa kwanza, sababu naona mnataka kuupotosha Umma, kitu ambacho si cha kweli.

Kwa ufahamu wako, waingilieni mpendavyo, ndio wameruhusiwa kuingiliwa nyuma na mbele?

Hilo suluhisho umelitoa wapi?

Waingilieni mpendavyo inahusiana vipi na kuingiliwa nyuma na mbele?
Nimetoa hadithi acha kukurupuka kama hujui kaa kimya.
Ungekuwa msomi ungeitafsiri hiyo hadhithi kwamba inamapungufu haya ama la au inalenga hili au la sio kubisha bisha....... Unahatibu jukwaa hapa
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Update 1:
Tafadhalini tuulize maswali kiheshima . Heshima ni kitu cha bure na hii JF yetu pendwa inasomwa na wengi, tujiheshimu.

Update 2:
Siku kadhaa zimepita toka tuanzishe uzi huu na nimesikitishwa na aina ya maswali yanayoulizwa kwenye huu uzi.

Tumetowa fursa ya kuulizana na kila niwezapo kujibu au kutafuta majibu muafaka kutokana na hayo maswali na fursa ya wachangiaji kujibu maswali yatakayojitokeza ya "general knowledge" lakini hadi hii leo ni maswali machache sana yenye faida kwa wengi yameulizwa. Maswali yaliyojaa ni amma ya kutaka kuanzisha ubishi "ligi" na amma yamelenga mtu binafsi, hususan amelengwa mleta mada. Ni masikitiko makubwa sana.

Nnawashauri wote waliouliza maswali yenye kulenga binafsi na wale waliouliza maswali yenye kubomoa badala ya kujenga wabadilike na waanze kuuliza maswali yenye kujenga, kuelimisha, kutujaza hekima na maarifa.

Nilipoweka aina ya elimu niliyoisomea nilidhani ntakumbana na kibano kikali kuhusu hilo na nijibu ili iwe faida kwa wengi lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna hata mmoja aliyeuliza swali lolote kuhusu hilo.

Isitoshe, mna fursa ya kuuliza kuhusu chochote. Ndege, mimea, dunia, sayari, nyota, maajabu, maswali yasiyokuwa na majibu, viumbe kwa ujumla vinavyojulikana na visivyojulikana, maajabu ya duniani, elimu na vitu vingi kama hivyo na vinginevyo.

Nnauhakika wale walioleta maswali ya kiajabu ajabu ya ubishi wana mengi sana ya kuuliza yanayoweza kuwapa faida wengi na kuna wengi kati yao wana mengi wanayajuwa na wanaweza kuchangia kwenye majibu kwa faida ya wengi.

Ombi langu kwa wote ni tuboreshe aina ya maswali na majibu.

Karibuni.
( الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ )

الحج (40) Al-Hajj

Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.

AYA HII NI YA KWELI?
 
Weka link ya source.
 
Ni sahihi, tena sana.

Hapo kama nilivyosema, inaingia kote kote.

Nikiwa na maana,

Ukijiombea wewe Mwenyewe ni sahihi, na ukiwaombea Watoto ni sahihi pia.

Lengo kuu hapo ni kumuomba Mwenyezi Mungu akuepushe na Mabalaa yote, kwa kuyataja machache ikiwemo Shirki, Labda Ndoto za ajabu ajabu, kuweweseka.

Kwahiyo kwa kumuombea Mtoto inafaa sana, kama nilivyosema Mabalaa yote, pia HUSDA inahusu sana hapo.

Kama ujuavyo, Watu wana HUSDA sana linapokuja suala la Watoto.

Unafanya vyema sana.

ALLAH akubariki sana, akulinde, na akufanyie wepesi kwa kila jambo lako InshaAllah
Shukraan sana rihaa. [emoji1]
 
Weka link ya source.
Faizafoxy
Nataka kujua tu kama aya hii ya Quran inaukweli wowote ndani yake au haina ukweli wowote kulingana na uana zuoni wako.
Wakati huo naomba pia utoe ufafanuzi wa aya hii

( إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ )

المائدة (69) Al-Maaida

Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
 
Usiwe na wasi wasi, ondoa hofu. Hizo utajibiwa amma na mimi amma na mchangiaji mwengine yeyote, hii ni open forum.

Nilichokuomba mimi ni link ya source ya uliyobandika hapa.
 
Kajirutaluka heshima kwako, nipo ndani ya swala kabla imam kutoa salam, ushuzi ukanibana, naweza toa salam kabla imam ili swala ikamilike , maana nikimsubiri imam sitofika, mkuu unapojibu jaribu ku- quote kwa kutumia swali
 
Unatakiwa uwende uwani ukatoe hewa chafu.mkojo.hajakubwa kabla hujachukua udhu na kuanza kuswali.
Huwezi toa asalam kabla ya imam hairuhusiwi kumtangulia imam lazima umfate.
Utakacho Fanya ni kukata swala na hapa humsubirii imam. Unakatacswala na unaenda chukua udhu upya. Ukirudi kama imam kashatoa salam unaanza kuswali upya. Kama bado unaunga alipo na kulipa rakaa alizo kwisha swali.

Rakaa za mwanzo hazitambuliki.zishafutika.

Ikitokea umetokwa na udhu kwa njia au kitu chochote ukiwa ndani swala itakubidi ukatize swala ukajitwaharishe tena.

Allah sw anajua zaidi. Karibu
 
Back
Top Bottom